JK: Hatutaki kuingiliwa mgogoro na Malawi

nngu007

nngu007

JF-Expert Member
Joined
Aug 2, 2010
Messages
15,871
Points
1,225
nngu007

nngu007

JF-Expert Member
Joined Aug 2, 2010
15,871 1,225

HABARI
Na Moses Mashalla, Arusha

Posted Jumanne,Novemba20 2012 saa 23:26 PM

KWA UFUPI

"Malawi na Tanzania bado tuko kwenye mazungumzo, tusingependa nchi au mtu yeyote aingilie kati suala hilo kwa namna yoyote ile, " alisisitiza Rais Kikwete.RAIS Jakaya Kikwete amesema mgogoro wa mpaka wa Ziwa Nyasa kati ya Tanzania na Malawi bado unajadiliwa na nchi hizo mbili, hivyo hakuna haja ya mataifa mengine kuingilia.

Rais Kikwete alitoa kauli hiyo jana mkoani Arusha alipokuwa akifungua mkutano wa tatu wa Wakuu wa Nchi Wanachama wa Jumuiya ya Maendeleo Kusini mwa Afrika (Sadc).Pamoja na mambo mengine, katika mkutano huo Rais Kikwete alizindua mkakati wa pili wa chombo kinachoshughulikia masuala ya ulinzi, siasa na usalama katika nchi za Sadc ambazo ni Tanzania, Msumbiji, Zambia, Malawi, Botswana, Afrika Kusini, Namibia, Lesotho, Zimbabwe, Swaziland na Angola.
"Tanzania na Malawi bado tunazungumza kuhusu suala hilo na bado halijatushinda," alisema Rais Kikwete.Rais Kikwete alisema vyombo mbalimbali ikiwamo Sadc, vina wajibu wa msingi wa kuingilia suala hilo, lakini kwa kuwa Tanzania na Malawi bado wako kwenye meza ya mazungumzo, sasa siyo wakati mwafaka."Malawi na Tanzania bado tuko kwenye mazungumzo, tusingependa nchi au mtu yeyote aingilie kati suala hilo kwa namna yoyote ile, " alisisitiza Rais Kikwete.
Rais Kikwete alikwenda mbali zaidi na kueleza kuwa suala hilo liko mikononi mwa nchi hizo mbili, hivyo ni vyema likaachwa kwanza mazungumzo yaendelee kabla ya kuingiza nguvu ya ziada.Alisema kwamba Tanzania na Malawi bado zinaangalia ni namna gani ya kuutatua mgogoro huo bila athari kwa pande mbili na kuomba mazungumzo ya amani yaendelee kuchukua mkondo wake.Kuhusu mkakati wa pili wa chombo kinachoshughulikia masuala ya siasa, ulinzi na usalama katika nchi za Sadc, Rais Kikwete alisema chombo hicho kiko imara na kimejidhatiti kuyasimamia masuala hayo kwa umakini zaidi.Alisema kwa mara ya kwanza mkakati huo ulizinduliwa mwaka 2004, lakini kutokana na mabadiliko ya tabianchi, masuala ya uharamia na biashara ya usafirishaji wa binadamu miongoni mwa nchi za Sadc, ndiyo maana mkakati wa pili umezinduliwa mwaka huu.Katibu Mtendaji wa Sadc, Thomas Salomao aliwaambia wajumbe wa mkutano huo kwamba kuna sera mbalimbali zilizotungwa ndani ya chombo hicho kupambana na rushwa, dawa za kulevya na sera za masuala ya ulinzi na usalama.Kauli ya Rais Kikwete kuhusu mgogoro wa mpaka katika Ziwa Nyasa, imekuja siku nne baada ya ujumbe wa Tanzania na Malawi kukutana jijini Dar es Salaam kwa ajili ya kuzungumzia mgogoro huo.Katika mkutano huo wa Dar es Salaam, nchi hizo mbili zilikubaliana kuwaita marais wastaafu wa nchi za ukanda wa Sadc kusaidia kumaliza mgogoro huo kwa amani.
Akizungumza baada ya mkutano huo uliofanyika Dar es Salaam, Waziri wa Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Kimataifa, Benard Membe hivi karibuni alisema: "Tumekubaliana kutokubaliana, hivyo tulifikiana kuwatumia wakuu wastaafu wa Mataifa ya Sadc kusaidia kutatua mgogoro huu."Membe alitoa taarifa hiyo kwa waandishi wa habari katika mkutano uliomshirikisha pia Waziri wa Mambo ya Nje wa Malawi, Ephraim Chiume.

Katika hatua nyingine, Rais Kikwete jana alizindua mradi wa ujenzi wa hospitali ya kushughulikia tatizo la fistula kwa wanawake katika Kituo cha CCBRT jijini Dar es Salaam.
Mradi huo ambao unagharimu Dola za Marekani 10 milioni, mchakato wake wa ujenzi ulianza mapema mwaka huu na tayari nusu ya fedha hizo zimeshapatikana.

Father of All

Father of All

JF-Expert Member
Joined
Feb 26, 2012
Messages
3,090
Points
1,225
Father of All

Father of All

JF-Expert Member
Joined Feb 26, 2012
3,090 1,225
JK mwanangu, Muingiliwe mara ngapi iwapo kila mnachofanya ni kuingiliana? Tatizo si kuingiliwa bali watawala kuwa bize na kutengeneza pesa badala ya kutumikia wananchi. Angekuwa Kambarage alishatoa ultimatum au kufanya kweli. What is your take mwanangu Njaa Kaya Kikwekwe? Yaani unababaishwa na kibinti ambacho mnaweza kukutana mahali mkayamaliza kiutu uzima? Angekuwa nduli Banda si ungenywea kuliko sasa?
 
S

Sometimes

JF-Expert Member
Joined
Dec 28, 2010
Messages
4,562
Points
1,500
S

Sometimes

JF-Expert Member
Joined Dec 28, 2010
4,562 1,500
Suala tete kwa majibu tata! Tumekubaliana kuto kukubaliana na mazungumzo bado yanaendelea!
 
Chibolo

Chibolo

JF-Expert Member
Joined
Oct 13, 2012
Messages
3,519
Points
2,000
Age
38
Chibolo

Chibolo

JF-Expert Member
Joined Oct 13, 2012
3,519 2,000
Kwanini malawi wasiachiwe ziwa lote jamani make najua hatuna faida nalo!
 
Wiyelelee

Wiyelelee

JF-Expert Member
Joined
Nov 9, 2012
Messages
1,072
Points
1,170
Wiyelelee

Wiyelelee

JF-Expert Member
Joined Nov 9, 2012
1,072 1,170

HABARI
Na Moses Mashalla, Arusha

Posted Jumanne,Novemba20 2012 saa 23:26 PM

KWA UFUPI

"Malawi na Tanzania bado tuko kwenye mazungumzo, tusingependa nchi au mtu yeyote aingilie kati suala hilo kwa namna yoyote ile, " alisisitiza Rais Kikwete.RAIS Jakaya Kikwete amesema mgogoro wa mpaka wa Ziwa Nyasa kati ya Tanzania na Malawi bado unajadiliwa na nchi hizo mbili, hivyo hakuna haja ya mataifa mengine kuingilia.

Rais Kikwete alitoa kauli hiyo jana mkoani Arusha alipokuwa akifungua mkutano wa tatu wa Wakuu wa Nchi Wanachama wa Jumuiya ya Maendeleo Kusini mwa Afrika (Sadc).Pamoja na mambo mengine, katika mkutano huo Rais Kikwete alizindua mkakati wa pili wa chombo kinachoshughulikia masuala ya ulinzi, siasa na usalama katika nchi za Sadc ambazo ni Tanzania, Msumbiji, Zambia, Malawi, Botswana, Afrika Kusini, Namibia, Lesotho, Zimbabwe, Swaziland na Angola.
"Tanzania na Malawi bado tunazungumza kuhusu suala hilo na bado halijatushinda," alisema Rais Kikwete.Rais Kikwete alisema vyombo mbalimbali ikiwamo Sadc, vina wajibu wa msingi wa kuingilia suala hilo, lakini kwa kuwa Tanzania na Malawi bado wako kwenye meza ya mazungumzo, sasa siyo wakati mwafaka."Malawi na Tanzania bado tuko kwenye mazungumzo, tusingependa nchi au mtu yeyote aingilie kati suala hilo kwa namna yoyote ile, " alisisitiza Rais Kikwete.
Rais Kikwete alikwenda mbali zaidi na kueleza kuwa suala hilo liko mikononi mwa nchi hizo mbili, hivyo ni vyema likaachwa kwanza mazungumzo yaendelee kabla ya kuingiza nguvu ya ziada.Alisema kwamba Tanzania na Malawi bado zinaangalia ni namna gani ya kuutatua mgogoro huo bila athari kwa pande mbili na kuomba mazungumzo ya amani yaendelee kuchukua mkondo wake.Kuhusu mkakati wa pili wa chombo kinachoshughulikia masuala ya siasa, ulinzi na usalama katika nchi za Sadc, Rais Kikwete alisema chombo hicho kiko imara na kimejidhatiti kuyasimamia masuala hayo kwa umakini zaidi.Alisema kwa mara ya kwanza mkakati huo ulizinduliwa mwaka 2004, lakini kutokana na mabadiliko ya tabianchi, masuala ya uharamia na biashara ya usafirishaji wa binadamu miongoni mwa nchi za Sadc, ndiyo maana mkakati wa pili umezinduliwa mwaka huu.Katibu Mtendaji wa Sadc, Thomas Salomao aliwaambia wajumbe wa mkutano huo kwamba kuna sera mbalimbali zilizotungwa ndani ya chombo hicho kupambana na rushwa, dawa za kulevya na sera za masuala ya ulinzi na usalama.Kauli ya Rais Kikwete kuhusu mgogoro wa mpaka katika Ziwa Nyasa, imekuja siku nne baada ya ujumbe wa Tanzania na Malawi kukutana jijini Dar es Salaam kwa ajili ya kuzungumzia mgogoro huo.Katika mkutano huo wa Dar es Salaam, nchi hizo mbili zilikubaliana kuwaita marais wastaafu wa nchi za ukanda wa Sadc kusaidia kumaliza mgogoro huo kwa amani.
Akizungumza baada ya mkutano huo uliofanyika Dar es Salaam, Waziri wa Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Kimataifa, Benard Membe hivi karibuni alisema: "Tumekubaliana kutokubaliana, hivyo tulifikiana kuwatumia wakuu wastaafu wa Mataifa ya Sadc kusaidia kutatua mgogoro huu."Membe alitoa taarifa hiyo kwa waandishi wa habari katika mkutano uliomshirikisha pia Waziri wa Mambo ya Nje wa Malawi, Ephraim Chiume.

Katika hatua nyingine, Rais Kikwete jana alizindua mradi wa ujenzi wa hospitali ya kushughulikia tatizo la fistula kwa wanawake katika Kituo cha CCBRT jijini Dar es Salaam.
Mradi huo ambao unagharimu Dola za Marekani 10 milioni, mchakato wake wa ujenzi ulianza mapema mwaka huu na tayari nusu ya fedha hizo zimeshapatikana.

Mi naona kabla ya "kulilia ziwa la Malawi", tutafakari iwapo tumenufaika na chochote kutokana na maziwa tulionayo. Huko Ziwa Vicky mnakumbuka ya Darwins Nightmare? Je Ziwa Tanganyika tumefaidika na nini kama si tu kuvua samaki at small scale level? Na hapa L.Natron je? Sasa tuje hili la Bahari ya Hindi, tumenufaika na nini hasa? Kule Dar es Salaam, naambiwa eti hakuna boti kutoka, achilia Bagamoyo, lakini kutoka Bunju au Mbezi hadi Posta! Labda wa kule Mbagala wanalo boti sijui? Ila naskia kuna kiberenge kutoka Kigamboni hadi Posta kinachopita pale Magogoni. Sasa jamani, Je serikali ina Mkakati wowote na jinsi nchi inavyoweza kunufaika na hizi raslimali? is there any national strategy for utilising such natural resources? Au je serikali inajua kwamba kuwa na Ziwa au Bahari ni vitega uchumi?
 
J

JokaKuu

Platinum Member
Joined
Jul 31, 2006
Messages
15,276
Points
2,000
J

JokaKuu

Platinum Member
Joined Jul 31, 2006
15,276 2,000
Suala tete kwa majibu tata! Tumekubaliana kuto kukubaliana na mazungumzo bado yanaendelea!
Sometimes,

..nimecheka kweli!!

..Jk amekuwa kama dereva aliyelala kwenye usukani.

..hivi tuseme hana habari na tamko la Waziri wake wa mambo ya nje kwa vyombo vya habari kwamba mazungumzo baina ya Tanzania na Malawi yamekwama na inabidi kutafuta msuluhishi??
 
Last edited by a moderator:
DALLAI LAMA

DALLAI LAMA

JF-Expert Member
Joined
Jan 31, 2012
Messages
8,614
Points
1,500
Age
37
DALLAI LAMA

DALLAI LAMA

JF-Expert Member
Joined Jan 31, 2012
8,614 1,500
Jk na Membe lao moja wakikutana na huyo mwanamke wa Nyasaland!!
 
SHERRIF ARPAIO

SHERRIF ARPAIO

JF-Expert Member
Joined
Aug 25, 2010
Messages
8,655
Points
2,000
SHERRIF ARPAIO

SHERRIF ARPAIO

JF-Expert Member
Joined Aug 25, 2010
8,655 2,000
Jk na Membe lao moja wakikutana na huyo mwanamke wa Nyasaland!!
Usikute wweshauza hilo ziwa kwa huyo mama. Lakini najua kuna tembo wengi mitaa ile so Kinana hawezi kukubali ziwa liende Malawi
 
Monsgnor

Monsgnor

JF-Expert Member
Joined
Mar 26, 2012
Messages
478
Points
500
Monsgnor

Monsgnor

JF-Expert Member
Joined Mar 26, 2012
478 500
Mhh! God Help!

Sent from my BlackBerry 9700 using JamiiForums
 
TANMO

TANMO

JF-Expert Member
Joined
Apr 12, 2008
Messages
8,982
Points
1,500
TANMO

TANMO

JF-Expert Member
Joined Apr 12, 2008
8,982 1,500
Sometimes,

..nimecheka kweli!!

..Jk amekuwa kama dereva aliyelala kwenye usukani.

..hivi tuseme hana habari na tamko la Waziri wake wa mambo ya nje kwa vyombo vya habari kwamba mazungumzo baina ya Tanzania na Malawi yamekwama na inabidi kutafuta msuluhishi??
Hawana mawasiliano, kila mmoja anaibuka na la kwake, akijisikia....
 
Forum statistics

Threads 1,286,228
Members 494,902
Posts 30,887,738
Top