Rais anataka kutimiza utabiri wa kishirikina wa mlinzi wake wa majini, Sheikh Yahya? Kutafuta kukutana na Chadema bila kupambana na ufisadi kwanza ni kutapatapa! Hiyo ni danganya toto kwa vile ameona maji yako shingoni kwani hapo tulipofikia, hata taahira anahisi kuwa upepo sio mzuri! Kuna kila dalili kwamba moto waweza kulipuka wakati wowote.
Hata Sheikh Yahya anajua hivyo, kwamba pamoja na ushirikina, sasa watanzania wako standby, na wako tayari kwa lolote. Harakati za kutaka kukutana na Chadema tu, bila kujibu kwanza tuhuma za Chadema kuhusu ufisadi na umaskini wa watanzania, ni ufukunyuku! Na mikakati yenyewe haina tija kwa vile ni mikakati ya kishirikina!