JK angani tena

Hivi ule mshipa wake wa aibu ulikatika? Maana ana kila rasilimali nchini kwake na anawauzia wao afu bado anaenda kuwaomba wakimpa zinaishia mifukoni mwa watu wachache afu bila hata aibu anaipeleka sura yake tena na tabasamu juu anataka tena huku serikali yake ikishutumiwa na kila aina ya baya, sura ingewezekana kuificha mfuko ningekushauri uende ukiwa hivyo ila kwavile haiwezekani basi kaa na tafakari kisha tulia nyumbani simamia vyema matumizi ya rasilimali zako utaendelea bila kuwa omba omba. Kwazi kwako Jk kabla hayajakushinda
 
Probably Tanzania is part of Eurozone....maana hizi safari inawezekana zimeshatuunganisha na nchi za mashariki ya mbali badala ya East Africa.
Heeheeeheee! Tatizo ni kuwa hata nchi za far-east haziko ndani ya Eurozone!
 
labda watu weusi tuna laana...huu umasikini na milasilimali yote hii..wao hawaji,yeye ndio anaenda tu,kuna haja ya kuidiscuss wizara ya mambo ya nje kwenye katiba
 

Anafahamu watanzania walivyo wajinga kwake hawawezi kufanya kitu chochote, anatawala misukule
 
Kweli lakuvunda halina ubani. Tumeingia choo cha kike, lol!!!!
 
Mpiga picha/rafiki yake (michuzi) ameshatangulia, angalia kwenye blogu yake (michuzi) ameshauza sura akiwa kwenye snow. safari hiyo ipo kweli lakini details bado.
 
Jamani, pia kuna swala la kucheki 'afya' si mnajua tena bandugu.

Kama ni suala la afya yake , mganga wake kisha mwambia afya yake tete atulie nyumbani asisafiri safiri ama sivyo atakuja dondoka barabarani!! Lakini huyu mkweree mbishi hata kwa waganga wake anang'ang'ania per diem za ulaya.
 
Nimesikia leo kwny News kwamba kale kandege kake kako juu ya mawe kwa miezi miwili sasa! kako nje ya nchi kwa matengenezo, ndo maana ametulia kwa muda sasa!😛oa

DUh hivi hii ndege ilinunuliwa na nani vile ? naomba nikumbushe !
 
Kama ni suala la afya yake , mganga wake kisha mwambia afya yake tete atulie nyumbani asisafiri safiri ama sivyo atakuja dondoka barabarani!! Lakini huyu mkweree mbishi hata kwa waganga wake anang'ang'ania per diem za ulaya.


Alishaambiwa akili za kuambiwa changanya na zako ! sasa wewe watakia nini tena? hebu mwacheni, hivi hamjui uchumi ukiharibika nchi za Ulaya nasisi tunaathirika jamani? mbona hivi lakini?
 
Mmemchosha na misiba yenu lukuki -- mwacheni akapumzike kidogo.
 
labda watu weusi tuna laana...huu umasikini na milasilimali yote hii..wao hawaji,yeye ndio anaenda tu,kuna haja ya kuidiscuss wizara ya mambo ya nje kwenye katiba
Tatizo kubwa kwetu waafrika tulijengewa inferiority culture ya kudhani kila kitu hatuwezi kufanya bila miongozo au misaada ya wenzetu. Labda kitu tunachoweza kufanya bila misaada ni kuuana wenyewe kwa wenyewe, God show us the way
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…