‘JK anavunja Katiba’ | JamiiForums | The Home of Great Thinkers

Dismiss Notice
You are browsing this site as a guest. It takes 2 minutes to CREATE AN ACCOUNT and less than 1 minute to LOGIN

‘JK anavunja Katiba’

Discussion in 'Jukwaa la Siasa' started by nngu007, Jan 23, 2012.

 1. nngu007

  nngu007 JF-Expert Member

  #1
  Jan 23, 2012
  Joined: Aug 2, 2010
  Messages: 15,871
  Likes Received: 58
  Trophy Points: 145

  [​IMG]
  Na Jabir Idrissa - Imechapwa 11 January 2012

  [​IMG][​IMG]
  DK. Willibrod Slaa amemtuhumu Rais Jakaya Kikwete kuvunja Katiba ya Jamhuri ya Muungano wa Tanzania aliyoapa kuilinda.

  Akiongea na MwanaHALISI juzi Jumatatu, alisema vitendo vya rais havilingani na kauli anazotoa ambamo anadai kuongoza kwa misingi ya sheria na kuheshimu katiba.


  Dk. Slaa amesema kitendo cha Rais Kikwete kusamehe walioiba mabilioni ya shilingi kutoka Akaunti ya Madeni ya Nje (EPA) katika Benki Kuu ya Tanzania (BoT) ni ushahidi kamili wa kuvunja katiba.


  Miaka mitatu iliyopita Rais Kikwete alitangazia walioiba fedha za EPA kuwa iwapo watarejesha sehemu ya fedha walizoiba, basi serikali haitawapeleka mahakamani.


  Rais aliunda kile alichoita "Timu Maalum" kuchunguza walioiba fedha za EPA. Timu iliongozwa na Mwanasheria Mkuu Jonston Mwanyika.


  Wajumbe wengine walikuwa Inspeka Jenerali wa Polisi, Said Mwema na Mkurugenzi wa TAKUKURU, Edward Hoseah.


  Baada ya uchunguzi huo, rais alitangaza kuwa tayari ana majina ya wote waliokwapua mabilioni ya EPA. Alisema baadhi ya wakwapuaji walikuwa tayari wameahidi kurejesha fedha hizo.


  "Kauli ya rais iliondoa ukungu juu walioiba kutoka BoT. Wananchi walisubiri serikali itoe orodha ya wezi hao, lakini hadi leo haijawekwa hadharani," anasema Dk. Slaa kwa sauti ya masikitiko.


  "Rais anasema sana kwamba nchi inaendeshwa kwa sheria na kwamba anafuata katiba, hivyo serikali haiwezi kumhukumu mtu bila ya kuwa na ushahidi wa tuhuma zake," anashangaa Dk. Slaa.


  Anauliza, "Rais anataka ushahidi gani zaidi ya walioiba kukiri kuwa waliiba? Uko wapi ushahidi zaidi ya kurejesha ulichoiba? Tunachoona ni rais kutoa msamaha kwa wezi."


  "Rais aliwataka walioiba fedha za EPA wazirudishe na watakaoshindwa kuzirejesha watashitakiwa kisheria. Kweli, wapo walirejesha na mpaka leo hawajashitakiwa mahakamani.


  "Huku ni kuvunja sheria mama, kwani mtuhumiwa yeyote sharti apelekwe mahakamani kwa kuwa huko ndiko sheria itaamua iwapo ana hatia," amesema Dk. Slaa.


  "Hakuna popote katika katiba ya nchi panapotoa mamlaka kwa rais kusamehe mtuhumiwa kabla ya kuwa ameshitakiwa na kuhukumiwa.


  Akisisitiza, Dk. Slaa amesema, "Nimesoma katiba sijaona popote pale, kifungu kinachompa rais mamlaka haya ya kusamehe watuhumiwa ambao hawajafikishwa mahakamani."


  "Wala hakuna mahali popote ambako katiba inatoa mamlaka kwa rais kusamehe mwizi, tena aliyekiri waziwazi kuwa ameiba," ameeleza Dk. Slaa.


  Alipoulizwa sasa rais afanye nini, Dk. Slaa alisema, "Rais hajawaambia Watanzania ukweli wa jambo hili. Wapo watuhumiwa ambao bado hawajapelekwa mahakamani kushitakiwa kwa wizi wa fedha za umma."


  "Hili ni kosa zito kwa rais aliyeapa kulinda katiba. Kama anasamehe mtu ambaye hajapelekwa mahakamani kushitakiwa je, wale walioko magerezani watolewe kwa kuwa rais ana mamlaka ya kuwasamehe?" amehoji.


  Amesema nchi ikifikishwa hapo, ina maana viongozi wake hawaamini tena utawala wa sheria na kuongeza, "…hatua hiyo itasababisha nchi isitawalike kwani kila mtu aliyeko karibu au anayeweza kumfikia rais atafanya atakavyo akijua hakuna atakayemgusa."


  Wiki iliyopitam Dk. Slaa aliwaambia waandishi wa habari jijini Dar es Salaam kuwa Rais Kikwete hajawatendea haki Watanzania kwa kushindwa kuwashitaki
  watuhumiwa wa ufisadi.


  Alikuwa akitoa tathmini ya yaliyojiri na utendaji wa serikali katika mwaka 2011.

  Mapema Januari 2008, serikali ilitangaza orodha ya kampuni 22 zilizotajwa katika ripoti ya ukaguzi uliofanywa na maodita wa kimataifa kuwa zilichota zaidi ya Sh.130 bilioni kutoka BoT.

  Katika mkutano huo na waandishi wa habari, Dk. Slaa alitaja kampuni ambazo alisema zimerejesha Sh. 70.7 bilioni.


  Akiongea kwa sauti ya uchungu, Dk. Slaa alisema licha ya serikali kukataa au kushindwa kutoa hadharani orodha ya waliorejesha fedha hizo, bado pia haijaeleza ni kampuzi zipi zimekataa kurejesha fedha za wizi.


  Akizidi kushusha tuhuma, Dk. Slaa amesema bado serikali haijaeleza ukweli wa zilipohifadhiwa fedha zilizorejeshwa na waliokiri kuiba.


  Ajabu ya jambo hili, anasema katibu mkuu wa CHADEMA, "…ni kwamba rais haoni kuwa anawajibika kulieleza bunge masuala haya. Hii inaonyesha alivyo mzito katika kushughulikia tatizo la ufisadi."


  "Tena hapa tunarudi nyuma kule ambako watendaji wake wa vyombo vya uchunguzi waliwahi kusema kuwa, kuwashitaki watuhumiwa wa ufisadi wote waliokutwa wameiba kunaweza kuvuruga usalama wa nchi," alisema.


  Kauli hiyo ilikaririwa na mkurugenzi wa TAKUKURU, Edward Hoseah, IGP Said Mwema na Rais Mstaafu awamu ya pili, Ali Hassan Mwinyi.


  Wakati kiza kinaendelea kufunika ukusanyaji wa fedha na matumizi yake, Rais Kikwete amelihakikishia Shirika la Kimataifa la Fedha (IMF) kuwa atasimamia misingi ya utawala bora wa fedha.


  Katika barua yake kwa Mkurugenzi Mtendaji mpya wa IMF Christine Lagarde, rais amesema kumekuwepo changamoto katika mahusiano kati ya Tanzania na shirika hilo.

  Amesema, hata hivyo, serikali yake itajitahidi kuweka nidhamu katika menejimenti ya fedha. Barua ya rais iliwasilishwa kwa Lagarde na Waziri wa Fedha na Uchumi Mustapha Mkulo mwezi uliopita mjini Washington.

  Wachunguzi wa mambo ya siasa na uchumi wanasema, "…kama rais hawezi kuwa muwazi kwa Watanzania, atawezaje kuwa muwazi kwa IMF?"   
 2. Kimbunga

  Kimbunga Platinum Member

  #2
  Jan 23, 2012
  Joined: Oct 4, 2007
  Messages: 13,012
  Likes Received: 1,817
  Trophy Points: 280
  nadhani hii ilikuwa ni moja ya agenda za mkutano wa juzi!
   
 3. All TRUTH

  All TRUTH JF-Expert Member

  #3
  Jan 23, 2012
  Joined: Nov 20, 2011
  Messages: 3,277
  Likes Received: 985
  Trophy Points: 280
  duh. ila kila jambo lina mwisho
   
 4. MAMA POROJO

  MAMA POROJO JF-Expert Member

  #4
  Jan 23, 2012
  Joined: Nov 22, 2007
  Messages: 4,966
  Likes Received: 27
  Trophy Points: 135
  hakuna siku ninayotarajia kwamba Dr Slaa atamsifia Jk
   
 5. MAMA POROJO

  MAMA POROJO JF-Expert Member

  #5
  Jan 23, 2012
  Joined: Nov 22, 2007
  Messages: 4,966
  Likes Received: 27
  Trophy Points: 135
  Dr Slaa alishasema kaibiwa kura kwenye sanduku la kura sasa ni yapo mazuri tunafikiri atazungumza juu ya anayemwita mwizi wa kura? hakika anaweza hata kumtengenezea kesi Jk ili tu nchi isitawalike. kwa hakika sishangazwi na matamko mengi ya Slaa dhidi ya JK. Matamko haya yataendelea hadi mwisho wa utawala wa Jk .....amini usiamini.
   
 6. MAMA POROJO

  MAMA POROJO JF-Expert Member

  #6
  Jan 23, 2012
  Joined: Nov 22, 2007
  Messages: 4,966
  Likes Received: 27
  Trophy Points: 135
  agenda ya Dr Slaa dhidi ya JK bado inanipa utata
   
 7. Mag3

  Mag3 JF-Expert Member

  #7
  Jan 23, 2012
  Joined: May 31, 2008
  Messages: 9,094
  Likes Received: 6,188
  Trophy Points: 280
  Hapana MAMA POROJO, hayo unayoita matamko ya Dr. Slaa dhidi ya JK yanaweza kumalizika wakati wowote ule utawala huu utakapoamua kuiachia sheria kuchukua mkondo wake kwa Jakaya Mrisho Kikwete kuitii katiba aliyoapa kuilinda.

  Kikwete anatoa hukumu kwa kuamuru mwanachi anayedai haki yake apigwe risasi na hata kuuawa lakini anamsamehe mwizi wa mabilioni ambayo kama yangetumika vizuri yangempunguzia huyo mwananchi matatizo yanayomsukuma kudai hiyo haki.

  MAMA POROJO amini usiamini, hii nchi inatawalika hadi leo kwa sababu moja tu nayo ni matumaini waliyo nayo wananchi kwa watu kama Dr. Slaa kwamba hayo matamko yao iko siku yataleta mabadiliko kama pole pole tunavyoanza kushuhudia.

  Wahenga walisema kimya kingi kina kishindo na katu usitamani watu kama Dr. Slaa wakae kimya, wakifanya hivyo nchi hii inaweza kufikia hali ambayo tumeishuhudia ikitokea sehemu nyingi ambapo milango ya utawala wa sheria ilitiwa kufuli na funguo kutupwa.

  MAMA POROJO, ajenda ya Dr. Slaa itazidi kuwapa utata watu wote wale ambao walimwezesha Kikwete kuukwaa Uraisi mwaka 2010 baada ya kuonyesha katika awamu yake ya kwanza kuwa hana uwezo hata chembe wa kuumudu uongozi wa taifa.

  Ajenda ya Dr. Slaa itaendelea kuwapa utata watu kama MAMA POROJO ambao kama lilivyo jina lenyewe utawala bora unaweza kudumishwa kwa porojo, udanganyifu, utapeli, wizi, unyanyasaji, ubabe na ikibidi mauaji kama utawala huu wa Kikwete.
  MAMA POROJO huo unaouita utata, naomba mimi niuite hofu na woga kwa pamoja kwa sababu hauwezi kupata utata vitendo vya kihalifu kama wizi vinapokemewa isipokuwa pale ama wewe mwenyewe ni mwizi au mshiriki mkubwa katika vitendo vya wizi.
   
 8. Mkondakaiye

  Mkondakaiye JF-Expert Member

  #8
  Jan 23, 2012
  Joined: Dec 5, 2011
  Messages: 839
  Likes Received: 0
  Trophy Points: 33
  Je matamko hayo siyo ya ukweli? Watanzania tunapaswa kujenga utamaduni wa kusema ukweli na kuutetea
   
 9. Third Eye

  Third Eye JF-Expert Member

  #9
  Jan 23, 2012
  Joined: Jan 8, 2012
  Messages: 332
  Likes Received: 79
  Trophy Points: 45
  Dr Slaa bhana,asa alitegemea JK atoe majina na wakati na lake JK na la mtangulizi wake lipo?hahahaha hata ningekuwa mie ningejisamehe tu,
  viva JK, viva to Wizi
   
 10. p

  politiki JF-Expert Member

  #10
  Jan 23, 2012
  Joined: Sep 2, 2010
  Messages: 2,356
  Likes Received: 154
  Trophy Points: 160
  KATIBA KATIBA KATIBA NDIYO JAWABU PEKEE, Katiba iliyopo hivi sasa haiwapi wananchi mamlaka au nguvu ya kuweza kumwajibisha Rais directly. Katika mabadiliko ya katiba mpya lazima kiwemo kipengele kinachowapa wananchi si uwezo wa kumchagua Rais directly pia kiwepo kipengele cha kuweza kumshitaki rais siyo tu kwa makosa ya jinai bali hata pale inapoonekana dhahiri kushindwa kuchukua hatua kwa ajili ya sababu za kisiasa au kirafiki (incompetent).
   
 11. Duduwasha

  Duduwasha JF-Expert Member

  #11
  Jan 23, 2012
  Joined: Nov 3, 2010
  Messages: 5,142
  Likes Received: 2,177
  Trophy Points: 280
  Hizi habari mbona ni za siku za nyuma ... 11 jan 2012 leo 23 jan 2012??
   
 12. K

  Kisinga Member

  #12
  Jan 23, 2012
  Joined: Jan 18, 2012
  Messages: 6
  Likes Received: 0
  Trophy Points: 0
  Napita tu...hayo ya Dk Slaa na JK wananchi ndo wataamua
   
 13. K

  Kihodombi Member

  #13
  Jan 23, 2012
  Joined: Jan 23, 2012
  Messages: 39
  Likes Received: 0
  Trophy Points: 13
  kwenye ukweli uongo hujitenga
   
 14. nngu007

  nngu007 JF-Expert Member

  #14
  Jan 24, 2012
  Joined: Aug 2, 2010
  Messages: 15,871
  Likes Received: 58
  Trophy Points: 145
  Sidhani kama Rais wetu ana Uchungu na Nchi yetu; hasa mali za nchi zinakwenda wapi...
   
 15. W

  WildCard JF-Expert Member

  #15
  Jan 24, 2012
  Joined: Apr 22, 2008
  Messages: 7,477
  Likes Received: 70
  Trophy Points: 145
  JMK anavunja zaidi KATIBA kwa masuala ya Muungano wetu na Zanzibar. Kwa nini anawaacha hawa watoto kama Jussa watoe kauli na matamshi ambayo ni wazi yanavunja katiba ambayo yeye aliapa kuilinda siku yake ya kwanza ya Urais wake wa JMT? Kwa nini analiacha Baraza la Wawakilishi kutoa maazimio na kupitisha miswada ambayo ni kazi ya Bunge la Muungano?
   
 16. GeniusBrain

  GeniusBrain JF-Expert Member

  #16
  Jan 24, 2012
  Joined: Nov 3, 2010
  Messages: 4,321
  Likes Received: 18
  Trophy Points: 135
  Maskini huyu mzee wa watu anazeeka vibaya sana, hana jipya siku hizi ni yale yale tu. Ameanza kuchuja kwa kasi ya ajabu sana !

   
 17. MAMA POROJO

  MAMA POROJO JF-Expert Member

  #17
  Jan 24, 2012
  Joined: Nov 22, 2007
  Messages: 4,966
  Likes Received: 27
  Trophy Points: 135
  Jk hakuandaa katiba anayoivunja tutumie fursa aliyotupa kuandaa katiba mpya ili kuondao mapungufu.
   
 18. MAMA POROJO

  MAMA POROJO JF-Expert Member

  #18
  Jan 24, 2012
  Joined: Nov 22, 2007
  Messages: 4,966
  Likes Received: 27
  Trophy Points: 135
  Kila mtanzania ni mlalamikaji ni nani atatupa fikra mpya za kupambana na changamoto za maisha? tumepewa fursa ya katiba mpya badala ya kutumia muda wetu mwingi kujadili kasoro tunaendelea kulalamika
   
 19. MNAMBOWA

  MNAMBOWA JF-Expert Member

  #19
  Jan 24, 2012
  Joined: Oct 17, 2011
  Messages: 1,984
  Likes Received: 57
  Trophy Points: 145
  Mzee wewe huna aibu kbs au umeishiwa maneno ya kuwaambia watanzania?,, hv kati ya wewe slaa na jk nani ambaye aliiba kura za mwenzake?, kama kunasehemu washabiki walitaka kupata matokeo ya uchaguzi kwa ku2mia nguvu huo cyo wizi? Kwani Wagombe mlikuwa wewe na jk tuu? Dokita slaa wewe ndy mwizi wa kura unapaswa kutulia au tafuta jambo lingine la kuwaambia watanzania, staili yako ya vitukovituko sidhani kama utaweza kutatua matatizo ya watanzania ukiwa Rais wao.
   
 20. W

  WildCard JF-Expert Member

  #20
  Jan 24, 2012
  Joined: Apr 22, 2008
  Messages: 7,477
  Likes Received: 70
  Trophy Points: 145
  Aliapa kuilinda na kuitetea siku ya kwanza ya URAIS wake. Bunge letu nalo limelala tu. Katiba yetu ya sasa ina mazuri mengi tu yakilindwa na kutetewa na Rais ambaye ndie mlinzi mkuu wake. Wahuni wachache wa Zanzibar wanautumia udhaifu huu wa JMK kusema na kufanya watakalo.
   
Loading...