ccm hawatumii akili, wao hawajui matokeo ya migomo ni watu kuzitambua haki zao, wanafikiri ile karne ya 19 JKT ilikuwa suluhisho la nidhamu kumbe hapana woga na vitisho vya kupotezwa bila kujua ulipowekwa na kufungwa vifungo vya nyumbani kwenu ndivyo viliwafanya watu wanyamaze huku wanaumia, hii karne watu wameamua lazima nipewe sababu ni haki yangu wao wanaenda kuwavuruga vijana kwenye matope na kuwapa mafunzo ya kupanda mboga wanajisifu wanafundisha uzalendo. Waache ufisadi wawape watu haki zao ndio mwisho wa migomo. Hela ipo mtoto wa maskini hapewi hela ya kujikimu chuoni, akigoma leo kesho hela imetoka sasa ni akili gani hii? Au ndio walikuwa wanapima kama somo la uzalendo walilowafundisha JKT limewaingia? Jibu ni kuwa wamefeli hao wenye mawazo mgando ya kuwafunga watu midomo.