JMP ni msema kweli na si mnafiki?

Genghis Khans

JF-Expert Member
Dec 5, 2015
502
462
Rais wangu ni mtu makini sana kwenye number na siku zote anasema msema kweli ni mpenzi wa mungu na ni bora kuwa kukaa na mchawi kuliko mnafiki.

Lakini juzi nimemsikia akasema 99.999% ya mapolisi wako safi. Sithani huu ni ukweli. Tukifanya polygraph kwa police wote nchini 99.999% ya watakuwa sio wasafi.

Sithani kuhamisha wakuu wa police ni kusafisha jeshi wakati bado wako ndani ya police. Kama kweli wanataka kulibadili jeshi hili inabidi wawetayari kutumbuana majipu pale kwenye matatizo.
 
Rais wangu ni mtu makini sana kwenye number na siku zote anasema msema kweli ni mpenzi wa mungu na ni bora kuwa kukaa na mchawi kuliko mnafiki.

...kutumbuana majipu pale kwenye matatizo.
Nimesikia wadanganyika huku mtaani wanasema, " Kitu ambacho Mwanasiasa anasema kweli ni jina lake tu"
Mtumbua "majipu" ni mwanasiasa?

Nilisikia wadanganyika wanasema wanataka Rahis dikteta badala ya chekacheka. Dikteta hutenda na kusema atakacho, kwa kawaida msamiati wa msema kweli au mnafiki hautumiki tena baada ya siku 100 za utawala. Baada ya siku 100 mwansiasa anayehamia Ikulu hugeuka "malaika".
Malaika hutukuzwa tu. Malaika hakosei.

Ujumbe wako utamfikia Rais wako, Rais makini ambaye anakaa na wachawi na anayeepuka wanafiki.

Nikukumbushe kitu moja tu, uanasiasa na unafiki ni "ndugu pacha".

Siasa ni nini?
Wakisema demokrasi wanamaanisha Domo-krasi.

Kulingana na uzoefu wangu wa wanasiasa wa Nchi yetu, wametudanganya sana kwa miaka 50+. Tuliwaamini sana, walitwambia tukaze mikanda, tuliikaza. Walitwambia ujamaa, tulipanga foleni kugawiana umasikini, walitwambia ruksa, tukaamua kula panya, walitwambia utandawazi na ubinafsishaji, tukaamua kuwa wabinafsi na kuwa wajasirimali, walitwambia wanatuletea maisha bora, wakawa wanapanda mapipa na kutuletea "tabasamu na vicheko", wameingia wasema ukweli na watumbua majipu, tumekuwa watukuzaji na wasifia watu tu huku bei ya sukari ikizidi "kushuka na kudidimia". Tutajiramba kama wala asali.

CCM ina kila mbinu ya kumtawala mdanganyika. Jitayarishe kutumbuliwa. Mtu zote zimekuwa waoga, zinaogopa kutumbuliwa.

Msema kweli ni mpenzi wa Mungu, tusema ukweli hata kama wanafiki watachukia.
 
Back
Top Bottom