JK vs Lowasa: Dhana ya Maamuzi Magumu

JK vs Lowasa: Dhana ya Maamuzi Magumu

Maswala

JF-Expert Member
Joined
Feb 28, 2011
Posts
560
Reaction score
226
Wana JF,

Lowasa amekuwa akiinyanyasa serikali ya Kikwete kuwa hawezi kufanya maamuzi magumu, akilenga changamoto mbali mbali zilizokuwa zikijitokeza utawala wake.

Siku chache baadae Lowasa alikumbushwa uamuzi juu ya sakata la Richmond, lakini akapuuza.

Sasa kwa mara nyingine JK kamdhihirishia kuwa naweza kufanya maamuzi magumu; tena maamuzi yake magumu yanauma kweli kwa sababu yanauza ndoto za wengine, akiwemo yeye Lowasa.

Pamoja na kwamba mimi siishabikii CCM, nawapongeza kwa kutegua kitendawili kigumu cha urais uliosakwa kwa udi na uvumba, kwa mabiliona mengi ya fedha, kuwapiga chini wote waliotumia pesa! Mwisho wa siku ingebidi hao jamaa wapewe "Richmond" na ni wananchi tungeishia kuumizwa.

Natumaini mtabadili pia mfumo, muondeshe ufisadi, japokuwa hilo ni kitendaiwili kigumu, kwa maana ufisadi ndani CCM ni tatizo la kimfumo zaidi. Akioza samaki mmoja, samaki wote wanaoza!

Nakuomba sana Mh Magufuli, ukifanikiwa kuwa rais wa nchi hii, mbwembwe zako ulizozionyesha ukiwa waziri kuleta nidhamu ya kiutendaji zitasirike juu ya serikali yako, ambapo kwa sasa utendaji ni mbovu sana, umejaa rushwa, kujuana, milango ya nyuma n.k.

Pia utahitaji kufanya maamuzi magumu mno kulifanikisha hilo! Nakuomba uanze kwa kuteua sura mpya zaidi kuliko kurudisha wale wa zamani! Pia usiwaonee haya watendaji mbali mbali na waajiliwa wa serikali ambao etendaji wao hauridhishi, na ama wala rushwa!

Hicho ni kitendawili kingine, ambacho labda maamuzi yake ni magumu kuliko ya "Richmond", "ESCROW", na kukata jina la mgombea 1 maaurufu ktk mchakato wa kumpata mpeperusha bendera wa CCM. Maana kinahusu kuharibu mfumo rushwa, uzembe kazini, kujua n.k. Kazi ambayo itawagusa wengi.
 
Alidhani ananguvu kuliko chama na hapo ndipo kunatofauti kati ya pwani na bara
 
JK amefanya maamuz magumu chamani kwake ila si kwenye serikali yake.Utawaambiaje wez rudishen pesa,then wasishtakiwe???
 
Back
Top Bottom