Muungwana kama kweli anataka kubadili waziri mkuu anaweza kuangalia mambo yafuatayo.
1:Muda wake uliobaki kumaliza ngwe ya kwanza ya uongozi wake
2:Gharama za kumtunza waziri mkuu mwingine,
3:Mtu anayekubalika na watu
4:Mtu mwenye uwezo wa kuhimili vishindo vipya na nguvu inayoongezeka kutoka kwa wapinzani na asasi za kijamii.
nianze na namba moja
1:Muda wake uliobaki kumaliza ngwe ya kwanza ya uongozi wake
kwa kuwa imebaki takribani miaka miwili muungwana amalize ngwe ya kwanza ni dhahiri kwamba kwa hivi sasa akiamua kufanya uteuzi wa waziri mkuu mpya,itakuwa ni kama wakati wa mpito kuelekea kupata waziri mkuu mwingine kumsaidia ngwe ijayo, na kwa kuwa ni wakati wa mpito basi ni dhahiri atahitaji mtu mwenye uzoefu mkubwa wa shughuli za siasa na kiserikali kwa ujumla hapa ndipo ninaposhawishika kwamba malechela anaweza kuwa miongoni mwa watu wa namna hiyo.
2:Gharama za kumtunza waziri mkuu mwingine,
Kwa kuwa Mawaziri wakuu baada ya uwaziri mkuu ni wenye kutunzwa kwa pesa za walipa kodi basi ni dhahiri kwamba ni rahisi kwa muungwana kuteua Waziri mkuu wa mpito kutoka miongoni mwa mawaziri wakuu wastaafu ambao ni wabunge kwa sasa ili kupunguza gharama za mafao,kwa sababu ninaamini kuwa waziri mkuu atatunzwa kwa kiwango cha pesa ile ile bila kujali amewahi kuwa waziri mkuu katika awamu ngapi(nipo tayari kukosolewa na kuelimishwa).hapa ni dhahiri Malechela ana uwezekano.
3:Mtu anayekubalika kwa Watu.
kutokana na maskendo mengi yaliyoikuta serikali kwa hivi sasa,basi Muungwana anahitaji mtu msafi,asiye na maskendo,mtu mwenye kukubalika kwa watu, nikiangalia katika kundi la wanasiasa na nikajumuisha na sababu nyingine nitakazotoa, niangalie haraka haraka ni nani huyu anaweza kuwa waziri mkuu wa Mpito?(wa kumsaidia muungwana mpaka hapo mwaka 2010?). hebu nimuangalie mzee malecela, hivi je huyu Mtu anakubalika kwa Watu?, hili ni vigumu kusema, lakini je mbona mzee huyu ameweza kubadili fikra za wananchi na kukomboa majimbo kibao kutoka upinzani?, je ni kukubalika kwa mzee huyu na wananchi au ni kutoka na CCM as a team na sera zake?, hapa nimeshindwa kujibu swali hili.
4:Mtu mwenye uwezo wa kuhimili vishindo vipya na nguvu inayoongezeka kutoka kwa wapinzani na asasi za kijamii
Hapa ni dhahiri Muungwana anahitaji Mtu mwenye uwezo wa kumuhakikishia kwamba ataweza kuhimili vishindo vya mashambulizi kutoka pande mbalimbali, kutoka kwa Wapinzani kina Mbowe,lipumba,Mbatia,Slaa ,n.k,yule mtu atakayeweza kuzijibu hoja za wapinzani kwa ufasaha ili kulinda hadhi ya serikali na CCM ,ni nani huyo atakayeiweza kazi hii ya mpito angalau mpaka hapo mwaka 2010?. ila kwa sasa nashawishika kwa mitazamo yangu kwamba Malecela anaweza kuwa miongoni mwa wale ambao Muungwana anaweza kuwapa kazi hii ya muda,
na ikumbukwe kwamba kama Muungwana anaona kwamba wanamtandao wanamkwamisha katika serikali yake,basi ni dhahiri atataka kuhakikisha anauvunja nguvu Mtandao kuto ndani ya CCm yenyewe na kutoka serikalini, je hii haiwezekani ikawa sababu ya kumuweka asiye mwana mtandao katika nafasi ya waziri mkuu?
Tusubiri tuone