JK anaamini kila mtu anaweza kuwa rais! | JamiiForums | The Home of Great Thinkers

Dismiss Notice
You are browsing this site as a guest. It takes 2 minutes to CREATE AN ACCOUNT and less than 1 minute to LOGIN

JK anaamini kila mtu anaweza kuwa rais!

Discussion in 'Uchaguzi Tanzania' started by Mzizi wa Mbuyu, Jul 1, 2010.

 1. Mzizi wa Mbuyu

  Mzizi wa Mbuyu JF-Expert Member

  #1
  Jul 1, 2010
  Joined: May 15, 2009
  Messages: 5,497
  Likes Received: 1,061
  Trophy Points: 280
  Tatizo la Kikwete, ndiyoo.. huyu Raisi wetu..

  Yeye anaaamini mtu yeyote yule anaweza kuwa Raisi, cha muhimu ni mbinu tu tena hasa mbinu chafu kama alizotumia yeye mwaka 2005 kuhonga wanahabari na watu mbali mbali, ni mara nyingi amekuwa akisema mtu yeyote anaweza kuwa kiongozi yaani waziri, raisi, mbunge n.k yaani yeye Kingwendu, Bambo, Rage, Ridhwani, Joti, Alilungwa, Hawa Ghasia, N.K woote hao wanafaa sana tu kuwa maraisi wa Tz, kinachotakiwa ni fitna tu ya kufa mtu!

  Yaani yeye anajiona bonge la kiongozi mkuu 'levo" za kina Mwalimu .....................kama huamini angalia uteuzi wake wa viongozi..umejaa mashudu kibao!! angalia Sophia Simba, Masha, Hawa ghasia n.k

  Na sasa hivi anamtenenezea mwanae mazingira ya kuwa rais wa nchi hii baadae, na msishangae ikawa 2015!!! ausishngae akiamua mtasemaje????? yeye anaamini Ridhwani atakuwa bonge la raisi ....mbona yeye kaweza!, AU MBONA AMANI Karume kaweza!??
   
 2. N-handsome

  N-handsome JF-Expert Member

  #2
  Jul 1, 2010
  Joined: Jan 23, 2008
  Messages: 2,317
  Likes Received: 128
  Trophy Points: 160
  :twitch:
   
 3. Luteni

  Luteni JF-Expert Member

  #3
  Jul 1, 2010
  Joined: Jan 9, 2010
  Messages: 2,274
  Likes Received: 10
  Trophy Points: 0
  Mzizi wa Mbuyu

  Usikate tamaa BELIEVE ME OR NOT mwisho wa CCM umekaribia, CCM inachechemea inaanguka inasimamishwa inaanguka inasimamishwa (elewa siyo inasimama) mwisho wasimamishaji watachoka wataiacha ilale, ni sawa na kuku aliyekatwa kichwa atarukaruka mwisho ni kunyoosha miguu.

  CCM imekuwa kubwa kiasi kwamba hakuna mtu wa kuiweza kama enzi za Mwalimu, enzi zake zimefikia ukingoni itaishia kwa hawa kina Kikwete, kina Ridhwani wanamalizia makombo yake tu hawataifaidi vizuri, nakuhakikishia kubali kuwapa miaka minne ijayo halafu njoo kumbushia thread hii.
   
 4. Oxlade-Chamberlain

  Oxlade-Chamberlain JF-Expert Member

  #4
  Jul 1, 2010
  Joined: May 26, 2009
  Messages: 7,928
  Likes Received: 103
  Trophy Points: 160
  Ni kweli anachosema mtu yoyote anaweza kuwa kiongozi tanzania kutokana na yeye mwenyewe kuona kapewa nchi wakati hana uwezo wowote wa kuongoza.
   
 5. Mzizi wa Mbuyu

  Mzizi wa Mbuyu JF-Expert Member

  #5
  Jul 2, 2010
  Joined: May 15, 2009
  Messages: 5,497
  Likes Received: 1,061
  Trophy Points: 280
  Hiki chama kimekuwa cha wezi wakubwa nchini!!!
  Mkuu naomba na iwe sawa na utabiri wako, itakuwa ukombozi wa hali ya juu mno!!
   
 6. Ntemi Kazwile

  Ntemi Kazwile JF-Expert Member

  #6
  Jul 2, 2010
  Joined: May 14, 2010
  Messages: 2,145
  Likes Received: 8
  Trophy Points: 135
  Tehe tehe teheeee:roll:
   
 7. Mwanamayu

  Mwanamayu JF-Expert Member

  #7
  Jul 2, 2010
  Joined: May 7, 2010
  Messages: 7,939
  Likes Received: 2,088
  Trophy Points: 280
  Si amwachie mkewe, Salma, tuone!
   
 8. J

  Jafar JF-Expert Member

  #8
  Jul 2, 2010
  Joined: Nov 3, 2006
  Messages: 1,138
  Likes Received: 12
  Trophy Points: 0
  Kama ndiyo mawazo yake hayo - ana mtindio wa ubongo na ndio maana wafadhiri wamemstukia na visafari kapunguza
   
 9. Lucchese DeCavalcante

  Lucchese DeCavalcante JF-Expert Member

  #9
  Jul 2, 2010
  Joined: Jan 10, 2009
  Messages: 5,473
  Likes Received: 53
  Trophy Points: 145
  Kula tanmo mwana wane kama ndivyo anavyofikiria kweli hatuna Rais
   
 10. A

  August JF-Expert Member

  #10
  Jul 2, 2010
  Joined: Jun 18, 2007
  Messages: 4,505
  Likes Received: 723
  Trophy Points: 280
  Kikwete: Nina mke mmoja
  • Asema hakusudii kuoa, kuzaa tena

  na Salehe Mohamed


  [​IMG]
  RAIS Jakaya Kikwete jana alirejesha fomu zake za kuomba Chama Cha Mapinduzi (CCM) kimpitishe kuwa mgombea wake wa wadhifa huo, huku akisisitiza kuwa yeye ni mume wa mke mmoja na hakusudii tena kuoa.
  Kikwete aliyerejesha fomu hizo za urais baada ya kudhaminiwa na wanachama 25,000 wa CCM kutoka mikoa 10 ya Tanzania, aliwaomba wanachama wa chama hicho kumpa fursa ya kugombea kiti hicho ili hatimaye aweze kumaliza kazi aliyoianza.
  Akizungumza mbele ya umati mkubwa wa viongozi wa juu na makada wa CCM na serikali waliomsindikiza wakati akirejesha fomu za kugombea urais, aliomba apewe kipindi kingine ili amalizie kazi aliyoianza kwa mafanikio mazuri.
  “Nina mke mmoja na watoto wanane, pamoja na mwingine ambaye tulimuokota baada ya kutupwa na mama yake mara baada ya kujifungua, sitarajii kupata mke mwingine wala mtoto,” alisema Rais Kikwete, hali iliyowafanya watu waangue kicheko.
  Alisema pamoja na ukweli kwamba anacho kibali kwa mujibu wa dini yake ya Kiislamu kuoa wake wanne, anaamini hana sababu ya kufanya hivyo katika siku za usoni.
  Kikwete alilazimika kutoa ufafanuzi huo kutokana na kauli aliyoitoa Katibu Mkuu wa CCM, Yusuf Makamba, ambaye alisema kiongozi huyo alikuwa ana sifa zote anazopaswa kuwa nazo askofu isipokuwa alikuwa hana uhakika iwapo ile ya kuwa na mke mmoja ni sifa ambayo alikuwa nayo pia.
  Awali Makamba ambaye ndiye aliyepokea fomu za Kikwete na kuzihakiki alisema kiongozi huyo alikuwa na sifa zote za askofu za uadilifu, uchapa kazi na ile ya kutopenda pesa kama zilivyoandikwa katika kitabu cha Timotheo kwenye Biblia.
  Hata hivyo, si Makamba wala Kikwete aliyekuwa tayari kueleza kwa undani ni kwa sababu gani hasa hoja ya mke zaidi ya mmoja iliibuliwa katika hafla hiyo ya urejeshwaji fomu ambayo pia ilihudhuriwa na mke wa rais, Salma Kikwete.
  Tukio linaloweza kufananishwa na hilo ni lile lililotokea Machi 3, mwaka jana nchini Kenya, wakati rais wa nchi hiyo, Mwai Kibaki, alipoitisha mkutano wa dharura wa waandishi wa habari na kukanusha tetesi zilizosambaa za yeye kuwa na mke mwingine zaidi ya Lucy.
  Ingawa Makamba anakuwa kiongozi wa kwanza kueleza wasiwasi huo hadharani, hakujapata kuwapo taarifa zozote za wazi zinazoeleza kuhusu maisha binafsi ya Rais Kikwete.
  Hafla hiyo ya Kikwete kurejesha fomu ilishuhudiwa pia na umati mkubwa wa watu wakiwamo Waziri Mkuu, Mizengo Pinda, Waziri Mkuu wa zamani, Edward Lowassa, Mbunge wa Igunga, Rostam Aziz na Katibu Mkuu mstaafu wa CCM, Philip Mangula.
  Akizungumza katika hafla hiyo, Kikwete aliwaomba Watanzania na wanachama wenzake wamchague ili aweze kumalizia kazi aliyoianza katika miaka mitano ya utawala wake.
  Alibainisha kuwa watu wenye sifa za kuwania urais wapo wengi ndani ya CCM lakini hawajajitokeza kuwania nafasi hiyo kwa sababu ya kuwa na imani naye.
  Alisema hana cha kuwalipa ila anawaahidi Watanzania kuwa kazi aliyoianza katika utawala wake ataendelea nayo ili nchi iweze kupiga hatua kwenye maendeleo sambamba na kuwakomboa Watanzania katika lindi la umaskini.
  “Napenda kuwaahidi wanachama wenzangu na Watanzania kuwa mkinichagua nitaendeleza yale mafanikio tuliyonayo hivi sasa, naomba NEC na Kamati Kuu ya chama inipitishe na hatimaye wananchi wanichague kuwa rais wao Oktoba 31, niendeleze yale niliyoyaanza,” alisema.
  Rais Kikwete alitumia fursa hiyo kueleza kuwa aliamua kumkabidhi mwanawe Ridhiwan na marafiki zake fomu za kuomba wadhamini kwa sababu jukumu hilo si la chama, bali ni la mgombea binafsi na yeye kwa kuwa ana mtoto mkubwa ndiyo maana ameamua kumpa kazi hiyo.
  “Sijawadharau viongozi wa chama kama watu wanavyosema, bali mchakato huu unamhusu mgombea mwenyewe. Namshukuru Ridhiwan, Beno Malisa na marafiki zao kwa kutembeza fomu zangu za wadhamini mikoani,” alisema.
  Kwa upande wake Makamba alisema, Rais Kikwete ni mtaji mkubwa kwa chama hicho na kwa kuonyesha hilo amedhaminiwa na wanachama 14,690 katika mikoa yote, idadi ambayo ni kubwa kuliko iliyokuwa ikitakiwa ya wanachama 2,500 katika mikoa isiyopungua 10.
  Alibainisha kuwa wana CCM wenzake hawakutangaza nia ya kuwania kiti hicho ndiyo maana Mbunge wa Maswa, John Shibuda, aliyekuwapo katika hafla hiyo ya jana aliamua kutoendelea na nia yake ya kugombea kama alivyokuwa ametangaza awali.
  Alisema kuwa jina la kiongozi huyo linatarajiwa kupelekwa kwenye vikao vya Kamati Kuu na Halmashauri Kuu ya chama hicho kabla ya kufikishwa kwenye mkutano mkuu utakaofanyika Julai 10-11 ambao ndio utakaomteua mgombea wa urais, ambaye atapambana na wagombea wengine kutoka vyama vya upinzani.
  Naye mwakilishi wa mtandao wa wanafunzi wa vyuo vikuu (CCM), Harous Sanga, alitoa tamko la mtandao huo kuwa wataendelea kushirikiana na Rais Kikwete bega kwa bega mpaka hapo atakaposhinda urais.
  Akizungumza katika hafla hiyo, Shibuda alitoa shilingi 200,000 kuchangia kampeni za urais za Kikwete.
  Alisema kuwa alitangaza nia ya kutaka kuwania kiti hicho lakini baada ya kufanya upembuzi yakinifu, aliamua kutowania kwa sababu ya utendaji mzuri wa kiongozi huyo kwenye nyanja za uchumi, elimu, kilimo na nyinginezo. “Sikulazimishwa na wana usalama wala viongozi wa juu wa chama changu kutowania urais mwaka huu, dhamira yangu ndiyo iliyonituma, sikunyanyaswa na mtu, hii inadhihirisha kuwa Rais Kikwete anatuongoza kwa demokrasia,” alisema. Aliongeza kuwa Rais Kikwete si kiongozi mwenye fikra kandamizi, ndiyo maana kila mwanachama ndani ya chama hicho ana fursa ya kuwania uongozi kulingana na matakwa yake.


  " Ridhwani na Marafiki zake" hapo haoni kuwa hata huo umoja wa vijana kama hajabinafishwa , basi huko njiani kubinafsishwa.
  Kama Uongozi iwe kwenye CCM au serikali ni wa kidemokrasia mbona hakuna usawa katika kampeni na uteuzi, ume kaa kirafiki rafiki na kindugu?
  RA na mashabiki wake, EL na washabiki wake nk nk. Wezi wa EPA na Mashabiki wao
   
 11. Pengo

  Pengo JF-Expert Member

  #11
  Jul 2, 2010
  Joined: Oct 15, 2009
  Messages: 579
  Likes Received: 3
  Trophy Points: 0
  Huko sasa ni kuona gere tuu,huna lolote!
   
 12. Mzizi wa Mbuyu

  Mzizi wa Mbuyu JF-Expert Member

  #12
  Jul 4, 2010
  Joined: May 15, 2009
  Messages: 5,497
  Likes Received: 1,061
  Trophy Points: 280
  "Rais Kikwete alitumia fursa hiyo kueleza kuwa aliamua kumkabidhi mwanawe Ridhiwan na marafiki zake fomu za kuomba wadhamini kwa sababu jukumu hilo si la chama, bali ni la mgombea binafsi na yeye kwa kuwa ana mtoto mkubwa ndiyo maana ameamua kumpa kazi hiyo."

  Mkubwa kweli anaweza hata kumpa uraisi!!
   
 13. MwanaFalsafa1

  MwanaFalsafa1 JF-Expert Member

  #13
  Jul 4, 2010
  Joined: Feb 26, 2008
  Messages: 5,566
  Likes Received: 28
  Trophy Points: 135
  Lakini angesema si kila mtu anaye weza kuwa raisi si mgemuona ana majigambo na majivuno? Hakuna anaye penda kuambiwa hawezi kitu haswa na mtu ambae tayari yupo kwenye nafasi hiyo.
   
Loading...