Jk aponya madonda na maumivu ya wapinzani | JamiiForums | The Home of Great Thinkers

Dismiss Notice
You are browsing this site as a guest. It takes 2 minutes to CREATE AN ACCOUNT and less than 1 minute to LOGIN

Jk aponya madonda na maumivu ya wapinzani

Discussion in 'Uchaguzi Tanzania' started by wakushanga, Nov 8, 2010.

 1. w

  wakushanga JF-Expert Member

  #1
  Nov 8, 2010
  Joined: Nov 4, 2010
  Messages: 538
  Likes Received: 0
  Trophy Points: 33
  Ni mesikia katika vyanzo vya habari kuwa kauli ya JK, amewaambia wananchi kuwa uchaguzi umeisha kwa ivyo sasa ni wakati wa kuponya madonda ya uchaguzi, aidha amewataka watanzania kusahau yote yaliyo tokea na kuelekeza mawazo yao katika mambo mengine.

  sasa hisia zangu wana JF mimi bado vidonda havijapona na vinamaumivu yapo sana tu, kwa mawazo yangu wananchi wangeombwa radhi kwa uwongo uliofanywa na nec

  hii itasaidia kidogo kuponya hayo madonda yetu, lakini kura ziibwe na madonda yapone tu.....jamani kweli......!!!!

  hili jamani halijakaa vizuri!!!! sijui mnalionaje hili
   
 2. Profesa

  Profesa JF-Expert Member

  #2
  Nov 8, 2010
  Joined: Oct 28, 2010
  Messages: 902
  Likes Received: 93
  Trophy Points: 45
  Wakati mwingine ni vema kujifunza badala ya kujifua, haya yote yaliyokuwa na kasoro, hasa kwa nyinyi vyama vya upinzani mmeweka mkakati gani kuhakikisha hayatokei?

  Hakuna sababu ya kuendelea kugombana, ila kupambana kidiplomasia kwa kuweka pressure ya kisayansi tengenezeni realistic stratergies!

  Nawaambia imarisheni chama chenu, unganisheni wanachama anzisheni shughuli za kichama na muwe wengi muwe na ushawishi mkubwa wakati wa uchaguzi muone kama haitakuwa tofauti.
   
 3. Kigogo

  Kigogo JF-Expert Member

  #3
  Nov 8, 2010
  Joined: Dec 14, 2007
  Messages: 20,498
  Likes Received: 1,453
  Trophy Points: 280
  we unaongea nini bana?unataka kutukanwa hapa watu tupewe BAN
   
 4. Henge

  Henge JF-Expert Member

  #4
  Nov 8, 2010
  Joined: May 14, 2009
  Messages: 6,762
  Likes Received: 78
  Trophy Points: 145
  Madonda ni mengi sana:
  JK kuita CHADEMA ni chama cha kidini ni donda ambalo haliwezi kufutwa kilahisi bila kukanusha
  Kuita CUF ni chama cha kidini pia ni donda jingine kubwa!
  Kuita chadema ni chama cha kikanda hilo donda linaweza kufutika just kwa maneno au kwa kutamka amefanya kuwa kubwa zaidi!
  Haya madonda yanaweza kufutika kwa kupigana na ufisadi kwa nchi nguvu zote,
  Adui yetu mkubwa ni ufisadi hata msijalibu kuleta hoja za ajabu huku tukiiibiwa!
   
 5. S

  Sheka Senior Member

  #5
  Nov 8, 2010
  Joined: Oct 4, 2010
  Messages: 114
  Likes Received: 3
  Trophy Points: 35
  wewe kweli hamnazo bila kufanya marekebisho ya hii tume ya uchaguzi hata wa-TZ wote wawe wapo upinzani itakuwa ngumu kushinda mifano ipo hebufikiaria mkuu wa wilaya ana amrisha watendaji wahalmashauri wafanye wawezavyo kuhakisha upinzani haushindi kwenye eneo lake eti ikitokea hivyo kibarua hana na huu ndo msingi wa uchakachuaji wa kura sasa ktk hali hii hiyo mikakati inatakiwa ianzie kwenye marebibisho ya hilodubwashika tume NEC
   
 6. Kituko

  Kituko JF-Expert Member

  #6
  Nov 8, 2010
  Joined: Jan 12, 2009
  Messages: 9,365
  Likes Received: 7,001
  Trophy Points: 280
  hakuna kitu kibaya kama kupandikiza Udini na ukabila, JKaliona vitakuwa ni vya kupita lakini kwa baadhi ya watu hivyo vitu havitoki na taratibu vinawaingia watu na mwisho wa siku tutakuja kujuta
   
 7. sijui nini

  sijui nini JF-Expert Member

  #7
  Nov 8, 2010
  Joined: Sep 29, 2010
  Messages: 2,382
  Likes Received: 306
  Trophy Points: 180
  JK anataka kujikosha tu kwa watu...kuporomoka kwa zaidi ya 20% si kitu kidogo!!
   
 8. Masikini_Jeuri

  Masikini_Jeuri JF-Expert Member

  #8
  Nov 8, 2010
  Joined: Jan 19, 2010
  Messages: 6,809
  Likes Received: 364
  Trophy Points: 180
  Profesa kasema kweli; kuna uwezekano mkubwa kabisa ya yaliyojiri kuruhusiwa na kutokea na upinzani wenyewe kwa kutojua ama kwa kujua!

  Na ngd yangu kalamu...................matusi yatakuondolea heshima uliyonayo! Tunaelekezana na sio kutukanana!:A S angry:
   
 9. w

  wakushanga JF-Expert Member

  #9
  Nov 8, 2010
  Joined: Nov 4, 2010
  Messages: 538
  Likes Received: 0
  Trophy Points: 33
  Kwani hii tume kunashida gani kama wakiirekebisha ikawa Huru na Haki jamani
   
 10. Edson

  Edson JF-Expert Member

  #10
  Nov 8, 2010
  Joined: Mar 7, 2009
  Messages: 9,200
  Likes Received: 718
  Trophy Points: 280
  mi nakwambia hili donda langu halitapona

  mi nakwambia as long as huyu jamaa( kikwete) yuko pale

  wala dawa siweki ntaliacha hivyo hivyo, wacha linuke
   
 11. d

  dotto JF-Expert Member

  #11
  Nov 8, 2010
  Joined: Sep 29, 2010
  Messages: 1,720
  Likes Received: 18
  Trophy Points: 135

  Yeye ndiye alikuwa akihubiri huo ujinga kuwa wapinzani wana tumia dini kuingia ikulu huku akijua kuwa alikuwa anataka kupata kura za uongo. Yeye mwenyewe afanye hiyo kazi kwa kuwa ndio ulikuwa mtaji wake.
   
 12. w

  wakushanga JF-Expert Member

  #12
  Nov 8, 2010
  Joined: Nov 4, 2010
  Messages: 538
  Likes Received: 0
  Trophy Points: 33
  kwani kama anajua ukweli hawezi akakubali tu kama sio kuomba radhi kuwa tume ilichakachua na kudanganya wananchi!!!???
   
 13. j

  junior2008 JF-Expert Member

  #13
  Nov 8, 2010
  Joined: Apr 27, 2009
  Messages: 528
  Likes Received: 0
  Trophy Points: 0
  JK aache kutoa kauli zake kirahisi rahisi hivyo wakati anajua yeye ndiye msababishaji mkubwa na amelazimisha kurudi ikulu kwa uchakachuaji kupitia taasisi yao NEC. Cha msingi ni kutoa tamko rasmi ya kuwaeleza umma wa watanzania na jamii ya kimataifa jinsi uchaguzi ulivyovurugwa na NEC ya CCM na msimamo wa CHADEMA. Zaidi ya hayo ni kujipanga vizuri kama chama na kudai haki ya kuwa na tume huru ya uchaguzi itakayoundwa kwa kushirikisha vyama vyote. Huo ujumbe wa dini uliowatembelea CHADEMA pekee yake mara mbili kabla na baada ya uchaguzi ni mamluki wa CCM pia.
   
 14. P

  PapoKwaPapo JF-Expert Member

  #14
  Nov 8, 2010
  Joined: Jun 5, 2008
  Messages: 380
  Likes Received: 3
  Trophy Points: 0
  anajua nini alichokifanya ndio maana amasema tuponye madonda eeeeh.......haya poni ivi ivi kaka
   
Loading...