JK hizi ni shukrani au ni mbio zako kuelekea uchaguzi?

mnyikungu

JF-Expert Member
Jul 26, 2009
1,960
2,464
Ukija Iringa msimu huu utaona wakandarasi walivyo tigwa,wanajenga na kukarabati barabara mno,na hili ndilo lililonosukuma kuandika post hii, kuna miradi mingi inayotekerezwa msimu huu hapa iringa.

Kuna miradi ya ukarabati wa barabara,kuna mradi mkubwa wa maji na pia upo mradi wa kupereka umeme vijiji,miradi ya barabara na maji nimeishuhudia na nimeridhika nayo jinsi inavyotekerezwa ila huo wa umeme vijijini bado sijauona.Pia mwaka huu raisi alikuja kupumzika Iringa tena nimedokezwa atakuja tena kwa ajiri ya kuifungua mbuga kubwa kuliko zote tanzania ya Ruaha.

Barabara ya kwenda dabaga imejengwa kwa kiwango cha rami japo siyo yote na barabara za mjini zinakarabatiwa pamoja kile kipande cha ipogoro ambacho ni gharama mno lakini kinatanuliwa na milima inatinduliwa kukiongezea upana achilia mbali barabarakuu inayofanyiwa ukarabati wa hali ya juu pamoja na kutanuliwa. Mradi wa maji ndio unaowafurahisha wakazi wengi wa mjini hapa kwa maana miundombinu inajengwa upya yaani wamefanya kama vile Iringa haijawahi kuwa na maji.

Mwanzo nilifikiri ni shukrani ya kikwete kwa wakazi wa iringa kwa maana ndio mkoa ulioongoza kwa kumpa kura mheshimiwa rais,lakini nikaanza kujiuliza mbona hii shukrani imechelewa kiasi hiki na inatolewa karibu na uchaguzi? Kwa nini isitolewe 2006 au 2007? Au alikuwa anajikusanya? Lakini nikaja kugundua kuwa kipindi hiki viongozi wengi wako kwenye mbio zao kuelekea uchaguzi basi nikahisi labda na mheshimiwa yuko kwenye mbio hizo
 
wasipojenga barabara mnasema wamesahau ahadi,wakijenga mnasema mbio za kuelekea uchaguzi, siasa bwana,huo ni utekelezaji tu wa ilani ya uchaguzi
 
Ujue serikali ina mipango. Wakati wa Iringa ndiyo huu. Je ulitaka pajengwe wapi sasa? Kuna maswali ya kuuliza na kuhitaji majibu..lakini maswali yako hayana msingi maana majibu unayo. Ahadi zinatekelezwa mpaka hata beyond 2010. Iringa ni mkoa muhimu sana kwa uchumi wa Tanzania hivyo unahitaji miundo mbinu thabiti. Hapa lazima timpe JK shavu. Kazi nzuri.
 
mimi natamani kila mwaka kuwe na uchaguzi maana tutapata maendeleo sana
 
mjomba huu ndio wakati wa kurekebisha kwa kuwafanyia vitu vizuri wananchi ili wadanganyike kwenye uchaguzi ujao, tuwe makini watanzania tusisahau yaliyotupata
 
Hapa lazima timpe JK shavu. Kazi nzuri.
Na kama angeendeleza ule mpango wa Mkapa wa kutenga Bil 1 kila mwezi kutoka kwenye makusanyo ya kodi kwa ajili ya ujenzi wa barabara, nadhani tungekuwa tumefika mbali sana
 
Na kama angeendeleza ule mpango wa Mkapa wa kutenga Bil 1 kila mwezi kutoka kwenye makusanyo ya kodi kwa ajili ya ujenzi wa barabara, nadhani tungekuwa tumefika mbali sana
Hizo zote ni Zima Moto kuelekea kwenye uchanguzi mkuu mwakani, Wale wote waongo mwisho wao mwakani
 
Nd.Mnyikungu,

>na milima inatinduliwa<

Hichi ni kiswahili au kihehe?
Kuuliza siujinga. Tafadhali tusomeshane!
moz-screenshot.png
moz-screenshot-1.png
moz-screenshot-2.png
 
Back
Top Bottom