JK azishukia halmashauri nchini kwa ubadhirifu | JamiiForums | The Home of Great Thinkers

Dismiss Notice
You are browsing this site as a guest. It takes 2 minutes to CREATE AN ACCOUNT and less than 1 minute to LOGIN

JK azishukia halmashauri nchini kwa ubadhirifu

Discussion in 'Habari na Hoja mchanganyiko' started by MziziMkavu, Jun 11, 2010.

 1. MziziMkavu

  MziziMkavu JF-Expert Member

  #1
  Jun 11, 2010
  Joined: Feb 3, 2009
  Messages: 39,616
  Likes Received: 4,617
  Trophy Points: 280
  [​IMG]
  Rais Jakaya Kikwete  Rais Jakaya Kikwete amesema kuwa hatazielewa halmashauri nchini ambazo zitashindwa kuchukua hatua za kisheria kwa kuwafikisha mahakamani wale wote watakaobainika kufanya ubadhirifu wa fedha za umma.
  Rais Kikwete alitoa onyo hilo mjini hapa jana, wakati akifungua mkutano wa mwaka wa Jumuiya ya Tawala za Mitaa Tanzania (ALAT) katika ukumbi wa chuo cha Polisi Moshi (CCP).
  Alisema taarifa ya Mdhibiti na Mkaguzi Mkuu wa Hesabu za Serikali (CAG) na Kamati ya Bunge ya Hesabu za Serikali za Mitaa (LAAC) zinaonyesha kuwa bado kuna watumishi ambao sio waaminifu ,wadokozi na wezi kwani fedha za serikali zinaonekana kutumika, lakini kazi haionekani au haifanani na gharama iliyotajwa.
  Rais Kikwete alisema kuwa matatizo yanakuwa makubwa na hata kuota mizizi pale ambapo halmashauri husika hazichukui hatua sahihi kwa sababu viongozi ni wazembe au wanafumbia macho vitendo hivyo kwa kuwa wenyewe ni sehemu ya tatizo na matokeo yake wananchi kukosa huduma stahili na hivyo kupoteza imani kwa serikali yao.
  “Kwanini mnakuwa na kigugumizi katika kuwafikisha mahakani wezi hawa, mnataka muwajadili katika mabaraza ya halmashauri, mnataka kujadili wezi?” alihoji na kuongeza:
  “Sitawaelewa kamwe, mtu kaiba na mnajua ameiba ila mnataka mkamjadili kwenye kikao cha madiwani, mwaka 2006 nilisema hatuwezi kuacha fedha za halmashauri zitumiwe ovyo kama vile hazina mwenyewe.”
  Alisema wananchi wanalipa kodi na Serikali Kuu inachangia gharama za kuendesha halmashauri kwa matumani ya kuwahudumia wananchi.
  Aidha, Rais Kikwete aliwataka madiwani kuwa makini katika kuwasimamia watendaji kwa kuwa wakali dhidi ya wezi na wabadhirifu kwani huko ndiko kutetea maslahi ya wananchi waliowachagua.
  “Kwa kweli husononeka sana ninapoona wizi unatokea, madiwani wapo na hakuna hatua inayochukuliwa, hivi ni kwa sababu ya madiwani kuwa mbumbumbu au kwa kuwa wanakula nao?” alihoji na kuongeza: “Lazima tuwawajibishe wale wote wanaotumia fedha vibaya…tusiwafumbie macho.”
  Rais Kikwete alisema anasikitishwa sana anaposikia minong’ono kuwa baadhi ya madiwani wanatuhumiwa kuwa sehemu ya mitandao ya wizi katika halmashauri na kwamba huo ni utovu wa hali ya juu wa wajibu na ni kuvunja mkataba na wananchi.
  “Halmashauri ni madiwani, hakuna halmashauri bila ya madiwani, watendaji wako pale kuwasaidia madiwani kuendesha halmashauri, watendaji ni mkono wa kulia wa madiwani kwa ajili ya utekelezaji wa mipango iliyopangwa na madiwani,” alisema.
  Aliiagiza Tasisi ya Kuzuia na Kupambana na Rushwa (Takukuru) na Jeshi la Polisi kuzimulika halmashauri ili kubaini wale ‘mchwa’ wanaotafuna rasilimali hizo za maendeleo ya wananchi wanachukuliwa hatua bila ajizi.
  Vile vile, aliiagiza ALAT kushikilia bango jambo hilo kwa kuwaaibisha na kuwaadhibu vikali wale wanaobainika kutumia vibaya fedha za umma na kwamba ili wafanikiwe ni lazima wasiwe sehemu ya uovu huo.
  Alisema baadhi ya halmashauri zimefanikiwa kufanya vizuri katika ukusanyaji wa mapato baada ya kudhibiti vyanzo vya mapato na kwamba wapo waliokuwa jasiri kupitia upya mikataba waliokuwa wamewekeana na mawakala na kuirekebisha au hata kuivunja na kwamba katika halmashauri hizo uboreshaji wa huduma umeongezeka na kuwapa wananchi matumani ya kuboresha maisha yao na kuondoa umaskini.
  Alisema uwajibikaji na uadilifu wa watumishi katika Serikali za Mitaa ni suala muhimu sana katika azima ya kuboresha utoaji wa huduma kwani nidhamu katika utendaji ndio nguzo ya kuleta ufanisi na tija.
  Hata hivyo, aliitaka ALAT kuangalia uwezekano wa kuwa na miongozo itakayosimamia miiko na maadili ya wanachama wake na namna ya kudhibiti pale mwanachama mmoja anapokiuka maadili au miiko hiyo achukuliwe hatua.  CHANZO: NIPASHE
   
 2. d

  damn JF-Expert Member

  #2
  Jun 11, 2010
  Joined: Feb 22, 2010
  Messages: 585
  Likes Received: 4
  Trophy Points: 35
  Hana ubavu wa kumshukia ye yote
   
 3. jaxonwaziri

  jaxonwaziri JF-Expert Member

  #3
  Jun 11, 2010
  Joined: Feb 17, 2010
  Messages: 378
  Likes Received: 54
  Trophy Points: 45
  Sure thing, never seen him akimshukia mtu yeyote labda kundi la watu ambalo ni TUCTA. Tena kwa maneno!

  Shouldnt we correct there badala ya kusomeka ''....atamshukia mtu yeyote...." kwa sasa isomeke: "...atamsema mtu yeyote?"

  Sometimes I get the impression that our presidaa has his hands tied or something, he hardly gets something accomplished! Duh, what happened to him wandugu? This is so alarming and troubling at the same time!

  Ni mtazamo tu wandugu msijenge chuki na mtazamo wangu unatokana na muenendo wake!
   
 4. Jethro

  Jethro JF-Expert Member

  #4
  Jun 11, 2010
  Joined: Mar 23, 2009
  Messages: 2,223
  Likes Received: 98
  Trophy Points: 145
  Ati anajifanya kujua faire game kwenye kuiongoza nchi ati kila kitu kitafanyika kwa sheri haki itendeke since when TZ kuna haki sawa.

   
 5. B

  Bibi Ntilie JF-Expert Member

  #5
  Jun 12, 2010
  Joined: May 30, 2008
  Messages: 245
  Likes Received: 3
  Trophy Points: 0
  JK anaweza kubadilika kwenye awamu ya pili ya uongozi wake ili astaafu kwa 'amani'.
   
Loading...