JK: Ridhiwani hahusiki kuondolewa Bashe | JamiiForums | The Home of Great Thinkers

Dismiss Notice
You are browsing this site as a guest. It takes 2 minutes to CREATE AN ACCOUNT and less than 1 minute to LOGIN

JK: Ridhiwani hahusiki kuondolewa Bashe

Discussion in 'Uchaguzi Tanzania' started by Quinine, Aug 20, 2010.

 1. Quinine

  Quinine JF-Expert Member

  #1
  Aug 20, 2010
  Joined: Jul 26, 2010
  Messages: 10,936
  Likes Received: 12,207
  Trophy Points: 280
  MWENYEKITI wa Chama Cha Mapinduzi(CCM) Taifa, Rais Jakaya Kikwete amesema hana tatizo na wanachama wa chama hicho wanaohamia vyama vingine,lakini wasijaribu kukihujumu.

  Kikwete amesisitiza kuwa,walioenguliwa na Halmashauri Kuu ya Taifa (NEC), wataelezwa kwa maandishi sababu za kuenguliwa.


  Aidha amesema,mwanawe Ridhiwani hahusiki katika sakata la kuenguliwa kuwania ubunge Jimbo la Nzega, Hussein Bashe kama ilivyoripotiwa kwenye baadhi ya vyombo vya habari.


  Rais Kikwete aliyasema hayo Dar es Salaam kwenye Ofisi Ndogo za Makao Makuu ya CCM, Mtaa wa Lumumba, wakati akiwahutubia mamia ya wanachama wa chama hicho mara baada ya kurejesha fomu zake za kuwania Urais kwa Tume ya Taifa ya Uchaguzi (NEC).


  Alisema,wakati wa kura za maoni, wengi walijitokeza kugombea, lakini lazima mmoja ashinde na wengine washindwe, lakini wapo waliogombea kwa kutaka washinde wao na hao ndiyo ambao sasa wanahamia vyama vingine.


  "Katika uchaguzi lazima mmoja ashinde. Tatizo kuna wagombea waliingia katika ushindani ili wao tu washinde, hiyo ndiyo sababu ya kutaka kuhama…anayehamia kwingine sina haja naye, aende anakotaka, mbaya ni kukihujumu chama," alisema Rais Kikwete jana.


  Alisema hata kama aliyegombea hakuridhishwa na mazingira ya namna aliyeshinda alivyoshinda, ndiyo ameshapata,hivyo jambo la msingi ni kuacha makundi yaliyokuwepo wakati wa kura za maoni, bali wajielekeze katika kutafuta ushindi wa kishindo huku wakijiandaa kwa kugombea kipindi kingine.


  Kikwete alisema,utaratibu huo wa kura za maoni utaendelea ingawa mchakato ulikuwa na changamoto mbalimbali ambazo wamejifunza na kuwahakikishia kuboresha mapungufu yaliyojitokeza ili yasitokee na wanaendelea kuzichambua kasoro hizo na baada ya uchaguzi watazifanyia kazi.


  "Pamoja na mapungufu yaliyojitokeza, mamlaka tuliyowapa wanachama wa CCM hatutawanyang'anya, ila jukumu ni kurekebisha kasoro zilizojitokeza kwani imesaidia kuwapata wagombea wanaohitajika huku wakijitokeza wanachama wengi kugombea nafasi mbalimbali," alisema.


  Kuhusu Bashe, Mwenyekiti huyo wa CCM Taifa alisema kuenguliwa kwa kijana huyo kulifanywa na Kamati Kuu ambayo ilifanya hivyo kwa manufaa ya chama.


  Alisema Kamati Kuu hiyo ilijitahidi kuheshimu uamuzi ya wanachama wake, lakini kutokana na sababu mbalimbali kama uraia na utovu wa maadili ambao ungesababisha chama hicho kuanguka katika jimbo husika, walimteua wanayeona anafaa.


  Alisema kuna magazeti yanasema maneno mengi ili wanachama wa chama hicho wachukiane na yakishindwa kuona mema ya chama hicho kwa mwaka mzima.


  Aliwaomba Makamu wake, Pius Msekwa na Katibu Mkuu, Yusuf Makamba kuacha kujibizana katika magazeti, badala yake, majibu yatapatikana katika kura baada ya CCM kushinda kwa kishindo.


  Bashe ambaye alikuwa Mjumbe wa Baraza Kuu la Umoja wa Vijana (UVCCM), alienguliwa na Kamati Kuu baada ya kubainika kuwa si raia wa Tanzania, na kutakiwa na NEC kuanza mchakato wa kupata uraia. Anadaiwa kuwa raia wa Somalia na alivuliwa uanachama na kupoteza nafasi zote za uongozi.


  Hata hivyo, baadhi ya vyombo vya habari vilidai kuenguliwa kwa Bashe aliyeongoza kwa kura zaidi ya 14,000 dhidi ya wagombea wengine wawili, Lucas Selelii na Dk. Hamis Kigwangala, kumetokana na tofauti zake na Ridhiwani ambaye kama Bashe ni Mjumbe wa Baraza Kuu la UVCCM.


  Aidha, Rais Kikwete aliwataka wana-CCM kutoa jasho katika kutafuta ushindi kwa kupita nyumba kwa nyumba, chumba kwa chumba na hata mtu kwa mtu kuwashawishi wananchi watatu wasiokuwa mwanachama wa chama hicho kupigia kura CCM, hivyo kati ya wanachama milioni tano waliopo, kila mmoja akiwa na watatu, watakuwa wamepata kura milioni 15 ambao ni ushindi wa kishindo.


  Mgombea Mwenza wa Rais Kikwete kwa chama hicho, Dk. Mohamed Gharib Bilal, alisema wamemaliza awamu ya kwanza ya kutimiza masharti kikatiba, sasa wanaanza awamu nyingine kuelezea sera ya chama chao hivyo, aliwataka wanachama kujitokeza katika uzinduzi wa kampeni wa chama hicho utakaofanyika kesho katika Viwanja vya Jangwani, Dar es Salaam.


  Source:
  Habari Leo
   
 2. Steve Dii

  Steve Dii JF-Expert Member

  #2
  Aug 20, 2010
  Joined: Jun 25, 2007
  Messages: 6,416
  Likes Received: 67
  Trophy Points: 145
  Ahadi nyingine hii... Nachelea kusema utekelezaji wake utakuwa sifuri kama zilivyo ahadi nyingine nyingi alizowahi kutoa. Kwanini kusubiri watu waingie madarakani kwa 'changamoto bin rushwa' mbalimbali halafu ndiyo kushughulikia utomvu huo?? GIGO!! Garbage In = Garbage Out! Hao watakaoingia madarakani kwa rushwa wataendeleza rushwa na kujihami msiwashughulikie baada ya kuwa wamepita kinjama kwenye chaguzi!
   
 3. M

  Mkandara Verified User

  #3
  Aug 20, 2010
  Joined: Mar 3, 2006
  Messages: 15,443
  Likes Received: 132
  Trophy Points: 160
  Mbona JK hakueleza kwa nini Seleli ambaye alikuwa mbunge pia kaachwa pamoja na kuwa ndiye mshindi wa pili?..
  Uchaguzi ulifanywa na wanachama hivyo majibu ya kumkataa mgombea waliyemchagua ni lazima yarudi kwa wananchi na sio mgombea.
   
 4. Steve Dii

  Steve Dii JF-Expert Member

  #4
  Aug 20, 2010
  Joined: Jun 25, 2007
  Messages: 6,416
  Likes Received: 67
  Trophy Points: 145
  eeerrrrm.... ameyasema yafuatayo:
  In other words, "haitajiki"!!

  Sababu nyingine labda yaweza kuwa:
  He couldn't be more brunt could he?!! :glasses-nerdy:
   
 5. Quinine

  Quinine JF-Expert Member

  #5
  Aug 20, 2010
  Joined: Jul 26, 2010
  Messages: 10,936
  Likes Received: 12,207
  Trophy Points: 280
  Kikwete bwana yaani anawaambia Msekwa na Makamba waache kujibizana na magazeti wakati yeye anajibizana nayo, kweli tunalo....
   
 6. Steve Dii

  Steve Dii JF-Expert Member

  #6
  Aug 20, 2010
  Joined: Jun 25, 2007
  Messages: 6,416
  Likes Received: 67
  Trophy Points: 145
  Wapinzani, kaeni chonjo!.... Print press around the globe could be busy perfecting just that!!:confused2:
   
 7. Nyambala

  Nyambala JF-Expert Member

  #7
  Aug 20, 2010
  Joined: Oct 10, 2007
  Messages: 4,470
  Likes Received: 21
  Trophy Points: 135
  For how long JK atakuwa anamtetea mtoto wake kwenye the so called uzushi? Why not UVCCM kuita waandishi wa habari kufafanua hilo? What if this young man was caught on tape somewhere pompously claiming to have done wht he's accused of? Hata kama si kweli kwamba yeye alihusika na hayo maamuzi lakini I see Ridhwani not much different from many Tz youths ambao ku-exaggerate mambo ni hulka ya kawaida especially kwenye social talks?

  It is therefore high time kwa JK to be a leader, mambo ya mtoto wake ni ya mtoto wake! Let him deal with it. Sidhani kama hayo magazeti kwa namna yeyote ile yamemtaja JK kupewa habari au kuchochewa na Ridhwani kufanya maamuzi juu ya Bashe.
   
 8. mwanatanu

  mwanatanu JF-Expert Member

  #8
  Aug 20, 2010
  Joined: Jan 22, 2008
  Messages: 850
  Likes Received: 42
  Trophy Points: 45
  Mimi najiuliza leo imekuwaje unajibu magazetii?...Ulikuwa wapi watu walipolalamika ya EPA,KIGODA,RICMOND..etc..ulikaa kimya hukushtuka...je leo unaona bora kumtetea mwanao?...ulikuwa wapi wananchi walpotaka kusikia kemeo lako la fedha nyingi zetu zilzo kupuliwa?...NASIKITIKA SANA...


  Huoni kuwa utaratibu huo wenu ni wa kidikteta...Wananchi wanamchagua mtu na nyie mnaweka mtu wa masilahi yenu....je kuna haja gani ya kuara ya maoni?..hamuoni ni ufujaji wa pesa na muda?  Basi ungetupa hata angalau mema matatu ambacho CCM imefanya kwa mwaka mzima.

  Hapo umejitahidi kwa sababu hawo jamaa wanaongea utumbo tu ni bora wakae kimya
   
 9. M

  Mutu JF-Expert Member

  #9
  Aug 20, 2010
  Joined: Mar 30, 2008
  Messages: 1,333
  Likes Received: 6
  Trophy Points: 0
  maswali yote hayo aulizwe kwenye kampeni,wananchi wenye kufunguka masikio wafunguke
   
 10. MKANDYA

  MKANDYA Senior Member

  #10
  Aug 20, 2010
  Joined: Aug 12, 2009
  Messages: 166
  Likes Received: 0
  Trophy Points: 33
  JK hiki nacho kichesho, kuwa wahame lakini wasikihujumu chama(CCM).Kama wao mmewahujumu! itakuwaje wao wasiwahujumu pia? Au ni mkuki kwa nguruwe kwa binadamu mchungu??JK mwache Ridhiwan ajitetee mwenyewe,wewe ni kiongozi wa Taifa; haya unayotoa hayakusitahili kumjibia mwanao,Ridhiwan ni mtu mzima; mwache ajibu yeye.
   
 11. Mdau

  Mdau JF-Expert Member

  #11
  Aug 20, 2010
  Joined: Mar 29, 2008
  Messages: 1,771
  Likes Received: 252
  Trophy Points: 180
  teh teh teh........kumekucha ndo unakumbuka shuka???
   
 12. f

  fungamesa Senior Member

  #12
  Aug 20, 2010
  Joined: Feb 20, 2009
  Messages: 128
  Likes Received: 1
  Trophy Points: 35
  yetu macho
   
 13. mrefu36

  mrefu36 Member

  #13
  Aug 20, 2010
  Joined: Aug 16, 2010
  Messages: 60
  Likes Received: 2
  Trophy Points: 15
  damu nzito kuliko maji
   
 14. Mwanamayu

  Mwanamayu JF-Expert Member

  #14
  Aug 20, 2010
  Joined: May 7, 2010
  Messages: 7,954
  Likes Received: 2,095
  Trophy Points: 280
  Hiyo hapo juu: je, mwandishi hajui hesabu au JK; hivi hiyo equation imekaa vizuri kweli? 5,000,000*(1+3)=15,000,000. Yaani hapa amewaambia wana-CCM kila mmoja atafute watu watatu wa kupiga kura halafu aliyewapata hao asipige kura! Kwa mtu mwenye uwezo wa kufikiri haraka haraka na kwa usahihi kama Dr. Slaa equation ingekuwa hivi: (1+3)*5,000,000=20,000,000. Hiki ndicho alichokuwa akimaanisha bila kufikiria kuwa NEC ina idadi ya wapiga kura 19.67m, sasa hawa 0.33m watatoka wapi. Ni heri angesema 'walau mmoja, wawili au watatu'!! Hivi JK anajua kweli hesabu? Kihesabu amejipa "a word problem" (hesabu za mafumbo) na kushindwa kui-solve! Hivi ndio maana anakimbia mdahalo?! Sasa watanzania mjue kuwa tatizo hili lake ni "just a tip of the iceberg" Kwani hesabu ni logic/ reasoning, hivyo kushindwa kuifanya hesabu nyepesi ni sawa na kushindwa kuona au kutengeneza logic/ ku-reason; sasa mambo makubwa ya nchi anayaweza? Ushahidi tunao hayawezi!!!

  Hivi unamjuaje mwanachama wa chama fulani cha siasa mbali na kuongea yeye mwenyewe au mavazi? Kutufuata mpaka chumbani au majumbani (ingawaje inaweza kuwa na maana ya 'kwa udi na uvumba'), je katiba inaruhusu hili? Hivi hakuna float political party members? Yaani kama kwenye wateja wa simu za mkononi - mtu mmoja kuwa na lines mbili. Kama ndio, hao 5,000,000 wanaweza kuwapatia kura 2,000,000 kwani kura haipigwi mara mbili!!! Je, hawajahesabu na kadi feki kwenye hao 5,000,000?

  Kama yeye analifahamu hilo la ushindi ni kwa mtu mmoja na washindani kawaida ni zaidi ya mmoja, kwa nini chama chake hakikutaka wagombea wengine wa urais ngazi ya chama wachukue fomu? Na hata kutumia mashetani kuwatisha - Sheikh Yahya?
   
 15. Kituko

  Kituko JF-Expert Member

  #15
  Aug 20, 2010
  Joined: Jan 12, 2009
  Messages: 9,367
  Likes Received: 7,008
  Trophy Points: 280
  Mkuu Kazi anayo, Huyu Mtoto anampeleka pabaya babake, ana kichwa kikubwa mno, Mwinyi alpelekwa na mama Sitti, sasa JMK anapelekwa na Ridhwan

  mbayaa
   
 16. TIMING

  TIMING JF-Expert Member

  #16
  Aug 20, 2010
  Joined: Apr 12, 2008
  Messages: 21,837
  Likes Received: 125
  Trophy Points: 160
  Na mkapa je, alipelekwa na nani?
   
 17. Mkimbizi

  Mkimbizi JF-Expert Member

  #17
  Aug 20, 2010
  Joined: Aug 23, 2008
  Messages: 222
  Likes Received: 1
  Trophy Points: 0
  Nimekukubali ingawa hiyo equation umeirahisisha inaweza kuleta mushkeli kidogo,,, ingekuwa wale watu 3*5,000,000 + 1*5,000,000=20,000,000. Ukiweka mabano unapata equation yako.

  Hapo ndio uone upunguani wa hawa jamaa,,,, sasa hizo 0.33 zitoke wapi zaidi ya wizi?
   
 18. Askofu

  Askofu JF-Expert Member

  #18
  Aug 20, 2010
  Joined: Feb 14, 2009
  Messages: 1,668
  Likes Received: 2
  Trophy Points: 133
  :drum::horn::horn::horn::fish2:
   
 19. The Finest

  The Finest JF-Expert Member

  #19
  Aug 20, 2010
  Joined: Jul 14, 2010
  Messages: 21,709
  Likes Received: 44
  Trophy Points: 145
  Like father like Son
   
 20. Edson

  Edson JF-Expert Member

  #20
  Aug 20, 2010
  Joined: Mar 7, 2009
  Messages: 9,202
  Likes Received: 722
  Trophy Points: 280
  kikwete bana
  yaani hajiamini kabisa

  mwaka huu analo, na hivi kawachefua wafanya kazi!!!!

  mdomo huo
   
Loading...