wazo hapa labda ni kuinua kiwango cha maisha cha watanzania. Ila sioni ni sahahi kama raisi wa nchi anakuwa na mkakati wa kuinua uchuki wa watu 100 tu kati ya watanzania milioni 40.
Hayo mawazo hata yakifanikiwa itakuwa ni kama zile pipi zinazotengenezwa na maprofesa wa mazingaombwe. Kwa sababu kuwa na mabilionea 100 wakati mamilioni ya watanzania wana maisha ya utata sio jawabu la matatizo ya nchi. Kama mabilionea 100 watasaidia watanzania wote wawe na huduma za uhakika za afya, wawe na elimu bora (na walimu bora) na makazi bora, kuwe na ajira zinazoeleweka na kiwango cha maisha kinachoridhisha basi huo mpango utakuwa poa!
Ingawa nakubaliana kinadharia na Mtanzania kuwa mabilionea 100 watasaidia kuunda ajira, si lazima mabilionea wote wa TZ wawe wajasiriamali kama alivyo Mengi. Kwa mfano si uwongo kuwa Lowassa ni bilionea (kwa shilingi za Tanzania) lakini ameajiri wangapi? Hawa mafisadi walioficha fedha zao Mauritius wameajiri wangapi? Nadhani serikali ingekazania basics, kama vile kuboresha elimu, madawati na vyoo katika shule zetu, huduma nzuri katika hospitali zetu na kuinua maisha ya wakulima, hapo wanaweza kusema kuwa wamejitahidi kuleta maisha bora kwa kila Mtanzania ifikapo mwaka wa uchaguzi 2010. Lakini hizi dana dana za New York zitaendelea kuwa poroja tu.
Good point FDr, Now can you take a time and defend JK? Tell me what Mr president anachoona ambacho wananchi hatuoni? Hiki sio kiini macho, useme unaweka shilling 10 inageuka million 10, haya mambo yanakuwa na plan, strategies, short term and long term goals. Huwezi kuamka asubuhi ukasema unataka kuongeza list ya mabillioner? How is the question that will rise in any intelligent thinker.Wana JF; Mh.Rais wetu yuko sahihi ktk hilo,tusipende kusahau mapema kiasi hiki jamani,nakumbuka sana misimamo yake alipokuwa anaelezea matumaini yake,muungwana ni mshabiki mkubwa sana wa yule mtalaalam wa Malaya ambaye alikuwa Primier wao (Mahathir).
Mageuzi ya Malaya yalichagizwa na mikakati mingi shirikishi ikiwemo hili analolilia Mheshimiwa Rais wetu.
Anaumizwa na umaskini wetu kwa dhati ,nadhani sasa wakati umefika Wana JF kulizungumza hili kwa udhati sana.
"The only thing we have to fear is fear itself." FDR
Good point FDr, Now can you take a time and defend JK? Tell me what Mr president anachoona ambacho wananchi hatuoni? Hiki sio kiini macho, useme unaweka shilling 10 inageuka million 10, haya mambo yanakuwa na plan, strategies, short term and long term goals. Huwezi kuamka asubuhi ukasema unataka kuongeza list ya mabillioner? How is the question that will rise in any intelligent thinker.
What make Mr Jk to believe he will change this overnight? Utakubaliana na mimi JK ameshajua fika kwamba mchezo umekwisha na matokeo ni kwamba amefungwa. JK alipoingia madarakani alikuwa over confidence, na mimi nikiwa mmoja wa mshabiki mkubwa wa bwana JK kwamba sasa ni mabadiliko time. Challange yakwanza ni pale alipo muweka EL kwenye uwaziri mkuu, nikasema mzee kachemsha lakini mapambano ya ukombozi yanaendelea. Zikaanza kuzuka balaa kwenye killa kona na hapo ndio bwana JK alipo kubaliana na Mwalim kwamba Ikulu si mahala pa mchezo mchezo.
We're in globalization generation, this time need globol oriented president and not Ujamaa or popularity oriented president. Tunaitaji rais mwenye best decisions, rais ambaye ataongoze nchi kwa best interest za wananchi na sio ma patner wenzie.
Jk ameweza kuzikimbia scandals nyingi sana tangu alipo ingia madarakani, kuanzia Richmond, mpaka BOT. Muheshimiwa ameonyesha weakness nyingi sana kwenye uongozi, kuanzia kushindwa kuwakemea wana CCM wenzie wanapoendesha Bunge kwa manufaa yao wenyewe, vile vile ameshindwa kusafisha corruption kwenye cabinet yake. Muheshimiwa raisi ameshindwa kutumia cheo chake cha kuajiri na kufukuza baada kuendelea kuwakumbatia watu kama karamangi na wengineo.
Muheshiwa, ameendeleza tabia yake ya ukinyonga... kwa kusema hili nchini, na kusema lile pindi awapo kwenye nchi za wadau. Serikali ya muheshimiwa imezidi kuzitumia fedha za walipa kodi pasipo kujiuliza, hii ni pamoja na unnecessary misafara ya muheshiwa na wapambe wake. Muheshimiwa, amendeleza kufanya Tanzania kuwa kama nchi ya kifalme kwamba kama wewe ni king then wanao wana enough credentials kuwa viongozi wa sector nyingine. Vile vile muheshimiwa ameajiri baadhi ya washauri wake kutokana na kujuana na sio resume, hii imesababisha Tanzania kuendelea kuseffer katika kila sector.
Mwisho... Muheshimiwa ameonyesha kuchanganyikiwa, kutolewa tena his jod duties.
Matokeo yake akaamua kuweka Tiles hadi kwenye mashamba ya mihogo huko kwao Msoga !JK kutengeneza Mabilionea 100 watanzania 1015, New York
Rais Jakaya Kikwete amesema huu ndiyo mpango wake hata kama atakuwa ametoka madarakani, mazunguzo haya yalifanyinka nchini marekani katika ziara yake ya mwaka huu Sep.2007,
akimkabizi muheshimiwa R.Mengi kazi hiyo ili kuweza kutafuta pesa za kuwasaidia wafanyabiasha hao ambao wata saidia wengi kwa kiasi kikubwa, kwa mimi niliona nimpango mzuri sana tuweze kuwa na watanzania mabilionea na kushika sehemu muhimu za uchumi wa nchi yetu ikiwa nipamoja na madini, utalii, elimu, na nyingine zilizoka Tanzania.
Muh. Mengi aliuliza pesa atapata wapi JK akamuwambia sijui nikazi nimekupa,
pesa hizo zitakuwa zina kopeshwa wafanyabiashara kwa vikundi na ni kiasi kukubwa na siyo pesa kidogo,
Rais aliongea kwa uchungu akisema uchumi wetu umeshikiliwa na wageni wakati sisi hatuna kitu,
katika safari yake hii haikuwa na wafanya biashara wakigeni kwasababu wao hawana shida na safari kama hizi
kwawale wanao jua hii habari zaidi basi watanisaidi kuongezea haya ndiyo ninayo kumbuka tu.
asanteni