JK angeliukwaa urais 1995 mambo yangelikuwa tofauti | JamiiForums | The Home of Great Thinkers

Dismiss Notice
You are browsing this site as a guest. It takes 2 minutes to CREATE AN ACCOUNT and less than 1 minute to LOGIN

JK angeliukwaa urais 1995 mambo yangelikuwa tofauti

Discussion in 'Jukwaa la Siasa' started by Byendangwero, Jul 3, 2012.

 1. B

  Byendangwero JF-Expert Member

  #1
  Jul 3, 2012
  Joined: Oct 24, 2010
  Messages: 872
  Likes Received: 4
  Trophy Points: 0
  Kwa vigezo vyovyote vile, hali ni tete sana hapa nchini mwetu.Mifarakano ya kila aina inayoikabili nchi yetu inatishia kumega taifa ili katika vipande vipande. Kuna mgawanyiko kwa msingi wa kipato unao sababishwa na kutupiliwa mbali kwa dhana ya uongozi ni dhamana, na badala yake kukumbatia dhana ya kwamba mbuzi anakula kulingana na urefu wa kamba yake; kuna mgawanyo kwa msingi wa dini, ambao unaendelea kukua kila ukicha hasa kutokana na serikali kunyamazia vitendo na kauri za uchochezi zinazotolewa na wale wenye misimamo mikali; kuna mgawanyiko kwa msingi wa utaifa, unaohusu Tanzania bara na visiwani, katika suala hili serikali ya muungano haiwezi kukwepa lawama kwa kuruhusu serikali ya visiwani kuendelea kuvunja katiba ya muungano mara kwa mara.

  Kwa maoni yangu mbengu iliyozaa mtafaruku tunao ushuhudia hivi sasa, ilipandikizwa wakati wa utawala wa Mkapa. Na ilihitaji mtu wa aina ya Mkapa,mwenye kujiamini na asiye mwoga kusimamia yale anayoyaamini, kuweza kufanikisha jambo hilo. Ikumbukwe, madhalani ujenzi wa tabaka la watu wachache walionacho, ulihitajika kwenda sambamba na kufutiliwa mbali kwa dira ya taifa iliyoongoza nchi hii kwa karibu miongo mitatu na nusu. Dira hiyo ilikuwa na waumini wengi katika ngazi zote za uongozi na hivyo ilimlazimu rais Mkapa kutumia nguvu nyingi kuvunjilia mbali upinzani mkubwa uliokabili sera zake. Nakumbuka ilifika wakati akaacha kushirikisha vikao rasmi vya chama chake katika masuala muimu ya kitaifa.

  Kwa hulka yake KJ hasingeliweza kuimiri vishindo hivyo vilivyo ambatana na ubadirishaji wa dira ya taifa, hivyo iwapo angelifanikiwa kuukwaa urais mwaka 1995, nchi yetu ingilikuwa bado inazingatia misingi ya utu na usawa wa binadamu, kinyume na sasa ambapo nchi yetu inaongozwa kwa msingi wa kujitafutia utukufu binafsi bila ya kujali maslahi ya taifa
   
 2. t

  tara Senior Member

  #2
  Jul 3, 2012
  Joined: Jun 5, 2012
  Messages: 190
  Likes Received: 0
  Trophy Points: 33
  Sasa hapa unatuambia udhaifu hapa sio wa kikwete wala ccm yake bali ni matokeo mabovu ya uwongozi wa Mkapa...Kikwete alishindwa vipi kuyaondoa hayo madudu kipindi yako mafano wa mchicha na kuyaaacha kukua na kufikia mfano wa mbuyu.....huu si ndo wehu huu......uwozo uwozo tu..............Hapa wa kulaumiwa ni sisi wananchi kwa kumpa miaka mingine mitano huyu mr.DHAIFU kutuongoza tena kwa kasi zaidi,nguvu zaidi na ari zaidi kuelekea katika maisha duni zaidi(sawa wapo watakao sema sio wote wana maisha duni,ila gap limeongezeka katika alienacho na asiye nacho)..............
   
Loading...