JK kumweka Malecela Waziri Mkuu?

Lunyungu

JF-Expert Member
Aug 7, 2006
8,873
1,890
Habarini waungwana . Habari toka kila kona ya Nchi na Jiji zimezidi kuvuma na kuvumika kwamba JK anakaribia kuvunja ufalme wake na aweke wapya ili kukinusuru Chama chake cha CCM.Kumekuwa na kashfa nyingi sana na za wazi kabisa na inasemekana anadhani kwamba ana watu wasio faa. watu hao mmoja wapo ni ndugu Lowasa na wengine ambao wewe unaweza kuwahisi.

Kubwa kuliko lote ni kwamba John Malecela ana angaliwa kwa jicho la huruma kama anavyopenda kusema mkubwa mmoja .Hivyo baada ya kusikia hili toka kwa walio karibu na mkuu huyu nimeingiwa na kiwewe maana kama ni kweli Malecela anarudia Ukuu ule maneno yake ya miaka ile yanaweza kujirudia na hapo Tanzania itakuwa inaisha kabisa. Je kuna unalo lijua juu ya tetetete hizi za mtaani lakini pia wana mtandao wanasema ?
 
Bora amuweke mtu mwenye experience aweze kumshauri kuliko Vipofu wawili kuongozana.
Though Huyo Malecele ni Old Wine in a new Bottle.
But for Stability Purpose ok, na katika kumshauri kwenye maamuzi yake ya kukurupka, yasiyo fuata Itifaki, atasaidia.
 
ah hata akimuweka Kingunge sawa tu... mimi naona yote ni tamthilia tu! lets hope kwa kitu halisi kuanzia 2010 kuendelea!
 
Habarini waungwana . Habari toka kila kona ya Nchi na Jiji zimezidi kuvuma na kuvumika kwamba JK anakaribia kuvunja ufalme wake na aweke wapya ili kukinusuru Chama chake cha CCM.Kumekuwa na kashfa nyingi sana na za wazi kabisa na inasemekana anadhani kwamba ana watu wasio faa. watu hao mmoja wapo ni ndugu Lowasa na wengine ambao wewe unaweza kuwahisi.

Kubwa kuliko lote ni kwamba John Malecela ana angaliwa kwa jicho la huruma kama anavyopenda kusema mkubwa mmoja .Hivyo baada ya kusikia hili toka kwa walio karibu na mkuu huyu nimeingiwa na kiwewe maana kama ni kweli Malecela anarudia Ukuu ule maneno yake ya miaka ile yanaweza kujirudia na hapo Tanzania itakuwa inaisha kabisa. Je kuna unalo lijua juu ya tetetete hizi za mtaani lakini pia wana mtandao wanasema ?

Hii inapendeza ikihamishiwa kwenye udaku....
 
Hizo tetesi zinafaa kuandikia tamthilia au kuwapelekea Ze Komedy (Masanja mkandamizaji na wenzie), hazina matumizi zaidi ya hayo.
 
Muungwana kama kweli anataka kubadili waziri mkuu anaweza kuangalia mambo yafuatayo.

1:Muda wake uliobaki kumaliza ngwe ya kwanza ya uongozi wake

2:Gharama za kumtunza waziri mkuu mwingine,

3:Mtu anayekubalika na watu
4:Mtu mwenye uwezo wa kuhimili vishindo vipya na nguvu inayoongezeka kutoka kwa wapinzani na asasi za kijamii.

nianze na namba moja
1:Muda wake uliobaki kumaliza ngwe ya kwanza ya uongozi wake
kwa kuwa imebaki takribani miaka miwili muungwana amalize ngwe ya kwanza ni dhahiri kwamba kwa hivi sasa akiamua kufanya uteuzi wa waziri mkuu mpya,itakuwa ni kama wakati wa mpito kuelekea kupata waziri mkuu mwingine kumsaidia ngwe ijayo, na kwa kuwa ni wakati wa mpito basi ni dhahiri atahitaji mtu mwenye uzoefu mkubwa wa shughuli za siasa na kiserikali kwa ujumla hapa ndipo ninaposhawishika kwamba malechela anaweza kuwa miongoni mwa watu wa namna hiyo.


2:Gharama za kumtunza waziri mkuu mwingine,
Kwa kuwa Mawaziri wakuu baada ya uwaziri mkuu ni wenye kutunzwa kwa pesa za walipa kodi basi ni dhahiri kwamba ni rahisi kwa muungwana kuteua Waziri mkuu wa mpito kutoka miongoni mwa mawaziri wakuu wastaafu ambao ni wabunge kwa sasa ili kupunguza gharama za mafao,kwa sababu ninaamini kuwa waziri mkuu atatunzwa kwa kiwango cha pesa ile ile bila kujali amewahi kuwa waziri mkuu katika awamu ngapi(nipo tayari kukosolewa na kuelimishwa).hapa ni dhahiri Malechela ana uwezekano.

3:Mtu anayekubalika kwa Watu.
kutokana na maskendo mengi yaliyoikuta serikali kwa hivi sasa,basi Muungwana anahitaji mtu msafi,asiye na maskendo,mtu mwenye kukubalika kwa watu, nikiangalia katika kundi la wanasiasa na nikajumuisha na sababu nyingine nitakazotoa, niangalie haraka haraka ni nani huyu anaweza kuwa waziri mkuu wa Mpito?(wa kumsaidia muungwana mpaka hapo mwaka 2010?). hebu nimuangalie mzee malecela, hivi je huyu Mtu anakubalika kwa Watu?, hili ni vigumu kusema, lakini je mbona mzee huyu ameweza kubadili fikra za wananchi na kukomboa majimbo kibao kutoka upinzani?, je ni kukubalika kwa mzee huyu na wananchi au ni kutoka na CCM as a team na sera zake?, hapa nimeshindwa kujibu swali hili.

4:Mtu mwenye uwezo wa kuhimili vishindo vipya na nguvu inayoongezeka kutoka kwa wapinzani na asasi za kijamii

Hapa ni dhahiri Muungwana anahitaji Mtu mwenye uwezo wa kumuhakikishia kwamba ataweza kuhimili vishindo vya mashambulizi kutoka pande mbalimbali, kutoka kwa Wapinzani kina Mbowe,lipumba,Mbatia,Slaa ,n.k,yule mtu atakayeweza kuzijibu hoja za wapinzani kwa ufasaha ili kulinda hadhi ya serikali na CCM ,ni nani huyo atakayeiweza kazi hii ya mpito angalau mpaka hapo mwaka 2010?. ila kwa sasa nashawishika kwa mitazamo yangu kwamba Malecela anaweza kuwa miongoni mwa wale ambao Muungwana anaweza kuwapa kazi hii ya muda,
na ikumbukwe kwamba kama Muungwana anaona kwamba wanamtandao wanamkwamisha katika serikali yake,basi ni dhahiri atataka kuhakikisha anauvunja nguvu Mtandao kuto ndani ya CCm yenyewe na kutoka serikalini, je hii haiwezekani ikawa sababu ya kumuweka asiye mwana mtandao katika nafasi ya waziri mkuu?

Tusubiri tuone
 
Inawezekana akabadilika kwani Maraisi waliopita ni wachumia tumbo na wauaji pale unapopingana kwa kukataa kupita kwenye anga zao.
Muungwana ni shujaa na shupavu na anawajua wachapa kazi,hata yeye kabla hajaukwaa alikuwa ni buzzer tu katika serikali zilizopita lakini baada ya mkakati wake kukamilika amefika pale alipopahitajia .ili kuwatengenezea na kuwaonyesha WaTANZANIA kama inawezekana kuifanya Tz kama Ulaya na ndio yupo njiani katika kutekeleza nia na lengo lake,mtarudi mkitaka msitake kwani shida za ulaya hazitafanana na TZ mtu kwao jiandaeni kurudi TZ na kama huna kiwanja cha kujenga nunua maana bei inapanda kwa kasi mpya.
 
mmmhhh....fununu zilizopo ni kuwa Chenge na Wassira wanauwania huo uPM....they have smelled blood,and they are lurking.
 
What about S.S... Standard and Speed, Samuel Sitta....... Nyepesi zinasema anatajwa na Kiti chake atapewa mwanamke, Anne Makinda huku Naibu Spika akawa mwanaume, ambaye anaweza kuwa Job Ndugai, ama yeyote atakayeangaliwa kulingana na KARATA ZA WAKATI HUO....
 
Huu wote uzushi tu.Siku kwanza livunjwe ndo tujue kama Mwungwana ana huo ubavu wa kumwacha swahiba wake mkubwa Lowassa.
 
JF sasa imekuwa BAROMETER ya baadhi ya viongozi ..kuwatumia watu kulete TETESI..ili kupima...JK kama atafanya kwa manufaa ya Umma wa watanzania,vema. wa-TZ tushakwama hadi sasa hatujajua nini tufanye kwani kila eneo limeoza...Nilikuwa nikifikiri Magufuli anaweza kuibadilisha wizara ya Ardhi, matokeo yake KERO Zimezidi..Viwanja hadi sasa watu wanayumbushwa...DUH ama kweli Bongo...
 

Similar Discussions

0 Reactions
Reply
Back
Top Bottom