JKCI yaweka mshipa bandia kwenye moyo

elivina shambuni

JF-Expert Member
May 31, 2018
461
295
1573582207170.png

KWA mara ya kwanza madaktari bingwa wa upasuaji wa moyo kwa watoto katika Taasisi ya Moyo ya Jakaya Kikwete (JKCI), wamefanya upasuaji wa kutenganisha mshipa wa kusambaza damu kwenye mwili na kuweka mshipa bandia wa kusambaza damu kwenye mapafu.

Upasuaji huo uliochukua muda wa saa nne na nusu, ulifanyika kwa mtoto mwenye umri wa miezi mitano ambaye alikuwa na tatizo la damu safi na chafu kutokea kwenye mshipa mmoja wa damu badala ya mishipa miwili tofauti.

Mtoto huyo alizaliwa na tatizo la kuwa na mshipa mmoja wa damu ambao ulikuwa unapeleka damu kwenye mwili na mapafu kutoka kwenye moyo badala ya mishipa miwili ya ‘Aorta’ ambao unapeleka damu kwenye mwili na ‘Pulmonary Artery’ ambao unapeleka damu kwenye mapafu.

Akizungumza na waandishi wa habari jijini Dar es Salaam, daktari bingwa wa upasuaji wa moyo kwa watoto wa taasisi hiyo, Godwin Sharau, alisema wametengeneza mshipa wa damu bandia ambao unabeba damu chafu kutoka kwenye chumba cha chini cha kulia cha moyo na kupeleka kwenye mapafu ili kutenganisha damu chafu na safi. “Katika upasuaji huo tumefanikiwa pia kuziba tundu la moyo na kulitenganisha kutoka kulia na kushoto ili kusaidia mzunguko wa damu kuwa katika hali ya kawaida.

Mshipa huu bandia utadumu kwa muda wa miaka 10 hadi 15 baada ya hapo utabadilishwa na kuwekwa mkubwa zaidi tofauti na wa sasa ambao ni mdogo,” alisema. “Aina hii ya magonjwa ya moyo ni nadra sana kutokea, lakini katika mazingira yetu tumekuwa tukiwaona watoto wenye matatizo kama haya na watoto kama hawa wasipopata matibabu ndani ya Alisema wawili walifanyiwa upasuaji katika kambi maalum ya matibabu ya moyo ya wataalamu kutoka Italia na Ujerumani na huyu wa sasa amefanyiwa na madaktari wazawa wa taasisi hiyo.

Neema Amani, mama wa mtoto aliyefanyiwa upasuaji huo, alishukuru kwa huduma ambayo mtoto wake alipatiwa na kuwaomba wazazi wengine ambao wataona watoto wao wana matatizo ya afya, wasikae nao nyumbani wawapeleke hospitalini kwa ajili ya matibabu. Alisema Septemba, mwaka huu, alipewa rufani kwenda kutibiwa JKCI kutoka Hospitali ya Rufani ya Mkoa wa Kinondoni ya Mwananyamala baada ya kugundulika kuwa na tatizo la moyo.

Kwa mujibu wa mama huyo, mtoto alikuwa na shida ya kubanwa na kifua, kukohoa na kutokwa na jasho jingi hasa wakati wa kunyonya. “Naishukuru sana taasisi hii kwani mwanangu hana bima ya afya na sikuwa na pesa ya kulipia matibabu ya moyo.

Lakini mwanangu amepatiwa matibabu na sasa anaendelea vizuri na ameruhusiwa kutoka katika chumba cha uangalizi maalum,” alisema. JKCI imekuwa ikifanya kambi maalum za matibabu ya moyo kwa kushirikiana na wataalamu kutoka nje ya nchi na miongoni mwa manufaa yaliyopatikana katika kambi hizo ni kubadilishana ujuzi wa kazi na mafunzo ambayo yamewasaidia wataalamu wa taasisi hiyo kupata elimu na utaalamu wa kisasa na wa hali ya juu.
 
View attachment 1261618

Nawaheshimu sana Madaktari na kada zake!!
Hongera kwao
 
Back
Top Bottom