JK aogopa kukatiza Arusha mjini | JamiiForums | The Home of Great Thinkers

Dismiss Notice
You are browsing this site as a guest. It takes 2 minutes to CREATE AN ACCOUNT and less than 1 minute to LOGIN

JK aogopa kukatiza Arusha mjini

Discussion in 'Jukwaa la Siasa' started by kitalolo, Jan 23, 2011.

 1. kitalolo

  kitalolo JF-Expert Member

  #1
  Jan 23, 2011
  Joined: Dec 4, 2006
  Messages: 1,846
  Likes Received: 13
  Trophy Points: 135
  Jana jk alienda chuo cha mafunzo ya kijeshi monduli kufunga mafunzo ya kijeshi kwa wanajeshi wa nyota moja, ila ilibidi ndege ikatue mojakwamoja jeshi, kisa eti hawezi kukatiza arusha anaogopa people's power. nashukuru mungu kuwa saa nyingine washauri wake huwa wanamshauri vitu vya maana kama wakati wa kampeni walivyomshauri asifiki mererani akamtuma dr. bilali maana kwenye kampeni za awamu ya kwanza aliwadanganya watu wa mererani kuwa akiwapa kura atawaaondoa wazungu kwenye migodi na kuwarudishia raia migodi yao na hakufanya hivyo. kwenye kampeni za awamu ya pili nilibahatika kuwa mererani na walikuwa wakimsubiri kwa hamu sana, watu wengi walikamatwa na kuwekwa ndani kwavile walikuwa wakiongea mitaani kuwa wanamsubiri wa watampiga na mawe. kama kuna mtu anaifahamu merari vizuri atafahamu jinsi wanaapolo na manyoka walivyochoka na waka tayari kwa lolote kama walivyomfanyia kitu mbaya mzee Mkapa wakati wa kampeni, hata maafa yalipotokea mogodini mkapa alienda pale wakati huo akiwa amekwishachaguliwa kuwa raisi na akawaambia watu wa merarini kuwa mlinirushia vumbi lakini leo maafa yametokea nimekuja kuwa pamoja nanyi sina kinyongo, hapo ndipo nilipogundua kuwa mkapa alikuwa na ustaarabu flani. sasa kwa hii ishu ya kikwete naona angekatiza jana watu wangejiuliza alikuwa wapi siku zote hizo mafaa yametokea arusha na bado kuna mgogoro hajaja wala kuonyesha kuwa yuko pamoja nao na leo hii akatize kwenda kufunga mafunzo ya kijeshi yaani. na kwa jinsi inavyooneka na wachunguzi wa mambo na Arusha watu wamekichoka chama cha wala na wana chuki ya hali ya juu na wako tayari hata kufa hivyo kujitoa muhanga si jambo la ajabu akaona akatize na ndege mpaka monduli, mkuu na bado mikoa ya kuogopa kwenda inazidi kuongezeka kuna siku utajikuta ukilazimika kutua nchi ya jirani au nchi za kiarabu umeanza kuogopa mikoa ya nchi yako mwenyewe? mwezio wa tunisia alitaka kukimbila ufaransa wakamkatalia wakamwambia mambo yako kwishinei we usifikiri haya mataifa makubwa unayoyatumikia wakiona mambo yako yameharibika watakusaidia watamwangalia yule anayeweza kuwasaidia kwa wakati whuo ndio wanajishika naye ujue na wao hawapendi sana jinsi unavyoendesha mambo hata kama kuna maslai yao. umeanza kuwa mkimbizi Arusha hizi ni dalili mbaya . nimewahi kupata maono na kuyatoa hapa jf na bado naona nguvu ya maono hayo kuwa uwezekano wa wewe kufikisha 2015 hii nchi ni mdogo na ya arusha ni mawingu tu ambayo ni dalili za mvua, mkuu naongea kama mrisho mpoto alisema akipa nauli atakuja naona bado hajapata nauli, nami nakwambia ukianza kuikimbia arusha kuna siku utaikimbia Tanzania.

  nawasilia
   
 2. j

  jerry monny Member

  #2
  Jan 23, 2011
  Joined: Dec 6, 2010
  Messages: 94
  Likes Received: 0
  Trophy Points: 0
  yaliyotoke tunisia kwa bongo yataanzia A town,jikumbushe azimio la Arusha maudhui yake yalikua nini.alipo fika uwanja wa ndege tamko lake la kwanza lilikua vurugu zimeisha?sijui ingekua vipi kama jibu lingekua bado zinaendelea,akumbukuke uhai wa watu uliopotea siku ile uko mikononi mwake,na damu ya mtu haimwagiki bure ita mcost kwa namna moja au nyingine.angekua mstaarabu angesema jamani poleni kwa msiba uliowapata,kuulizia kama fujo zinaendele ni dharau,au ndio u doctor wake anaotunukiwa kila aendako,u docto sio rahisi kama mnavyompa jamani.anaharibu sifa ya ma doctor wengine,amekua kama wamiliki wa magari,linapopata ajali badala yakutaka kujua kama dereva na watu wengine wamesalimika yeye anakimbilia kuuliza kama gari limeharibika. MUNGU inusuru Tanzania kwenye mikono ya wahujumu.
   
 3. Lizzy

  Lizzy JF-Expert Member

  #3
  Jan 23, 2011
  Joined: May 25, 2009
  Messages: 22,224
  Likes Received: 244
  Trophy Points: 160
  Na bado..mpaka aiogope Tanzania!
   
 4. R

  Ray 4 Member

  #4
  Jan 23, 2011
  Joined: Dec 4, 2010
  Messages: 37
  Likes Received: 2
  Trophy Points: 15
  Yaliyotokea A Town ni dibaji ya Anguko la Mkwere. Nashauri waandishi wa vitabu ya hadithi wanukuu matukio na kuyaandikia kitabu. Pengine wanaweza kupata senti kadhaa kutokana na anguko lake.
   
 5. G

  Gad ONEYA JF-Expert Member

  #5
  Jan 23, 2011
  Joined: Oct 26, 2010
  Messages: 2,641
  Likes Received: 4
  Trophy Points: 135
  Kwani arusha ishakuwa tunis kiongozi anaikimbia? eh, people's power!
   
Loading...