Akiwa katika ziara yake nchini Senegal, Obama alijikuta katika wakati mgumu kutokana na mwenyeji wake, Rais Macky Sall kupinga kauli yake ya kumtaka kurekebisha sheria zao za kutoa haki kwa makundi ya mashoga.
Rais huyo alipinga kauli hiyo, mbele ya wanahabari ambako alisema; ingawa Senegal ni nchi tulivu sana, lakini haiko tayari kuruhusu maingiliano ya ngono kati ya watu wenye jinsia moja, na hatuko tayari kubadili sheria kwa ajili ya kuwatambua kwa sababu nchi hii watu wake wengi ni waumini wa dini ya Kiislamu ambao wanakataa kusikia hilo likitokea.
Baada ya kuona sheria yake imeshindwa kupenya,Obama alisema kuwa nia yake katika mkutano huo haikuwa kufanya majadiliano ya suala hilo na Sally.