Elections 2010 jk,umesema vizuri lakini ???

fige

JF-Expert Member
Jul 4, 2010
376
0
Siku zote binadamu dhamira mara nyingi huenda tofauti na matendo.Haya yalishamkuta mfalme Suleiman yule binadamu anayesmwa kwenye vitabu vitakatifu kuwa na hekima sana, hata siku moja akasema 'jema ninalitamani silitenda bali hutenda baya'.
Nadhani haya ndiyo yanayomkuta Raisi wetu kwani anatamani hiki lakini hutenda tofauti kwani mara nyingi hufanya kinyume na yale anayoyasema, raia tukiamini kuwa anachokisema ndicho anachoamini.

Mfano ni vita juu ya ufisadi. kupitia serikali yake, Mramba ana kesi mahakamani lakini kupitia chama chake Mramba ni mtu safi
Anayestahili kuwa mbunge.

Naogopa zaidi pale anapokemea ukabila wakati anasifu familia kumpigia debe wakati wa uchaguzi.Nadhani amesahau kuwa kabila huanza na familia huwa ukoo na kisha kabila, na dini tulio wengi tumerithi kwenye familia zetu.

Katika maisha ni vizuri sana kujua mapungufu yako, lakini ni mbaya kuliko kuyajua na kutofanya chochote kubadilika.

Watz tumeendelea na kibwagizo cha AMANI na wakati tunafanya mambo yanayoweka vidonda hatimaye makovu ya amani yetu .Tukiendelea kuwekeana vidonda kuna siku havitapona kwani inawezekana tukawa na kisukari sugu (kama vile ufisadi ).Na hata vikipona vidonda huacha makovu, na makovu hayaponi.Tabia ya makovu kila baada ya muda fulani huwasha.
Wito kwa kiongozi na watz wenzangu na hasa viongozi wetu:
MSINGI WA NCHI YETU NI WA NONDO NA ZEGE, TUSIJENGE KUTA ZA TOFALI ZA BARAFU.
TUJITAHIDI KUTENDA SAWA NA MANENO YETU.
 

Toa taarifa ya maudhui yasiyofaa!

Kuna taarifa umeiona humu JamiiForums na haifai kubaki mtandaoni?
Fanya hivi...

Umesahau Password au akaunti yako?

Unapata ugumu kuikumbuka akaunti yako? Unakwama kuanzisha akaunti?
Contact us

Top Bottom