JK, Chenge, Lowassa, Rostam, Karamagi na Karume wameshampata mgombea Urais kupitia CCM | JamiiForums | The Home of Great Thinkers

Dismiss Notice
You are browsing this site as a guest. It takes 2 minutes to CREATE AN ACCOUNT and less than 1 minute to LOGIN

JK, Chenge, Lowassa, Rostam, Karamagi na Karume wameshampata mgombea Urais kupitia CCM

Discussion in 'Uchaguzi Tanzania' started by Yericko Nyerere, Aug 29, 2012.

 1. Yericko Nyerere

  Yericko Nyerere Verified User

  #1
  Aug 29, 2012
  Joined: Dec 22, 2010
  Messages: 16,212
  Likes Received: 3,774
  Trophy Points: 280
  Taarifa za kuaminika toka kwa chanzo muhimu toka ndani ya kamati kuu ya ccm na kutoka key-parsons wa urais wa Tz kwa tiketi ya ccm, zinasema kuwa:

  "Wale walioamini na wanaoamini kuwa Jk na Lowassa ni maadui, wamefilisika.

  Kundi linalounda maamuzi ya mwisho ya URAIS wa Tz kwa mkono wa ccm linaongozo na key-Parsons wasiozidi kumi ambao ni: 1) Jk 2) Lowassa (3) Rostam (4) Karamagi (5) Chenge (6) Mzee karume Rais Mstaafu (7) Nahodha

  Inaelezwa kuwa hawa ndio wenye maamizi ya misho kwa sasa na tayari wameshamchagua mgombea urais ajae, inazidi kuelezwa kuwa iwe usiku au mchana, kiangazi au masika, imwagwe damu au vicheko vitawale, wao wanae mgombea uraisi mmoja tu ambae ni EDWRD N. LOWASSA.

  Nanukuu moja ya maneno ya vikao vyao, "Kwakutumia mamlaka na raslimali nilizonazo, wewe kaka yangu endelea kuonyesha mbele ya jamii kuwa tunatofautiana, tena nipinge hadharani na ikiwezekana kwa kashifa", huku akicheka anaongeza "Nakuhakikishia vijana wangu hawatakusumbua, hilo nitawaagiza kabisa" Mwisho wa kunukuu!

  Moja ya vikao vinavyotajwa kuwa vilikuwa namafanikio nikile kilichokalika hivi karibuni ambapo inaelezwa kilinogeshwa na uhudhuriaji wa Rostam kwa njia ya video akiwa Malaysia na kuahidi kuchangia fungu la kutoa kuchagiza kampeni na malengo yao.

  Hayo ndio yanayojiri kwa siasa za Tanzania, sio lazima uamini ila tumia akili yako,
   
 2. The Boss

  The Boss JF-Expert Member

  #2
  Aug 29, 2012
  Joined: Aug 18, 2009
  Messages: 37,826
  Likes Received: 22,465
  Trophy Points: 280
  another Lowassa movie...
   
 3. N

  Ndinani JF-Expert Member

  #3
  Aug 29, 2012
  Joined: Aug 29, 2010
  Messages: 5,413
  Likes Received: 734
  Trophy Points: 280
  Hizo ni propaganda zenu; kwani kati ya hao wangapi wako cc ya magamba?
   
 4. O

  OgwaluMapesa JF-Expert Member

  #4
  Aug 29, 2012
  Joined: May 24, 2008
  Messages: 10,948
  Likes Received: 45
  Trophy Points: 145
  kwa hayo maneno tu ya jf ni ngumu kuamini ila na mimi i have my prediction kwa 2015 rais ni Lowasa au dr.slaa kwa maana nyingne first lady ni mama josephene au mama regina...
   
 5. Zipuwawa

  Zipuwawa JF-Expert Member

  #5
  Aug 29, 2012
  Joined: Nov 28, 2010
  Messages: 3,052
  Likes Received: 92
  Trophy Points: 145
  kazi kwao sisi tumewachoka sasa
   
 6. Yericko Nyerere

  Yericko Nyerere Verified User

  #6
  Aug 29, 2012
  Joined: Dec 22, 2010
  Messages: 16,212
  Likes Received: 3,774
  Trophy Points: 280
  Wena ccm wanaamini kuwa cc ndio muamuzi wa urais, lakini wamiliki wa ccm wanachombo kipya kilichojiunda automatically kinachoitwa key-parsons chenye maamuzi ya mwisho juu ya urais wa tz kwa tiketi ya ccm
   
 7. z

  zamlock JF-Expert Member

  #7
  Aug 29, 2012
  Joined: Dec 25, 2010
  Messages: 3,849
  Likes Received: 53
  Trophy Points: 145
  nyie ngoja mtape tape nchi imekwenda mikononi mwa dk slaa hv ccm bado wana matumaini ya kutaka kuja kutawala nchi hii? Ha ha ha ha ha dk slaa imarisha chama vijijini tuje tujichukulie nchi bila shida, atuitaki ccm tena
   
 8. K

  Kwame Nkrumah JF-Expert Member

  #8
  Aug 29, 2012
  Joined: Dec 2, 2008
  Messages: 887
  Likes Received: 31
  Trophy Points: 45
  Kwa hiyo Mkapa yupo kundi la Membe?
   
 9. Yericko Nyerere

  Yericko Nyerere Verified User

  #9
  Aug 29, 2012
  Joined: Dec 22, 2010
  Messages: 16,212
  Likes Received: 3,774
  Trophy Points: 280
  Haijathibitishwa ila inadokezwa kuwa yupo kundi la Sumaye lenye wahafidhina na wastaafu wengi
   
 10. A

  Ame JF-Expert Member

  #10
  Aug 29, 2012
  Joined: Mar 14, 2011
  Messages: 3,352
  Likes Received: 659
  Trophy Points: 280
  Baambie hii ndoto nibora wakaiota kukiwa bado usiku usiku maana usiku utakapoisha hata harufu yake hawataikumbuka.....The power has changed hand nobody amongst uliowataja atakanyaga jumba la ufalme I make this statement bold and clear! Keep this for your own record kama hawakuwahi kuona ama kukutana na kitu inaitwa power to change things basi this time will they feel the impact of what's called DUNAMIS!
   
 11. e

  eedoh05 JF-Expert Member

  #11
  Aug 29, 2012
  Joined: Apr 20, 2011
  Messages: 633
  Likes Received: 39
  Trophy Points: 45
  Mm!...Nimechoka. Ngoja nikalale. Lakini Samwel Sitta anataka japo miaka mitano tu...asafishe mafisadi na ufisadi. Kwa heri, naenda kulala.
   
 12. Yericko Nyerere

  Yericko Nyerere Verified User

  #12
  Aug 29, 2012
  Joined: Dec 22, 2010
  Messages: 16,212
  Likes Received: 3,774
  Trophy Points: 280
  Hilo ndio wengi wa wazalendo tunalipigania na kwakile upinde hawa mafisadi hawakanyagi ikulu yetu takatifu tena
   
 13. TOWNSEND

  TOWNSEND JF-Expert Member

  #13
  Aug 29, 2012
  Joined: May 8, 2011
  Messages: 2,597
  Likes Received: 48
  Trophy Points: 145
  usilale we mie nasubiri barcelona na madrid achana na hao wameshakufa wanasubiri kuzikwa ...kama iliangalia dkk 45 itv ungemona jamaa alivyochoka mikono inatetemeka hata shingo hawezi kuigeuza
   
 14. a

  armanisankara JF-Expert Member

  #14
  Aug 29, 2012
  Joined: Jul 15, 2011
  Messages: 283
  Likes Received: 2
  Trophy Points: 35
  Waziri Mkuu wa zamani, Edward Lowassa, amesema muda wa kutangaza iwapo atagombea urais au la katika Uchaguzi Mkuu wa mwaka 2015, bado haujafika na kwamba kufanya hivyo kwa sasa kunaweza kufungua uwanja wa mapambano, maneno mengi, zikiwamo tuhuma, kushutumiana na kuyapa magazeti cha kuandika.

  Kutokana na hali hiyo, amesema hana muda wa kubishana na watu ambao wamekuwa wakihusisha baadhi ya kauli zake na maandalizi ya kutaka kugombea urais mwaka huo kwa kuwa wanafanya hivyo kwa kutumia uhuru wao wa kikatiba wa kutoa maoni.

  Lowassa ambaye ni Mbunge wa Monduli (CCM), alisema hayo alipokuwa akihojiwa katika kipindi cha Dakika 45 kilichorushwa na televisheni ya ITV juzi usiku, ambacho pamoja na mambo mengine, Mtangazaji alimtaka kutoa kauli kuhusiana na kutajwa na baadhi ya watu kwamba anataka kugombea urais mwaka huo.

  Akijibu swali hilo, Lowassa alisema: “Waingereza wana msemo: ‘We shall cross the bridge when we get there’ (Tutavuka daraja tutakapolifikia). Hatujafika kwenye daraja lenyewe. Tuko kwenye uchaguzi wa chama chetu sasa hivi. Tunaendelea vizuri. Halafu tutaona mambo yanavyokwenda.”

  “Bado miaka ya uchaguzi wa 2015 bado mbali sana. Tukianza kusema huku, tutafungua tu uwanja wa mapambano tena na maneno mengi na magazeti na tuhuma, kushutumiana. Sasa nitavuka daraja nitakapofika.”

  Kuhusu watu wanaohusisha baadhi ya kauli zake na maandalizi ya kutaka kugombea urais, Lowassa alisema: “Kila mtu ana uhuru wa kutoa maoni yake. Katiba yetu inaturuhusu hivyo. Na kila mtu ana uhuru, siku hizi kila kitu ni siasa katika nchi yetu, kila kitu, chochote kile ni siasa.”

  “Hata kitu ambacho ni cha weledi kabisa itawekwa siasa, kitu gani itawekwa siasa, jambo la dini litawekwa siasa, jambo gani. Kila kitu ni siasa. Sasa mimi sina muda wa kubishana nao. Nafanya yale yanayonipasa, naomba Mungu anisaidie niyafanye, kwa kuwajibika, kwa wajibu wangu. Ila nasema ukifika wakati huo nitawaambia Watanzania. Lakini kwa sasa ni mapema mno kusema lolote.”

  Kuhusu misaada anayoitoa kupitia harambee, ambazo amekuwa akizifanya makanisani, misikitini na kwenye shule, alisema hufanya hivyo kwa kuelekezwa na busara zake na kwamba harambee hizo amejaliwa na Mungu na ni njia ya kumtumikia Mungu na Watanzania.

  “Nina maombi mengi sana ya harambee kwa makanisa kwa misikiti kwa shule. Yako mengi kweli kweli. Na mimi Mungu anisaidie yale nitakayoweza kuyafanya nitayafanya, yale nitakayoshindwa nitashindwa. Nitaomba radhi. Nitayafanya kwa nguvu zangu zote, kwa uaminifu wangu wote, kwa sababu ni njia ya kumtumikia Mungu, ni njia ya kuwatumikia Watanzania,” alisema Lowassa.

  KILIMO KWANZA

  Akijibu swali kuhusu changamoto inayosababisha sera nzuri ya ‘Kilimo Kwanza’ kutoeleweka vyema na kushindikana kutekelezeka, Lowassa alisema: “Hapa tuwe waangalifu kidogo. Mimi sikubaliani na Kilimo Kwanza. Na wanajua. Kwenye chama changu wanajua… Mimi naita ‘Elimu Kabla’ halafu ‘Kilimo Kwanza’.”

  Alisema hakubaliani na Kilimo Kwanza kwa sababu historia ya mataifa yaliyoendelea duniani inaonyesha kuwa ili kupata mabadiliko ya msingi katika kilimo inatakiwa kuwekeza kwanza kwenye elimu.

  Lowassa alisema hiyo ina maana kwamba, unapokuwa na mkulima aliyesoma, atalima vizuri zaidi, kadhalika unapokuwa na mfugaji aliyesoma, atafuga vizuri zaidi, kwa sababu ya elimu aliyonayo.

  “Sasa tumeleta Kilimo Kwanza tukavuruga kidogo. Elimu ya sekondari hizi za kata ikaenda ikanisumbua. Kwa hiyo, niliporudia mara ya kwanza nikasema mimi sikubaliani na sera hii mpaka waweke kwanza ‘Elimu Kabla’ Kilimo Kwanza. Elimu ni msingi kabisa. Kadiri unavyoelimisha taifa lako, ndivyo linavyokuwa na nguvu ya kujiendeleza,” alisema Lowassa.

  Alisema baadhi ya mataifa kama India, Indonesia na Malaysia, ambayo yalipata uhuru miaka ya 1960, yalikuwa nyuma kimaendeleo sawa na Tanzania.

  Hata hivyo, alisema leo mataifa hayo yako mbali kiuchumi kulinganisha na Tanzania kwa kuwa walifanya maamuzi ya msingi, kwani jambo walilosimamia kwanza ni elimu kwa kuwaelimisha watu wao ndani na nje.

  Alisema shule za sekondari za kata ni moja ya suluhu ya majibu hayo iwapo zitasimamiwa vizuri, watoto wakapata kusoma vizuri na kutoka vijana watakaoweza kuajiriwa hata kwenye viwanda.

  “Watarudi vijijini. Lakini arudi mtu imara, aliyesoma, aliyeelimika. Ni muhimu sana. Ukipata wakulima walioelimika, taifa linabadilika,” alisema Lowassa.

  GESI

  Alisema Watanzania wamepata baraka kwa kujaliwa neema ya gesi nyingi katika mikoa ya Lindi na Mtwara na kusema jambo hilo ni kubwa kwa kuwa kupata gesi au mafuta kunaweza kukawa ama laana au neema kwa nchi kutokana na namna rasilimali hiyo itakavyosimamiwa.

  “Mkiisimamia vibaya inakuwa laana kwa nchi yenu, mkisimamia vizuri inakuwa neema,” alisema Lowassa.

  Kutokana na hali hiyo, aliwaomba Watanzania, hasa walioko serikalini kuhakikisha wanaisimamia neema hiyo vizuri, ikiwa ni pamoja na kutunga sera haraka ili wananchi, ambao gesi itakakopatikana wajue faida na manufaa watakayoyapata.

  Alisema pia hakuna sababu ya kuendelea kutoa vitalu vingine, badala yake viachwe serikali ishughulike kwanza na neema iliyopatikana.

  “Nikisema hivi wataniona mjinga. Lakini I am not a fool, najua nasema nini,” alisema Lowassa.

  Alisema kwa mfano, nchini Finland katika mwaka 1962 waligundua mafuta, lakini hawakuanza kuyachimba na kwamba, walianza kuchimba baada ya miaka mingi kupita na hawajatoa yote, hivyo akashauri Watanzania kujifunza kutoka kwao.

  Lowassa alisema hata Baba wa Taifa, Hayati Mwalimu Julius Nyerere, enzi za utawala wake madini yalipogundulika kuwapo nchini, alizuia yasichimbwe kwa maelezo kwamba, Watanzania hawajawa tayari.

  “Juzi juzi tumeanza kuchimba madini. Kwa hiyo tusigawe yote. Hili ni suala la sera. Tusigawe vitalu vyote, tungojee muda upite. Hilo la kwanza, sera. Lakini la pili, ipite sheria inayotawala jambo hili kama walivyofanya Waganda. Kuna sheria ya management ya resources (kusimamia rasilimali) zile za gesi, mnatumiaje,” alisema Lowassa.

  AJIRA KWA VIJANA


  Alisema moja ya matatizo makubwa nchini na ya msingi, ni ajira kwa vijana na kwamba, kuna siku aliwahi kulisema hilo, waziri mmoja akamshambulia, lakini baadaye akamuelewa.

  “Nasema tatizo la msingi la Tanzania sasa kuliko kitu chochote ni ajira kwa vijana. Hawa vijana waliomaliza vyuo vikuu kwa maelfu kwa mamia, wanaomaliza high school (shule za juu), wanaomaliza taasisi nyingine, wako wengi, wamesoma, wana nguvu, wana akili. Na hawa ndipo Mungu alipowaweka nchi yao. Hawana ajira, hawana matumaini, ni very dangerous (hatari sana), very very dangerous (hatari sana sana),” alisema Lowassa.

  Alishauri kusambazwa viwanda vya pamba vinavyochukua watu wengi kwa ajira katika maeneo yanayolima zao hilo ili kuwawezesha vijana wanaomaliza masomo vyuo vikuu kupata ajira.

  Alisema iwapo vijana hao wataendelea kuachwa, amani iliyopo kamwe haiwezi kudumu, hivyo, akasema: “Tukope, tuendeshe viwanda vya kuajiri vijana wetu.”

  Pia alishauri kuwekeza mapato ya gesi katika uchumi wa kilimo, ambao alisema ndiyo una watu wengi zaidi nchini.

  “Kwa hapa ndipo kuna ajira ya watu wengi zaidi. Wekeza kwenye kilimo, utafanya nini, utafikiria baadaye,” alisema Lowassa.

  Alihoji kitakachomsaidia mkulima wa Tanzania kwenda kwa kasi zaidi baada ya gesi kupatikana kwa sababu kuna hatari inaweza kuikumba nchi kutokana na kubweteka kwa kuwa gesi imepatikana.

  Alishauri pia kutengwa fedha zitakazotokana na mauzo ya gesi dhidi ya zile zinazokusanywa na Mamlaka ya Mapato Tanzania (TRA), ambapo fedha za gesi zitumike kuanzisha miradi maalum, kama ya viwanda na kilimo.

  “Lakini angalia miundombinu uijue. Wekeza kwenye miundombinu, wekeza kwenye elimu, wekeza kwenye afya. Chagua maeneo unayoyasimamia, ambayo yataleta mabadiliko kwa Watanzania hawa wajue kweli tunapata gesi,” alisema Lowassa.

  Pia alishauri kuwapa mafunzo vijana ili wawe weledi katika maeneo ya gesi kwa kuwa anaamini kwa muda mrefu serikali itakuwa inawategemea wageni.

  MAAMUZI HAYASIMAMIWI
  Alishauri uamuzi wa serikali wa kupunguza matumizi yake usimamiwe kwa kuwa kuna tatizo nchini la kufanya maamuzi mengi yasiyosimamiwa.

  Alisema Rais wa Rwanda, Paul Kagame, ni mfano mzuri wa kuigwa kwa kusimamia maamuzi, yakiwamo yale ya kupunguza matumizi ya serikali.

  “Kwa hiyo, hili nalo lifanyiwe maamuzi na yasimamiwe. Tunatoa maamuzi mengi sana katika nchi yetu. Mara ooh, tunalaumiwa katika Afrika Mashariki tunafanya maamuzi hatuyasimamii. Wenzetu wanatuwahi kwenye suala la kufanya maamuzi. Tusimamie kwenye maamuzi. Tufanye maamuzi na tuyasimamie,” alisema Lowassa.

  APINGA UCHUMI KUTEGEMEA DOLA

  Lowassa alisema zipo sera nyingine za kifedha, ambazo zinachangia mfumuko wa bei ama kupanda au kushuka na kutolea mfano wa namna ambavyo uchumi wa kutegemea dola unavyopigiwa kelele.

  “Ndiyo maana nilisema dollarization of our economy is wrong (kutumia Dola ya Marekani kwenye uchumi), tutafakari upya kama ni sahihi. Pengine Gavana (wa Benki Kuu ya Tanzania-BoT) angekuja publicly (hadharani), akaanzisha mjadala kidogo, kwanini inflation (mfumuko wa bei) haujashuka,” alisema Lowassa na kushauri nchi kuingia kwenye uchumi wa viwanda.

  “Kwa mfano, ningekuwa na mamlaka mimi, vijana hawa walioko JKT, ningewachukua kwa maelfu kwa mamia, nikatafuta mashamba, tukapanda michikichi. Michikichi tu. Panda heka elfu kumi, elfu kumi, elfu ishirini, elfu thelathini.” alisema na kuongeza:

  “Nimekwenda Malaysia, Malaysia uchumi wao unategemea michikichi. Na Michikichi wale wameipata Tanzania. Lakini leo number one wa expert (wataalamu) wa michikichi. Na hata hapa tunakula mawese kutoka Malaysia.

  “Wamefanya nini? Wamepanda kila mahali, kila eneo la nchi yao wamepanda michikichi. Wamekwenda kukodisha ardhi kwa majirani zao Waindonesia, wanalima michikichi kule katika nchi ya wengine.”

  Alisema Tanzania kuna ardhi kubwa, ambayo Mwenyezi Mungu ameibarikia, ina mito na rutuba.

  “Tungegeuza mashamba ya michikichi vijana wa JKT kazi yenu kuanzisha mashamba ya JKT, tukatumia nguvu kazi hii kuanzisha uchumi…kwa majirani hawa tukawa sisi ndiyo tunatawala kwa mafuta, tunaweza, ni maamuzi. Maamuzi ya msingi yafanyike, tufanye mambo hayo,” alisema Lowassa na kuongeza:

  “Mwalimu (Nyerere) alifanya maamuzi mengi sana ya kiuchumi, ndiyo yaliyotusukuma mpaka hapa. Rais Mkapa, Rais Mwinyi walifanya maamuzi. Rais huyu (Kikwete) amefanya maamuzi. Lakini tufanye na mengine na mengine.”

  CHANZO: NIPASHE

   
 15. p

  philipoz Member

  #15
  Aug 29, 2012
  Joined: Nov 10, 2011
  Messages: 66
  Likes Received: 13
  Trophy Points: 15
  kwa maana hio, panga pangua rais anaekuja si muislam?, namwachia shekhe Ponda anijibie
   
 16. salosalo

  salosalo JF-Expert Member

  #16
  Aug 29, 2012
  Joined: Jun 7, 2012
  Messages: 579
  Likes Received: 71
  Trophy Points: 45
  Mimi sitaki kuamini hayo ya kwako ila yamekuja sawa na hisia zangu kwambaa, Pamoja na ufisadi mkubwa aliopata kuufanya Lowasa kipindi cha uongozi wake bado anabaki kuwa kiongozi pekee aliyebaki upande wa CCM mwenye sifa za kuwa rais. Bila yeye mimi maraisi wengine nawaona upinzani.
  Sifa za lowasa:
  • Anajua kukaripia pale mambo yanavyokwenda ndivyo sivyo
  • Anujua kucheka kwa kipimo pale jambo jema linapotokea
  • Si mtu wa kupigwa mikwara ya kijingajinga na ama viongozi wa chini yake au wale viongozi wa nchi zingine.
  • Hata anapokosea, hakosei kiasi cha kuwaumiza waliomtuma kazini,yaani wananchi
  • Si mbinafsi na wala haendekezi undugu, ukabila na udini
  • Ni kiongozi mwenye sifa ya kuheshimika bila kuomba
  • Ni mwizi wa pesa za Umma kwa manufaa ya Umma, yaani na maanisha pesa zake huzitumia kuwekeza hapahapa nchini kwa manufaa ya wananchi
  • mimi pia nashawishika kusema kuwa anajua kuwajibika pindi anapokosea(kitu ambacho ni adimu sana kwa viongozi waliowengi)
  • anauwezo wa kusimamia jambo likakamilika(fuatilieni historia yake tangu akiwa AICC)

  Kiufupi napenda namna yake ya uongozi, kukosea ni kawaida kwa binadamu ila mbaya ni kukataa kukosolewa pale unapokosea.
  NI KWELI LOWASA NA KIKWETE SIO MAHASIMU HATA KIDOGO,ila sidhani kama Kikwete kamruhusu amkandie na kumtukana kama ulivyosema
   
 17. F

  Froida JF-Expert Member

  #17
  Aug 29, 2012
  Joined: May 25, 2009
  Messages: 7,900
  Likes Received: 1,328
  Trophy Points: 280
  Hiyo mirenda na matambala ya kisiasa nani anayataka wameipeleka nchi yetu kwenye umaskini wa kutupwa halafu tuwarudishe wezi ,Lowassa hana soko Tanzania musituchoshe
   
 18. F

  Froida JF-Expert Member

  #18
  Aug 29, 2012
  Joined: May 25, 2009
  Messages: 7,900
  Likes Received: 1,328
  Trophy Points: 280
  Duh huyu chokoraa wakisiasa kaanza kulipa magazeti na watu wakuja kutuchock na masifa ya mwizi huyu anafanya kama walivyomuungiza marehemu wa kiutawala Jakaya Kikwete Lowasa asipoteze muda mwizi huyo
   
 19. Yericko Nyerere

  Yericko Nyerere Verified User

  #19
  Aug 30, 2012
  Joined: Dec 22, 2010
  Messages: 16,212
  Likes Received: 3,774
  Trophy Points: 280
  Sasa wamuweke nani agombee kupitia ccm ili amsindikiza Rais Dr W. Slaa ikulu?
   
 20. Yericko Nyerere

  Yericko Nyerere Verified User

  #20
  Aug 30, 2012
  Joined: Dec 22, 2010
  Messages: 16,212
  Likes Received: 3,774
  Trophy Points: 280
  Hehehe kwahiyo haya utawala wa jk unauona ni sawa tu?
   
Loading...