Jk avunja rekodi ya kuongoza kudanganywa-asema slaa | JamiiForums | The Home of Great Thinkers

Dismiss Notice
You are browsing this site as a guest. It takes 2 minutes to CREATE AN ACCOUNT and less than 1 minute to LOGIN

Jk avunja rekodi ya kuongoza kudanganywa-asema slaa

Discussion in 'Uchaguzi Tanzania' started by Negotiator, Sep 18, 2010.

 1. Negotiator

  Negotiator JF-Expert Member

  #1
  Sep 18, 2010
  Joined: Aug 9, 2010
  Messages: 303
  Likes Received: 3
  Trophy Points: 0
  Vile vile Dokta Slaa, alisema Rais Kikwete amevunja rekodi ya kudanganywa kuliko marais wote duniani katika miaka mitano iliyopita. Alisema mwaka mwaka 2007, JK alifungua mradi hewa wa maji huko Pwaga, Dodoma; mwaka 2009 Rais Kikwete aliletewa Ikulu mkurugenzi wa halmashauri isiyohusika na kukabidhiwa gari la wagonjwa; na alizindua hoteli moja ya kitalii mkoani Arusha, kesho yake ikavunjwa uzio na TANROADS, na mwaka huu alisaini kwa mbwembwe sheria iliyochomekwa vipengele ambavyo havikujadiliwa Bungeni; na kwamba hata baada ya matukio yote hayo, hakuna mtu aliyewajibishwa.

  Mwaka huu, siku alipozindua kampeni za CCM mkoani Mwanza, JK aliwaeleza wananchi kwa mbwembwe, kuwa Mbunge wa Nyamagana, Lawrence Masha, alikuwa amepita bila kupingwa; jambo ambalo Dk. Slaa alisema si kweli kwani mgombea wa Chadema alikuwa ameweka pingamizi, ambalo hatimaye limemrejesha ulingoni. "Ama JK alidanganywa na Masha au alijidanganya mwenyewe au hakuwa makini…Kikwete si makini. Awaombe radhi wananchi wa Nyamagana kwa kuwadanganya."

  Alisema Kikwete amekuwa rais wa majaribio, na kwamba miaka mitano inatosha. "Imetosha, Kikwete aende akapumzike, muda wake umekwisha, miaka mitano inamtosha. "Hatuwezi kwa miaka mitano kuendelea kuwa na rais mtalii, asiyejua matatizo ya wananchi wake, anayetetea maslahi ya wawekezaji badala ya wananchi, asiye na visheni," alisema.Dk Slaa alidai hata mipango mkakati kama MKURABITA, MKUKUTA na hata MINI-Tiger, hata na barabara anazojivunia JK kujenga ni za awamu ya tatu ya Rais Mstaafu Benjamin Mkapa, si zalo la awamu ya nne.

  TEMBELEA http://ngurumo.blogspot.com/ KWA HABARI ZAIDI( SLAA ACHARUKA MWANZA)
   
 2. m

  muhulo Member

  #2
  Sep 18, 2010
  Joined: Jul 15, 2010
  Messages: 43
  Likes Received: 0
  Trophy Points: 0
  Hata ahadi za jay key na ccm zikiwa nzuri vp ikiwa hakuna uwajibishwaji kwa watendaji ambao wengi wao wamepewa dhamana kwa kujuana pasipo hata kuonyesha uzalendo hata ule wa kinafiki mpaka wana dare kumdanganya bosi wao hii ni zaidi ya hatari kwa taifa na raia mmoja mmoja kufikia kule wanapotuhubiria kwamba wanatungoza. Watanzania tushughurishe ubongo wetu hada kidogo harafu ucruhusu tamaa ya mda mfupi kuharibu future ya wale wote unaowajari
   
 3. Njowepo

  Njowepo JF-Expert Member

  #3
  Sep 18, 2010
  Joined: Feb 26, 2008
  Messages: 9,297
  Likes Received: 381
  Trophy Points: 180
  Alafu pamoja na yote hayo bado hajistukii
   
Loading...