JK na CCM yake kweli inajali maisha ya Watanzania? Nani aliwachagua hawa??!! | JamiiForums | The Home of Great Thinkers

Dismiss Notice
You are browsing this site as a guest. It takes 2 minutes to CREATE AN ACCOUNT and less than 1 minute to LOGIN

JK na CCM yake kweli inajali maisha ya Watanzania? Nani aliwachagua hawa??!!

Discussion in 'Jukwaa la Siasa' started by eumb, Jul 19, 2012.

 1. eumb

  eumb Senior Member

  #1
  Jul 19, 2012
  Joined: Apr 2, 2012
  Messages: 149
  Likes Received: 1
  Trophy Points: 0
  Raisi mpya wa Malawi Manamama Joyce Banda, alipoingia madaraka kati ya maamuzi magumu aliyofanya ni kupunguza matumizi ya anasa kama kuuza ndege ya raisi na yeye kusafiri kwa kutumia ndege za abiria kwa ajili ya kubana matumizi ili kuwasaidia wananchi wake. Huyu aliwafundisha Maraisi wengine wa africa kuwa kuna mambo wanayofanya ya kifahari na kamwe haya manufaa yoyote kwa wananchi wao waliowachagua.

  Hapa kwetu hadithi ya ufahari ipo sana, kumbuka Madaktari wanalalamika hospitali hazina vifaa, mfano pale Muhimbili hospitali inayotegemewa na Taifa, CT Scan imeharibika mwaka mzima, mpya inauzwa about 250m, hiyo mbovu yawezekana ingetengenezwa kwa 100m. Katika hali hiyo tunaambiwa budget ya mwaka 2011/2012 iliyotengwa kwa wizara ya afya kwa ajili ya matumizi ya kawaida (warsha,mikutano,nk) ilikuwa bilioni 8, hivi inaingia kweli akilini kuwa hawa watawala wapo kwa ajili yetu?????

  Hebu jiulize JK na watawala wake wa CCM wangekuwa na utu hiyo ndege ya raisi si wangeuza halafu wangeimarisha vikosi vya uokoaji kwa kununua vifaa vya kisasa kama maboti, helkopta, nk. Kamwe tusingeendelea kupata aibu ya kuomba msaada kutoka South Africa. Jana ndugu zetu wameangamia, tumepata taarifa mchana kama saa tisa boti inazama, ikafika jioni saa kumi na moja nasikia kwenye clouds radio mkuu wa uokoaji anasema wanasubiri mafuta ili waweze kwenda eneo la tukio, baadae saa kumi na mbili nasikia radio one wanasema kuna chombo kimewasili eneo la tukio lakini waokoaji wachache, huku bunge badala ya wao 'viongozi' kuona umuhimu wa kuacha shughuli za bunge na kuweka nguvu pamoja kwa ajili ya kuharakisha uokoaji, yule Mama Makinda anasema mpaka wamalize mjadala, hivi angepata sms mwanae yupo kwenye boti angesubiri??!!

  Watz ni lazima tubadilike na tufumbue macho tuone ulazima wa kufanya mabadiliko makubwa, viongozi wetu wengi wamelewa madaraka, wanafanyakazi kwa mazoea, hawana jipya, kanuni na taratibu nyingi ni zile zile za miaka hiyo, tuchague chama kipya kitakachokuja na mawazo mapya ili hawa wengine wajifunze na pia wapate changamoto na kubadilika. Kule USA kuna Democratic na Republican, ndio vyama vyenye nguvu, wananchi wanasikiliza sera kila uchaguzi unapofika na kuchagua yule mwenye mtazamo mpya, leo wapo mbali, sisi tunabaki na hawa wenye mtazamo wa kuomba kila kukicha na sio kusimama na kujitegemea, ooohhh Tanzania yangu lini utaona hili??????
   
Loading...