Jk huyu ni mpya?

Mundali

JF-Expert Member
Sep 16, 2010
749
164
Ni takribani miaka mitano sasa tangu tumpate kiongozi mpya ndugu Jakaya Mrisho Kikwete. Katika mchakato waa uchaguzi mwaka 2005, alitoa ahadi kemkem kubwa ikiwa ni maisha bora kwa kila mtanzania. Nasikitika kwa sasa ahadi hiyo ni njozi iliyosahaulika. Watanzania napenda niwakumbushe mambo muhimu ambayo pengine wengi wetu tumesahau yaliyojiri katika utawala wake wa miaka mitano.
1. Akilihutubia bunge kwa mara ya kwanza, akiwa rais wa nchi alisema kwamba atapambana na rushwa bila kificho wala woga, na kwamba si lazima mtu akamatwe na rushwa bali tuhuma tu zingetosha kumuwajibisha.
2. Alitamka kwamba urais wake hauna ubia.
3. Aliwahi kutamka kwamba amepokea majina ya wauza madawa ya kulevya wakubwa, na dawa yao iko jikoni.
4. Pamoja na mambo mengi mazito aliyotamka hili sintolisahau. Akiwa katika mahojiano na radio Ufaransa aliulizwa swali, "kwamba Tanzania ni nchi iliyojaa rasilimali za aina nyingi na utajiri wa kupindukia, lakini kwa nini watanzania ni masikini?" Akajibu, "hata mimi sijui kwanini watanzania ni masikini".
Jibu lile limenifadhaisha mpaka leo hii. Hivi ni kweli rais wangu hajui ni kwanini mimi ni masikini?
Ni kwanini basi aliniomba kura aniongoze tuondoe umasikini? Je, mpaka leo hajui kwamba mimi ni masikini? Na kwanini anaomba kura za watu masikini ambao hajui sababu ya umasikini wao?
Hivi JK anaweza kweli kusimamia anachokiamini? Aweza kutenda anachosema?
Jamani watanzania wenzangu, na hususani wanaccm, jikomboeni katika utumwa wa kiakili, ukombozi wetu utaletwa na sisi wenyewe. Umasikini, ujinga na maradhi vitaondolewa na sisi wenyewe. Tuikomboe nchi yetu, kiokoeni chama chenu. Kiongozi wenu hajui tutokapo, tulipo na wala tuendapo. Kwa kiingereza hana Vision, Mission, Strategeis. Yupoyupo tu.
Kama aliletewa sheria ya gharama za uchaguzi akaisaini blindly, kisha kwenye kikao cha NEC akamuuliza Marmo, "hivi sheria hii ndiyo tuliyoipitisha?" Sitashangaa akiletewa mkataba wa kuuza sehemu ya nchi akausaini kwa sherehe kuubwa bila kujua kauza nchi.
Tusichague rais mbumbumbu!!!!!!!!!!!!!!!!!! Tutajutia uamuzi kwa kuchagua rais mbumbumbu.
 
Ndiyo JK huyu ni mpya! Kwani bado unasikia zile kauli za Tanzania yenye neema inawezekana, Ajilra milioni mbili, na Maisha bora kwa kila Mtanzania?
 
Jk mpya nani kasema ?ni yuleyule ambaye alitoa ahadi za kumwaga mwaka 2005 kwa mfano alisema kwamba hakuna mtoto wa maskini atakayekosa kusoma kwa kukosa ada ya chuo lkn ni wangapi sasa ambao wamekosa ada na kushindwa kwenda vyuoni na kuishia mitaani.
 
Asante kwa post. Watanzania wengi ni vichwa vigumu sijui kama wanaelewa kuwa wanahitaji ukombozi!
 
Jk mpya nani kasema ?ni yuleyule ambaye alitoa ahadi za kumwaga mwaka 2005 kwa mfano alisema kwamba hakuna mtoto wa maskini atakayekosa kusoma kwa kukosa ada ya chuo lkn ni wangapi sasa ambao wamekosa ada na kushindwa kwenda vyuoni na kuishia mitaani.

Msinikumbushe watoto walioachwa kwenye baridi kule Ukraine kama vile sio watoto wa mkulima na mfanyakazi wa Tanzania, kweli Mungu sio wetu sote
 
Jk ni yule yule ,ila upeo wake umefika kikomo. Ukutaka kujua hilo sikiliza hotuba zake anavyo jitapa ktk kutekeleza ilani ya ccm. Anawashanga mnao hoji utendaji wake maana kwake yeye amefanya makubwa. Shida ni kwamba alipata 80% ya kula kwa watanzania kutokujua uwezo wake na kuamini maneno yake, hadi ilifikia hata prof baregu kuandika makala za tumaini lilo lejea. Sasa tunajua uwezo wake akili ku mkichwa.
 
Uwezo wa huyu mtu ni mdogo sana, hivi kuna mtu amewahi kushuhudia akifanyiwa interview na watu kama shaka tsali wa vio? Nikikumbuka ile siku naharibu kabisa mudi yangu maskini.
 
Watanzania wana akili sana tofauti na mnavyodhani... only that waTanzania hawako tayari kucheza mchezo wa sadaka lau!!!

Give them reliable alternative and you will see!!! Kwa upuuzi wa wengi wanadhani alternative is not about mtu mmoja upande wa upinzani. It is about a reliable oposition in totality... kwa mfano huwezi kusema ati Slaa ni alternative yet mshauri wake mkubwa wa karibu kabisa ni darasa la saba... this is a joke.

Siku chache zilizopita nilikuwa nafikiria hivi wapinzani hawaoni kwamba strategy ya kupeleka wabunge competent kama 80 ni bora kuliko kutumia helcopta 50 kutafuta urais...

Angalia impack ya wabunge wa CHADEMA wasiozidi 20... what if wangekuwa 80.
 
Zile ahadi alizotoa 2005 kishazisahau. Sasa amekuja na ahadi mpya. Kule Bukoba atawaletea meli. Mwanza atawalipia madeni ya chama cha ushirika. Moshi atawaletea mbegu mpya za kahawa. Ukimkumbusha ahadi za 2005 ni kama unaongea na mtu mwingine kabisa. Sasa ni shauri ya Watanzania. Waamue kimoja kusuka na JK au kunyoa na uongozi mpya.
 
Zile ahadi alizotoa 2005 kishazisahau. Sasa amekuja na ahadi mpya. Kule Bukoba atawaletea meli. Mwanza atawalipia madeni ya chama cha ushirika. Moshi atawaletea mbegu mpya za kahawa. Ukimkumbusha ahadi za 2005 ni kama unaongea na mtu mwingine kabisa. Sasa ni shauri ya Watanzania. Waamue kimoja kusuka na JK au kunyoa na uongozi mpya.

Mbona ahadi za 2005 alizoshindwa kuzitimiza hamzitaji kama mnavyozitaja hizi za meli, mbegu za kahawa.

Na nyie lini mtarudi Tanzania kujenga kulijenga taifa badala ya kuongea online tu?
 
Back
Top Bottom