Kiranga
Platinum Member
- Jan 29, 2009
- 87,809
- 152,949
Kwa kukujulisha tu, katika taratibu za UN, unapokabidhiwa chapter 7 mandate ya UN charter, maana yake ni ruksa kujibu mapigo unaposhambuliwa. Hiyo ndo maana yake ndugu yangu! Hizo terms of reference ni kwa ajili ya utendaji wa jumla wa Misheni yenyewe lakini sio katika utendaji wa Majeshi yake. Sikutaka kulisema hili awali, lakini acha niliseme sasa, ukweli ni kwamba majeshi yetu yalijibu mapigo yaliposhambuliwa Juni mwaka jana kule Darfur lakini yalizidiwa nguvu kutokana na wale maadui kuwa na zana nzito zaidi. Tatizo lililopo katika operesheni ya Darfur ni kwamba Misheni inafanya kazi katika mazingira ya Taifa lenye 'serikali imara' kiasi kwamba inaweka vikwazo pale majeshi ya UN yanapotaka kuingiza silaha nzito--ni sawa na kuruhusu majeshi ndani ya majeshi!! Ushauri wangu ni nchi wanachama wa UN zenye majeshi Darfur, kupitia vikao vya UN, kuishinikiza 'serikali yenyeji' kuruhusu majeshi hayo ya UN kuingiza silaha nzito angalau kwa kiwango fulani ili yanaposhambuliwa yaweze kujibu mapigo kisawasawa. Huu ndio ushauri ambao mimi binafsi naweza kuutoa kwa kiwango changu cha uelewa.
Hii resolution uliyoisema haiwezi kupita UN kwa sababu wakubwa wenyewe watahofia itakavyowaathiri ama wao directly ama sehemu yenye interests zao.
Umwambie Mrusi leo, ambaye ana veto, apitishe resolution ya kumfanya Mmarekani apeleke majeshi yenye silaha nzito kumtoa Assad Syria, wakati there is still a cold cold war, hawezi kuipitisha.
Ndiyo maana nikasema Kikwete ama anaridhisha wananchi waone kuna kitu anafanya au yuko really naive.
UN hata kitu kidogo tu kinazua bonge la zogo, itakuwa haya makubwa yanayoweza kuathiri balances za geopolitics?