JK azungumzia changamoto sekta ya afya nchini


MziziMkavu

MziziMkavu

JF-Expert Member
Joined
Feb 3, 2009
Messages
40,013
Likes
5,440
Points
280
MziziMkavu

MziziMkavu

JF-Expert Member
Joined Feb 3, 2009
40,013 5,440 280

Rais Jakaya Kikwete


Rais Jakaya Kikwete amesema changamoto kubwa iliyopo kwenye sekta ya afya inatokana na ongezeko la idadi ya watu.

Kikwete aliyaema hayo mwishoni mwa wiki iliyopita wakati wa kufungua mkutano wa 46 wa mwaka wa Chama cha Madaktari Tanzania (MAT) uliofanyika jijini Dar es Salaam.

Akisoma risala kwa niaba yake Waziri wa Ardhi Nyumba na Maendeleo ya Makazi, Anna Tibaijuka alisema kuwa sensa ya mwaka 2002 ilionyesha wazi kuwa idadi ya watu inaongezeka kwa haraka.

Alisema katika sensa ya tano iliyofanyika imeonesha kuwa idadi ya watu imefikia 44,929,002 kutoka watu 12,313469 ni ongezeko la 32,615531 ambalo ni karibu mara tatu ya idadi ya watu waliokuwepo wakati wa kupata uhuru.

Alisema ongezeko hilo kubwa la watu linaongeza changamoto katika kufikia malengo ya maendeleo ya milenia ifikapo mwaka 2015 hasa ikizingatiwa kuwa muda uliobaki ni mfupi.

Alisema pamoja na kuwepo kwa changamoto nchi imepiga hatua za kujivunia katika kufikia malengo ya maendeleo ya milenia.

Alizitaja hatua za kujivunia kuwa ni pamoja na kupungua kwa vifo wa watoto chini ya miaka mitano kutoka vifo 165 mwaka 1990 hadi 54 mwaka 2013 kwa vizazi hai 1000.

Alisema kupungua kwa vifo vya wanawake vinavyotokana na uzazi kutoka 578 mwaka 1990 hadi 454 mwaka 2011 kwa kila vizazi hai 100,000. aliwataka wananchi kufanya mazoezi, kuzingatia mlo kamili wenye lishe zote na kuacha kunywa pombe kupindukia.

Naye Rais wa MAT, Primus Saidia, alisema vurugu na kutoelewana hapo awali ni kutokana na madaktari kutokuwa na chombo chao cha kupeleka malalamiko yao.

Alisema kwa sasa wamekuwa na Baraza la Kutetea Madaktari na Wafamasia ambacho kitakuwa kinasimamia kilio chao.
CHANZO: NIPASHE

 
C

CHUAKACHARA

JF-Expert Member
Joined
Jun 3, 2011
Messages
12,383
Likes
4,021
Points
280
Age
59
C

CHUAKACHARA

JF-Expert Member
Joined Jun 3, 2011
12,383 4,021 280
Mama Tibaijuka, anzisha mkakati wa kupunguza ongezeko hili kubwa bila kuathiri haki za binadamu! Sera ya watoto 2 tu can work!
 
B

Bawa mwamba

JF-Expert Member
Joined
Mar 19, 2010
Messages
351
Likes
3
Points
0
B

Bawa mwamba

JF-Expert Member
Joined Mar 19, 2010
351 3 0
[/QUOTE]Naye Rais wa MAT, Primus Saidia, alisema vurugu na kutoelewana hapo awali ni kutokana na madaktari kutokuwa na chombo chao cha kupeleka malalamiko yao[/QUOTE].

PRIMUS UNAFIKI MWISHO WAKE MBAYA? 2006 uliwafanya wenzako nini ?Na leo unaongea nini?

we jamaa ni bonge la cameruni ,PUNGA MKUBWA wewe 
Fadhili Paulo

Fadhili Paulo

Verified Member
Joined
Sep 1, 2011
Messages
3,237
Likes
87
Points
135
Fadhili Paulo

Fadhili Paulo

Verified Member
Joined Sep 1, 2011
3,237 87 135
Ongezeko la watu siyo tattizo, tatizo ni matumizi mabaya ya pesa za walipa kodi. Watu milioni 45 ni wengi hadi kukosa vifaa na dawa hospitalini? kuna nchi zina watu milioni 70 na dawa zipo na kila kitu kipo hospitalini. Madini tunayo, ardhi tunayo, misitu, mabonde, gesi kila aina ya rasilimali mhimu tunayo halafu eti tupo wengi ndiyo maana sekta ya afya inapata changamoto?!!! ninachoka sana.
 

Forum statistics

Threads 1,264,279
Members 486,258
Posts 30,178,715