JK, Serikali ya CCM yazinduka!

Lasikoki

JF-Expert Member
Joined
Jan 10, 2010
Messages
642
Points
0

Lasikoki

JF-Expert Member
Joined Jan 10, 2010
642 0
WanaJF, Salaaam!

Jana nilipata fursa ya kusikiliza hotuba ya JK kwenye Baraza la Idd ambapo alitumiwa jukwaa lile kujibu baadhi ya "masuali magumu" ambayo hakika yamekuwa yakifanya liwepo ombwe la uongozi na utashi wa kisiasa kuyasemea mambo magumu katika nchi yetu.

Kwa ufupi hotuba ile ilikuwa nzuri tena ifaayo kutoka kwa kiongozi wa nchi. Hata hivyo nilijikuta nina maswala mengi kichwani, tena kila swali likizaa tafakuri nyingine na cycle iliendelea hivyo hivyo..........then back to square one. Swali la msingi ni je CCM wakati wanaomba kura na idhini ya kushika dola hawakujua kuwa suala la mahakama ya kadhi ni la kidini zaidi, na kwamba dini ya kiislam na taasisi zake ndizo zenye jukuma maridhawa la kuunda na kusimamia? Je, CCM haikujua kuwa serikali haina dini? Je, hawakujua kuwa kuchanganya dini na siasa, tena siasa uchwara ni hatari sana kwa amani na mshikamano wa nchi au jamii yeyote ile?.

Sitaki kuamini kwamba CCM haikujua majibu ya haya maswali marahisi, ninachoamini ni kuwa CCM imewatumia, imewahadaa, imewadhihaki na kuwadhalilisha waislamu. Tena baada ya kupata walichotaka wakawatupilia mbali waislamu, kama used pad. lLakini the worse part of the issue ni kwamba hata na wao waislamu walikubali kutumiwa na CCM, walikubali kucheza ngoma na CCM, this is very pathetic indeed!

Hayo tuyaache, Je kitendo cha JK kuzungumza haya maneno mazito kwenye dhifa kama ile inaweza kuwa ndio wanatekeleza kaulo mbiu yao ya kujivua gamba? Nakumbuka Nape aliwahi sema kujivua gamba unalenga katika kubadili upya mfumo na fikra za chama katika mambo ya msingi......

lakini pia leo nimesikia through TBC SUMATRA imelifungia gari la CHAMPION kutoa huduma zake baada ya ajali maeneo ya DODOMA, hapo hapo JK kaahidi kusafirisha maiti za waliokufa hadi makwao kwa gharama ya serikali........kwangu mimi this is new phenomenon, kwani ajali huwa zinatokea nyingi lakini SUMATRA na SERIKALI kimyaaa...... kulikoni?......"MASWALI MAGUMU " ni je JK na serikali yake ndio wanaanza kujivua gamba au?

I'm just curios, What is your view?​

Nawasilisha.
 

Forum statistics

Threads 1,356,388
Members 518,903
Posts 33,131,796
Top