JK Baada ya Mawaziri mulika Manispaa ya Ilala

Shanat

Member
Mar 5, 2012
11
4
Kiasi fulani sasa nimeamini JK akiamua anaweza! Ombi langu kwa JK aonyeshe mfano kwa halmashauri ya manispaa ya Ilala kuna mada iliisha letwa humu JF juu ya ubadhilifu unao fanywa na meya wa manispaa hiyo kwanza kabisa lawama hizo ziuendee uongozi wa Manispaa hiyo mkurugenzi na timu yake niwatu walioshindwa kuwajibika ni viongozi wenye nidhamu ya woga wamewaachia madiwani ndiyo waendeshe shughuli zote za halmashauri maana sasahivi watumishi wamekuwa wakiwajibika kwa meya na madiwani wake maana wao ndiyo wanapanga kazi kwa ujumla halmashauri imepoteza muelekeo kabisa.chaajabu meya ndiyo amekuwa mwajili ushahidi ni mgambo ambao sasahivi wamesimamishwa kisa meya kachukua tenda ya askari ambao siku si nyingi ukweli utadhihiri.ila kwa kujihami anawaita waandishi wa habari ambao kila siku wanapigana vikumbo ofisini mwake ILA TAHADHALI YANGU KWA MKURUGENZI AJUE KWAMBA YALIYO MKUTA LUBUVA NDIYO NA YEYE YATAMKUTAIWAPO ATAENDELEA KUMCHEKEA HUYO MEYA. Kuna wizi umebuniwa na baadhi ya hao madiwani kwa kisingizio cha kuunda tume ya kukusanya mapato badala ya kuwa ni tume ya kukusanya mapato imekuwa ni tume ya kutumia mapato. hebu CAG naye aimulike hiyo kamati ambayo inamaliza mwezi wa pili sasa imekusanya kiasi gani ukilinganisha na matumizi maana tunaona kinachofanyika ni kulipana posho tu na mchana ukifika wanaenda Peacock kupata Lunch,wamefuta posho zote na staili kadhaa za watumishi lakini wao kila siku wanalipana posho kwa vikao visivyo na mwanzo wala mwisho Ombi langu kwa mkuu wa nchi ni kuangalia upya uwepo wa madiwani kwenye ofisi za manispaa kama kweli manispaa ina jukumu la kukusanya mapato, madiwani ni kikwazo kikubwa sana bora utafutwe utaratibu mwingine wa kuwapatia kazi hao madiwani lakini sio kuwachanganya na watumishi wa halmashauri mfano mzuri ni wakati ule wa TUME YA KEENJA kazi ya JIJI ilikuwa inaonekana sio sasa ni majungu na kutishana tu.
 
Back
Top Bottom