JK na miaka 50 ya UDSM: Nipo hivi nilivyo sababu ya UDSM

You get what you choose........ndivyo maisha yalivyo

Hivi mara ya mwisho kwa JK kwenda UDSM ilikuwa mwaka gani vile? Alishakuwa president?

Mara ya mwisho kama sikosei ilikuwa 2006 au 2007 wakati alipokuja kuzindua Chuo cha Injinia na Technolojia cha Chuo Kikuu cha Dar Es Salaam (CoET). Nakumbuka kindipi hicho JK alikuwa bado kwenye fomu. Yani wanafunzi walikuwa wamejipanga kuanzia geti maji hadi ndani ya kiwanja kidogo cha CoET ambapo uzinduzi wa Chuo kishiriki ulikuwa unafanyika. Kila alipopita umati wa wanafunzi walikuwa wanamshangilia na kuimba JK, JK, JK, JK. Nakumbuka sana siku ile. Leo hii kama amefika na kuzomewa inabidi atafakari sana, Je akistaafu atafanywaje??.
 
... nakwambia masikini akiibiwa chake ambacho ndicho cha pekee kati yake na umauti, usiombe - ndio kma hivo ulivyosikia waungwana wanapopewa japo kiduchu cha salam za hsira za wananchi hivi leo.
 
Duh hii kali pamoja na kuwachangia mil 700 bado wanamzomea ni hatari kwa rais wa nchi.
 
Inamaana UDSM isingalikuwepo watanzania tusingekuwa kwenye hali mbaya kama hii tuliyonayo. Udsm mmetuletea balaa gani hili?


Hapa UDSM hatuna wajinga kama yeye... Ufisadi ni Tabia yake mwenyewe.....anajisifia tu kwa jina la Chuo.
 
anajifanya kutabasamu lakini moyoni inamchoma kuona jamii inayomzunguka haimkubali.
 
dah, aibu jamani, mkuu wetu anaongea watu nje buuuuuu
 
Kaaaaaaaa, hawa watoto wetu jamani hawana adabu sana........mtu mzima mbele ya wageni haaibishwi lol

Wanamzomea wazi hadi inasikika kwenye ka TV kangu ka zamani ka ku-tune kama radio za mkulim
a....duh
 
Najua nitashambuliwa kwa nitakalosema lakini ndio ukweli,hope graduate wa udsm mtabadilisha hali lakini ud ilianzishwa ili kutoa vijana wataosaidia nchi yetu kiuchumi,kijamii na kisiasa lakini badala yake wamekuwa wabakaji wa kila kitu,

mi ckuping,na hakuna chuo ambacho kiliandaliwa kwa lengo la kuhujumu ustaw wa taifa
 
Sikio la kufa halisikii dawa hata kwa hili hatojifunza lolote ili abadilike
 
nasikia kwenye redio kama amezomewa!!!! ni pale aliposema kuwa anaipongeza serikali yake na chuo kwa mafanikio.....am i wrong dudes?
 
Tujiulize kati ya Kikwete na wanaharakati walioibua ufisadi wa EPA na RICHMOND nani anastahili kupewa Honorary degree leo hapo Nkuruma?
Maana kwa kadri JK anavyopewa hizi Degree za heshima ndio jinsi anavyozidi kuboronga.
Maprofesa wa hii nchi wanazidi kunidhihirishia kwamba wao na walimu wa sekondari+msingi wote ni sawa tu,kwa dhana kuwa wapo tayari kumtumikia kafiri ili wapate ujira.Tanzania haitaweza badilika kama hii saratani ya uwoga,uvivu na umaskini wa fikra haitadhibitiwa mapema.
 
Back
Top Bottom