JK aongeza sharti la rushwa msamaha wa wafungwa | JamiiForums | The Home of Great Thinkers

Dismiss Notice
You are browsing this site as a guest. It takes 2 minutes to CREATE AN ACCOUNT and less than 1 minute to LOGIN

JK aongeza sharti la rushwa msamaha wa wafungwa

Discussion in 'Jukwaa la Siasa' started by Zak Malang, Apr 27, 2010.

 1. Zak Malang

  Zak Malang JF-Expert Member

  #1
  Apr 27, 2010
  Joined: Dec 30, 2008
  Messages: 5,410
  Likes Received: 18
  Trophy Points: 0
  JK aongeza sharti la rushwa msamaha wa wafungwa

  By Sadick Mtulya, Nipashe

  WAFUNGWA wanaotumikia kifungo kwa kubainika kufanya makosa ya rushwa ni miongoni mwa watu ambao hawatanufaika na msamaha wa wafungwa 3,101 uliotangazwa jana na Rais Jakaya Kikwete kuadhimisha miaka 46 ya Muungano.

  Huku kukiwa na vita kali dhidi ya rushwa kubwa, rais ameongeza kipengele hicho ili kuzuia watu wanaotumikia kifungo baada ya kubainika kupokea au kutoa rushwa kunufaika na msamaha wake.

  Kwa kawaida msamaha wa rais huwa haujumuishi wafungwa ambao waliohukumiwa kunyongwa na waliohukumiwa adhabu ya kifo ambayo imebadilishwa na kuwa kifungo cha maisha, wanaotumikia kifungo cha maisha au makosa ya kujihusisha na biashara ya madawa ya kulevya.

  Wengine ni wafungwa hawanufaiki na misamaha ya rais ni wale waliopatikana na hatia ya kufanya makosa ya unyang'anyi wa kutumia silaha, wanaotumikia kifungo kwa makosa ya kupatikana na risasi au silaha.

  Pia, wafungwa wanaotumikia kifungo kwa makosa ya kujamiiana chini ya sheria ya sexual Offences Special Provisio Act 1998 ambao walifanya makosa dhidi ya watoto (defilement) na waliofanya makosa ya kubaka, kunajisi na kulawiti, huwa hawanufaiki na msamaha.

  Wengine wasionufaika na msamaha ni wale wanaotumikia makosa ya wizi wa magari kutumia silaha, waliohukumiwa kifungo kwa kosa la kuwapa mimba wanafunzi wa shule za msingi.

  Lakini kwa mujibu wa taarifa iliyotolewa jana kwa vyombo vya habari na Waziri wa Mambo ya Ndani ya Nchi, Lawrence Masha, msamaha huo kwa wafungwa 3,101 hautawahusu waliofanya makosa hayo ya rushwa.

  Uamuzi wa kuongeza kipengele hicho unaonekana unaunga mkono vita dhidi ya ufisadi ambayo imepamba moto katika kila ngazi, huku watu kadhaa wakiwemo mawaziri wa zamani, maofisa waandamizi ubalozini, wafanyabiashara wakubwa, maofisa wa juu katika taasisi za serikali wakiwa wamefikishwa mahakamani kujibu tuhuma za rushwa.

  Kwa ujumla taarifa hiyo inaeleza kuwa msamaha utahusu wale wanaotumikia kifungo kisichozidi miaka mitano ambao hadi jana walikuwa wametumikia robo ya vifungo.

  Kama ilivyo kawaida ya misamaha ya rais, wafungwa wengine watakaonufaika ni wale wenye magonjwa ya Ukimwi, kifua kikuu na saratani ambao wanaelekea kuwa katika siku za mwisho za maisha yao.

  "Wafungwa hao wagonjwa watathibitishwa kwanza na jopo la waganga chini ya uenyekiti wa mganga mkuu wa wilaya au mkoa," inaeleza taarifa hiyo.


  Pia wafungwa wengine waliopewa msamaha huo ni wazee wenye umri wa miaka 70 na zaidi ambao umri wao utathibitishwa na jopo la waganga chini ya mganga mkuu wa wilaya au mkoa.

  Wengine ni wafungwa wa kike waliofungwa gerezani wakiwa na mimba, pamoja na wale walioingia na watoto wachanga wanaonyonya.

  Wafungwa wengine walipewa msamaha ni wenye ulemavu wa mwili na akili ambao ulemavu wao utathibitishwa na jopo la waganga chini ya uenyekiti wa mganga mkuu wa wilaya au mkoa.

  Taarifa hiyo imeeleza kuwa wafungwa wengine ambao hawatanufaika na msamaha ni waliohukumiwa kifungo kwa makosa yanayohusu uharibifu wa miondombinu kama vile wizi wa nyanya za simu na umeme, njia za reli na transfoma.

  Pia wafungwa wengine ni ambao wanatumikia kifungo cha pili au zaidi, waliowahi kupunguziwa kifungo kwa msamaha wa rais na bado wanaendelea kutumikia sheemu ya kifungo kilichobaki.

  Wengine ni wafungwa wanaotumikia kifungo chini ya sheria ya bodi za Parole, 1994 na sheria ya Huduma kwa Jamii, 2002 pamoja na waliowahi kutoroka au kujaribu kutoroka chini ya ulinzi.
   
 2. Zak Malang

  Zak Malang JF-Expert Member

  #2
  Apr 27, 2010
  Joined: Dec 30, 2008
  Messages: 5,410
  Likes Received: 18
  Trophy Points: 0

  Hii ni joke kubwa: Kama lengo ni kuwabana wafungwa waliohukumiwa kwa rushwa kubwa, basi ni usanii tu, kama kawaida ya Muungwana huyu! Wangapi waliohukumiwa kutokana na rushwa kubwa wako jela?

  Huwezi ukaweka sharti hilo huku huna jitahida zozote za serious za kuwatupa gerezani wala rushwa wakubwa!
   
 3. Gaijin

  Gaijin JF-Expert Member

  #3
  Apr 27, 2010
  Joined: Aug 21, 2007
  Messages: 11,850
  Likes Received: 57
  Trophy Points: 0
  wafungwa wangapi tanzania walihukumiwa kwa kosa la kutoa au kupokea rushwa?
   
 4. SHUPAZA

  SHUPAZA JF-Expert Member

  #4
  Apr 27, 2010
  Joined: Aug 4, 2009
  Messages: 548
  Likes Received: 3
  Trophy Points: 35
  Sasa lengo la kuwasamehe hawa wala rushwa ni nini au warudi tena uraiani waendelee kutuumiza?
   
 5. Nyambala

  Nyambala JF-Expert Member

  #5
  Apr 27, 2010
  Joined: Oct 10, 2007
  Messages: 4,470
  Likes Received: 21
  Trophy Points: 135
  Huyu mkulu nae kila wakati sanaa tu!!!!!!!!!!
   
 6. N-handsome

  N-handsome JF-Expert Member

  #6
  Apr 27, 2010
  Joined: Jan 23, 2008
  Messages: 2,317
  Likes Received: 128
  Trophy Points: 160
  Aghhhhhhhhhhhhhhhhhhh
   
Loading...