Job Ndugai anaweza kushitakiwa Mahakamani ?

Erythrocyte

JF-Expert Member
Nov 6, 2012
125,745
239,398
Wakuu poleni na msiba wa Mzee Ndesamburo ( RIP )

Mimi si mtaalam wa mambo ya kisheria , lakini nafahamu kwamba katika Tanzania hakuna aliye juu ya sheria .

Je kitendo cha Job Ndugai kusimamia maamuzi ya kiharamia ya kuwafungia wabunge wa Chadema , Halima Mdee na Easter Bulaya kwa vikao vyote vya bunge , hadi bunge lijalo la bajeti hakiwezi kumfikisha Mahakamani hadi kupelekea kufungwa jela ?

Wito kwa Chadema - siasa za Tanzania ni sawa na mapambano ya waafrika na makaburu kule South Afrika hivyo msitegemee siasa laini , pambaneni kwa njia zozote .
 
Japo wapinzani hawajawahi kufungua kesi ya namna hii, nadhan wakati muafaka umefika sasa wa wao kufanya hivyo. Wafungue kesi ya kikatiba dhidi ya Spika kwa kosa la kuwanyima fursa ya uwakilishi wananchi wa majimbo yaliyoathirika.
 
True , na nina hakika wako Majaji ambao ni wazalendo ambao wanaweza kumtia matatani Ndugai , ikumbukwe kwamba maamuzi mengi anayotoa si maamuzi ya Uspika wake , ni maamuzi ya Job Ndugai .
 
Ha ha haaaa
Mbona spika kaliongelea hilo.... hamumpati hata kidunchu. Kama kawaida ya kutafutia kiki mliyozoea nendeni mahakamani mkapoteze muda, waende wakahudumie wananchi wao sasa wana muda.
 
Kwani hakukuwa na adhabu tofauti na hiyo, maana hapo humkomoi Halima Mdee na Esther Bulaya bali umawakomoa wananchi waliompa dhamana ya kuwawakilisha.
Nafikiri Ndugai atakuwa na kichuki fulani hivi.
 
duh, yaan pesa zetu za chama zitumike tena kwenda kusimamia kesi mahakamani?? inatosha sasa, pesa za ruzuku zitumike kwa mambo mengine! bulaya na mdee wavumilie tu mwakani sio mbali
 
Kwani hakukuwa na adhabu tofauti na hiyo, maana hapo humkomoi Halima Mdee na Esther Bulaya bali umawakomoa wananchi waliompa dhamana ya kuwawakilisha.
Nafikiri Ndugai atakuwa na kichuki fulani hivi.
Mbona kuna wabunge wawakilishi wa majimbo yao, hukaa mjengoni na hawachangii hoja! na bado kila uchaguzi ni wao tu! so kukaa nje ya jengo huenda hakuna uhusiano wowote na wana-jimbo, kwa maana ya kuwakomoa!! Napita tu
 
Mkuu;
Swali nataka kukujibu hivi;

Labda kwa mahakama nyingine ila sio hizi za kikwetu. Naona kila mhimili umesha jichanganya kabisaaa. Kila mkuu wa mhimili ulee anachunguzwa kama ana cheti cha chama tawala na kama huwa anakilipia na kama anakubaliana na fikra sahihi za m/kiti wake.

Hivyo; kwa Spika wetu kufunguliwa mashitaka hapa hapa nchini ni sawa sawa na tumbili kwenda kumshitaki sokwe kwa ngedere kuwa mtoto wa sokwe ni mtukutu na anawafanyia vitu vibaya watoto wa tumbili.
Hapo hakuna hukumu yeyote itatolewa na ngedere.

Kwa kuwa karatasi zipo na mawakili wa chama wapo, basi waende. Kama ingelikuwa, ni mwanasheria mkuu anaenda kumshitaki spika, nadhani ningelikuwa na tumaini hapo.

Kama tulisikia Loud and clear; sauti ikitoka kuwa; Mnyika ni mwiziiiii. Halafu spika anasema hana masikio 100 ya kusikiliza kila sauti.

Nadhani tufikiri vingine. Naona hiyo adhabu imetolewa vibaya. Wangewafukuza ubunge, wakitaka waende kuomba upya huko majimboni, halafu Spika atangaze kuwa majimbo hayo hayana wawakilishi. Sio kuwanyima uwakilishi wananchi.
 
Naina mnatafuta njia ya kula ruzuku...kama vile namuona lissu na kibatala wanacheeeka
 
Yaani kwa kitendo cha hiyo inayoitwa Kamati ya maadili ambayo inasemekana almost 95% ni wabunge wa CCM kumwadhibu Mnyika kwa kufungiwa kutohudhuria vikao vya Bunge hadi mwakani eti kwa 'kosa' la kumwomba tu Spika amwombe Mbunge mwanamama wa CCM aliyewasha mic na kumwita Mnyika mwizi kuwa aidha afute kauli yake au athibitishe wizi wa Mnyika........

Sasa Kamati ya maadili imekuwa 100% biased kwa kuwachukulia hatua Mnyika, Halima Mdee na Esther Bulaya walioamua kuprotest maonevu hayo ya dhahiri kwa wabunge wa upinzni kwa kuwafungia kutohudhuria vikao vya Bunge hadi mwakani na kumuacha bila kumchukulia hatua yoyote Mbunge 'mwenzao mtukutu' wa CCM aliyemwita Mnyika mwizi!

Hakika maovu yanayofanywa na Spika Ndugai akishirikiana na wabunge wenzake wa CCM hata shetani atakuwa anawashangaa, kwa kuwa kiwango hicho cha uonevu ni wa kiwango vya juu sana ambacho hata shetani mwenyewe hawezi kukifikia!
 
pambaneni kwa njia zozote .
MKUU EBU TOA HIYO ID FAKE YAKO...afu ndio uhimize hicho unacho wadanganya wenzio.......WENZIO WANAOGOPA KUFANYA UNACHO WADANGANYA MAANA WANA REAL IDENTITY.....sasa wewe upo shimoni unawadanganya wenzio
 
Mbunge hashtakiwi mahakamani kwa kosa alilofanya akiwa ndani ya bunge (sio jinai)
 
Wakuu poleni na msiba wa Mzee Ndesamburo ( RIP )

Mimi si mtaalam wa mambo ya kisheria , lakini nafahamu kwamba katika Tanzania hakuna aliye juu ya sheria .

Je kitendo cha Job Ndugai kusimamia maamuzi ya kiharamia ya kuwafungia wabunge wa Chadema , Halima Mdee na Easter Bulaya kwa vikao vyote vya bunge , hadi bunge lijalo la bajeti hakiwezi kumfikisha Mahakamani hadi kupelekea kufungwa jela ?

Wito kwa Chadema - siasa za Tanzania ni sawa na mapambano ya waafrika na makaburu kule South Afrika hivyo msitegemee siasa laini , pambaneni kwa njia zozote .

Ni vigumu sana
Kinachoamuliwa au kuzungumzwa bungeni hakiwezi kuhojiwa popote.

Ndio maana chadema walikuwa wana uwanja mpana sana wa kutukana viongozi wakiwemo ndani ya bunge.

Ndio maana chadema walishindwa kupinga mahakamani uchaguzi wa EALA kama walivyotudanganya.

Hao si wabunge wa kwanza kufukuzwa,hata zitto aliwahi kufungiwa na chadema haikwenda mahakamani

Kwa lolote lile linalohusiana na Bungeni,mahakama imefungwa mikono
 
Ha ha haaaa
Mbona spika kaliongelea hilo.... hamumpati hata kidunchu. Kama kawaida ya kutafutia kiki mliyozoea nendeni mahakamani mkapoteze muda, waende wakahudumie wananchi wao sasa wana muda.
Kanawe ule
 
Back
Top Bottom