Yericko Nyerere
JF-Expert Member
- Dec 22, 2010
- 16,987
- 20,271
Leo tukiwachekea tutakuja kustuka Nape na Kinana wakipangua baraza la Mawaziri kwa maagizo ya Mwenyekiti wake!
hili nalo neno
mawaziri ni makada wa chama kama ulikuwa haujui.Hainiingii kabisa akilini, eti chama kinatoa maagizo kwa mawaziri?
Wanajiandalia anguko lao wenyeweHainiingii kabisa akilini, eti chama kinatoa maagizo kwa mawaziri?
we umedundua leo, hata bungeni waziri mkuu alitoka tamko rasmi kwamba wakuu wa mikoa na wilaya ni makada wa chama so ni ruksa kufanya kazi za uhamasishaji na ujenzi wa chama --- aka kuhakikisha ccm inashinda chaguzi zote ndani ya wilaya / mikoa yao
Tangu ccm imalize mkutano wake wiki jana, kumeibuka staili mpya ya chama hiki katika kuendesha siasa zake!
Chama kimeamua kuchukua nafasi ya serikali, kinazindua miradi ya maendeleo ya nchi, kinatoa karipio kwa watendaji wa serikali, kinawapa maagizo mazito mawaziri,
Na zaidi kinapita nakuwapa ahadi mpya wananchi utadhani ni serikali mbadala ya Tz!
Hivi katiba ya nchi inaruhusu Kinana kumshurutisha Kagasheki, Mwakyembe, au Mwambungu?
Katiba inamruhusi Nape kumkaripia Said Mwema?
Naomba wadau tuangalie kwa pamoja katiba inasemaje hasa marekebisho yake yaliyozaa mfumo wa vyama vingi inasemaje juu ya vyama na serikali?
Leo tukiwachekea tutakuja kustuka Nape na Kinana wakipangua baraza la Mawaziri kwa maagizo ya Mwenyekiti wao!
Lazima kuwe na mstari wa kugawa kati ya majukumu ya chama na serikali.
Chama ni msimamizi wa serikali kiliyoiunda tu, kitoe ushauri huko sio kuingilia utendaji wa serikali!
Serikali ni ya WANANCHI haina chama haina itikadi kwamjibu wa katiba iliyopo na ijayo daima!
Utakiambia nini CHAMA cha KIMUNGU? Toka lini CHAMA sio SERIKALI wanagawa
Leseni kwa Wachimba MADINI??? HIYO NI KOSA KIKATIBA; Ni Sawasawa na RAIS KIKWETE anavyoitisha VIKAO vya CCM-NEC; CCM-CC IKULU DAR
** NI kununua WAPIGA KURA? Wamuulize Mr. ROMNEY alitumia 2 BILLION DOLLARS kununua kura na bado alishindwa na Wapiga KURA MASIKINI wanaojali HAKI zao na SIO MAPESA ya KUMWAGA au KOFIA; KHANGA; SCAFU na VINGI...
Katibu Mkuu wa CCM, Abdulrahman Kinana akikabidhi leseni za wachimbaji wadogo machimbo ya Mugusu, Geita, katika mkutano wa hadhara uliofanyika leo mkoani Geita. Jumla ya leseni 21 zilikabidhiwa kwa wachimbaji hao baada ya kutolewa na serikali ili kuwwezesha wachimbaji wadogo nao kunufaika na madini badala ya wachimbaji wakubwa tu.
Mzee wangu,Mwanangu Yericko Nyerere tatizo la Bongo si CCM bali kuzuka utawala wa kisultani wa Jakaya Kikwete. Kesho utamsikia mkewe hata mwanae nao wakitoa maagizo. Kulikuwa na uzi humu ukiuliza mke wa makamu wa rais anafungua miradi kama nani? Sasa tunakabiliwa na utawala balaa badala ya utawala bora. Tuna walaji tunaowaita viongozi. Kiongozi gani asiyejua mipaka ya mamalaka yake? Kiongozi gani asiyeongoza bali kujifanyia madudu bila kujali kuna kesho? Ni balaa kweli kweli.
Leo tukiwachekea tutakuja kustuka Nape na Kinana wakipangua baraza la Mawaziri kwa maagizo ya Mwenyekiti wake!
hili nalo neno
Kama sijakosea ni kwamba chama kinachoshinda uchaguzi ndio kinaunda serikali, kwahiyo serikali iliyopo ni ya CCM
kwa maana hiyo basi CCM kuamrisha viongozi wa serikali yake ni kama baba kumuongoza kijana wake hamna shida!!
Hayo ni mawazo yangu tu ya ujumla, sijaingia saana katika katiba.....

haya mazoea yana mipaka na kwanini uruhusu mazoea yakutawale hadi uzeeni changes begins with you nani atakukomboa kama sio mwenyewe kujifunga mkanda mkuu,
Daaaaaaah mkuu umeongeza maumivu yangu ya moyo!
My god! Yani haya utayaona tanzania tu!
Tangu ccm imalize mkutano wake wiki jana, kumeibuka staili mpya ya chama hiki katika kuendesha siasa zake!
Chama kimeamua kuchukua nafasi ya serikali, kinazindua miradi ya maendeleo ya nchi, kinatoa karipio kwa watendaji wa serikali, kinawapa maagizo mazito mawaziri,
Na zaidi kinapita nakuwapa ahadi mpya wananchi utadhani ni serikali mbadala ya Tz!
Hivi katiba ya nchi inaruhusu Kinana kutoa leseni za madini? Mbona ni kazi ya wizara husika?, katiba inamruhusu kumshurutisha Muhongo, Kagasheki, Mwakyembe, au Mwambungu?
Katiba inamruhusi Nape kumkaripia Said Mwema?
Naomba wadau tuangalie kwa pamoja katiba inasemaje hasa marekebisho yake yaliyozaa mfumo wa vyama vingi inasemaje juu ya vyama na serikali?
Leo tukiwachekea tutakuja kustuka Nape na Kinana wakipangua baraza la Mawaziri kwa maagizo ya Mwenyekiti wao!
Lazima kuwe na mstari wa kugawa kati ya majukumu ya chama na serikali.
Chama ni msimamizi wa serikali kiliyoiunda tu, kitoe ushauri huko sio kuingilia utendaji wa serikali!
Serikali ni ya WANANCHI haina chama haina itikadi kwamjibu wa katiba iliyopo na ijayo daima!
CCM wanajisahau wanahisi wapo kwenye mfumo wa chama kimoja!