Jk tumia mamlaka yako sasa! | JamiiForums | The Home of Great Thinkers

Dismiss Notice
You are browsing this site as a guest. It takes 2 minutes to CREATE AN ACCOUNT and less than 1 minute to LOGIN

Jk tumia mamlaka yako sasa!

Discussion in 'Habari na Hoja mchanganyiko' started by mzee wa inshu, Feb 19, 2011.

 1. m

  mzee wa inshu Member

  #1
  Feb 19, 2011
  Joined: Jan 25, 2011
  Messages: 49
  Likes Received: 1
  Trophy Points: 0
  Ndugu JK, nadhani sasa ni wakati muafaka kwako kutumia madaraka uliyo kabidhiwa na wananchi kama mkuu wa nchi, kiongozi wa serikali na amiri jeshi mkuu wa majeshi yote.

  Tunatarajia,kwa hili la gongolamboto waziri wa ulinzi na mkuu wako wa majeshi hutaruhusu kwa mara nyingine waendelee kuvutavuta sharubu zako.

  Ninaamini uwezo, nguvu na sababu za kuwachukulia hatua wazembe hawa unazo ila tatizo ni kwamba nia huna!

  Mh, inakuwaje wanauwa wananchi kisha wanatutunishia misuli ya kwamba hawawezi kujiuzuru? Hawa watu wanajivunia nini,kiburi wanakipata wapi? kama si dharau kwa wananchi ambao ndio wnaokufanya wewe uitwe rais?

  Kama kweli wananchi walikupa sauti ya kuongea na na nguvu za kutenda kwa niaba yao, mbona unawasaliti sasa? Unatufanya tuamini kuwa yawezekana ni kweli kwamba urais ulijipa mwenyewe na si watanzania ndio mana unafanya mambo kivyako kwa masilahi yako na rafiki zako na sio watanzania. Au ndo mtindo wa kusitiriana?

  Wang'oe hao watu kwanza ndio tuanze kuongea biashara nyingine na wewe la sivo hatukuelewi, na hueleweki kabisa mkuu!

  KIMYA KINGI..........................!
   
 2. d

  dorry Senior Member

  #2
  Feb 19, 2011
  Joined: Feb 2, 2011
  Messages: 136
  Likes Received: 1
  Trophy Points: 33
  Ndugu yangu kwani umeshasahau kuwa urais ni suala la familia? Nini tena afanye - familia mambo safi, marafiki kili siku ni sherehe. Waliojipendekeza kumchagua hawakuelewa ana maana gani? Pigieni mistari majibu.
   
Loading...