JK Hana Uongozi Stahili

donasheri

Member
Mar 11, 2008
18
0
Matukio mengi serikalini yanadhihirisha waziwazi udhaifu mkubwa wa uongozi wa JK. Nitajaribu kuelezea kidogo:
Kwanza uongozi wa nchi ni kama kitambaa cheupe ukutani. Wananchi wanakiangalia wakati wote ili kuwa na imani nacho. Kinapokuwa cheupe wakati wote wananchi kuwa na imani kubwa nacho.

Lakini kitambaa kikijaa madoa meusi kila mahali imani hiyo huondoka kabisa. Ndivyo ilivyo kwenye uongozi wa JK. Alitakiwa kukisafisha kila mara ili kuondoa madoam yanayoingia.

Pili kiongozi mkuu ana vyombo vyake vingi vinavyomsaidia kazi. Taarifa kama hazitumii ipasavyo unatarajia nini? Kama anazidharau taarifa hizo ajue kuwa hata wale wanaqomsaidia kumpelekea hizo taarifa hawatafanya hivyo kwa uaminifu na ufanisi mkubwa. Kwa kutozifanyia kazi huzaa majanga ndani ya mfumo wake.

Nadhani hali ndiyo hiyo. Kiongozi msikivu huvuna mazuri mengi kutoka kwa wasaidizi wake. Matokeo yake ni ubora wa uongozi wake. Lakini sivyo hivyo kwa JK.

Tatu kiongozi yeyote anayetuhumiwa anapoteza heshima mbele ya umma. Mponda hana sifa na heshima hadharani. Nkya pia. Na wale wote wanaotuhumiwa. JK anapowalazimisha waendelee na nyadhifa zao anawapa shida kubwa mbele ya umma.

Nne JK ni kitamaa cheupe kilichojaa madoa meusi hata kama yeye ni msafi. La usafi wake mimi sijui. Kutokana na madoa haya heshima yake mbele ya umma imepotea.
 
Back
Top Bottom