Job Description hazitolewi na waajiri wengi | JamiiForums | The Home of Great Thinkers

Dismiss Notice
You are browsing this site as a guest. It takes 2 minutes to CREATE AN ACCOUNT and less than 1 minute to LOGIN

Job Description hazitolewi na waajiri wengi

Discussion in 'Jukwaa la Sheria (The Law Forum)' started by Satanic_Verses, Jun 7, 2012.

 1. S

  Satanic_Verses Member

  #1
  Jun 7, 2012
  Joined: Sep 6, 2011
  Messages: 37
  Likes Received: 0
  Trophy Points: 0
  NI kwa nini employers wengi wanavunja sheria ya kazi kwa kutotoa orodha ya kazi za mwajiriwa yaani Job Description.

  Mimi napendekeza watumishi wa idara ya kazi waanzishe mtindo wa kuzunguka kwa employers mbalimbali hapa nchini na ndipo watagundua madudu yaliytojazana huko.

  Mtu anafanya kazi lakini kesho unambiwa kabadilishiwa bila kufuata utaratibu. Utaratibu ni kwamba unapokuwa na job description, basi mwajiri hatakiwi kukubadilisha kazi bila kwanza kushauriana na wewe.

  Ujanja wanaotumia waajiri ni kutumia ujinga wa employees wengi ambao kwao kupata ajira ni baraka tosha kiasi kwamba kuuliza mambo ya Job Description ni kujitakia kuonekana kilomolomo ambapo siku hizi waajiri wanaepuka kufukuza bali wanakuacha hapo ulipo ili uwe bored na uache kazi mwenyewe kwa sababu mshahara haupandi wala cheo hakipandi.

  Kwa waajiri ambao wameingia nchini kutokea nje wao wanatumia mtindo wa kuleta watu kutoka nchini mwao waje kujaza nafasi ambazo hata watanzania wanaweza kuzifanya.

  Bahati mbaya watanzania kama nilivyosema wengi hawajui kulidai hili kwa kupitia Job Description. Kwamba kwa sababu hawapewi Job Description, basi inakuwa si rahisi kumbana mwajiri kwamba mbona kazi namba fulani siku hizi hunipi na badala yake unampa yule foreigner.

  Wanasheria na watu wa idara ya kazi, tunaomba muangalie hili maana mtakuta mmesaidia wengi kuliko mnavyodhani. Wabunge pia tunaomba mlitizame hili.

  Taifa linateketea kwa uvunjifu wa sheria kwa waajiri wa aina hii ambao ni wengi
   
Loading...