Mwakalinga Bujo
JF-Expert Member
- Oct 22, 2008
- 2,719
- 1,440
Dahhh kwa kweli ni full magumashi, akivaa suti alizohongwa na kijana wa kiarabu unaona kweli kiongozi tumepata kumbe hana lolote maskin ya mungu, ubabaishaji mtupu, kuwa na kiongoz wa hivi ni mzigo kwa taifa, yan 2015 ni kama karne kwa watanzania.Duniani hayupo, ahera hayupo??!
tia maji tia maji....yani mguu kwenye break na kwenye accelerator.....ukiachia mafuta gari inazima, silence haipo.
Katika viongozi watakao weka historia mbaya nchini ,Rais huyu atakuwa wa kwanza.Nadhani washauri wake wameshindwa kusoma alama za nyakati.Yanayotokea Igunga ni chachu na picha ya mambo yatakavyakuwa tunakoelekea miaka ijayo hivi karibuni.
Kwa wanaofahamu falsafa ya Uongozi,kiongozi mkuu wa nchi (ambaye kwa Tanzania ni Rais).Viongozi hawa huchukuliwa kama ni watu wenye maono na karama za pekee kutoka kwa mwenyezi Mungu.Kiongozi mkuu wa nchi anapopita sehemu yoyote kama ilikuwa haina neema, itakuwa ni moja ya chachu na chanzo cha neema pindi atakapoondoka kutokana na matatizo atakayoelezwa na hatua madhubuti atakazo chukua kutatua kero/maswala mbalilimbali yanayogusa maendeleo ya eneo husika.
Yanayotokea kwa serikali ya mh. JK ni kutatua matatizo ya wanaomwanika hadharani kuwa yeye hana uwezo na karama ya kuwa kiongozi mkuu wa nchi (Vita hivi anapigana na wapinzani wake wa kisiasa ndani ya chama na nnje ya chama chake).Yapo mambo mengi ambayo kimsingi alitakiwa ayafumbie macho ili akimbilie kwa watetezi wake wamwisho ambao ni wananchi ( wapiga kura),kwa kusikiliza na kutatua kero zao.
Kiongozi ambaye hana umaarufu kwa wananchi wake siku zake za kukaa madarakani zinahesabika.Ni kitendo cha kustaabisha ukihesabu mambo yalimkumba Mh. Jk tokea ameingia madarakani,mfano kitendo cha msafara wake kupigwa mawe alipofanya ziara mkoani Mbeya.Matukio kama haya yanaweza yasipewe uzito kutokana na yanavyoripotiwa na vyombo vya habari.Ila ni kigezo kikubwa kwa kuangalia/kupima umaarufu wa kiongozi kwa wachambuzi /wafuatiliaji wa mambo.Kisiasa ni hatari sana kwa kustakabali wa kiongozi huyo.
Mambo mengine yanayodhihirisha kuwa kiongozi huyu amepoteza umaarufu ni kwenye mitandao ya kijamii.Mijadala mingi inayoendeshwa inakuwa inamkosoa na kumpinga wazi wazi kana kwamba sio Kiongozi wa nchi,mitandao ya kijaii ni muhimu kwa zama hizi kwani hutumika kama njia ya kuwasiliana baina ya mtu na mtu ,mtu na kundi ama kundi moja na kundi jingine.Nchi nyingine mitandao hii ya kijamii inatumiwa na viongozi kuwapasha habari wananchi na kutoa fursa ya kujadiliana/kushauriana maswala mbali mbali ya kijamii,kisiasa na kiuchumi.Kilichotokea tare 25/9/2011 wakati Rais alipoweka status na wachangiaji kuanza kuporomosha matusi ya wazi kuonyesha kuwa wamechoshwa na uongozi wake ni hatari sana.Kama watu unaowaongoza hawana imani na uongozi wako ni dhahiri unakosa/unapoteza sifa za kuwa kiongozi.
Yapo mengi yaliyotokea ila jingine ambalo litamtafuna sana Mh. Jk ni hili la hukumu ya leo -Tanesco iwalipe Dowans 94 bil. Tshs.Kweli Rais huyu hana washauri na hajaweza kusoma alama za nyakati ..Katika zama hizi za kiza /mgao mkali wa umeme,anaachia vyombo vilivyoko chini yake kufanya maamuzi bila kupima uzito wa jambo jenyewe.Anaamsha hisia za Watanzania kwa uchafu uliofanywa na watendaji wake!.Mbaya waliofanya uchafu huo wapo mtaani wanatembea na ma V8 kwa mbwembwe zote.
MUNGU IBARIKI TANZANIA.
Kosa hili la kuchagua mtu asiye na uwezo lisirudiwe tena. hii imetokana na pesa chafu za Rostam na Lowasa wanamtandao waliohonga wajumbe wa CCM na kumweka huyu mtalii madarakani
Nimejifunza jambo kwa JK. na nampongeza sana kwa ukomavu wa siasa, kwani pamoja na matusi, kashfa, maombi yote mabaya, na kutomtakia mema, ameendelea kuwa mvumilivu kisiasa sifa ambayo viongozi wengi duniani wameshindwa. chukua mfano tu wa vyama vingi ikiwemo vile tu ambavyo hata bado havijapewa dhamana kwa kiasi fulani inapofikia tu kiongozi kukosolewa anavyogeuka mbogo. angalia ya Mrema na mzee Tau, (TLP). Maamuzi zidi ya madiwani Arusha, na kwingineko ni baadhi tu ya ukosefu wa uvumilivu wa kisiasa.
Yapo mengi yaliyotokea ila jingine ambalo litamtafuna sana Mh. Jk ni hili la hukumu ya leo -Tanesco iwalipe Dowans 94 bil. Tshs.Kweli Rais huyu hana washauri na hajaweza kusoma alama za nyakati ..Katika zama hizi za kiza /mgao mkali wa umeme,anaachia vyombo vilivyoko chini yake kufanya maamuzi bila kupima uzito wa jambo jenyewe.Anaamsha hisia za Watanzania kwa uchafu uliofanywa na watendaji wake!.Mbaya waliofanya uchafu huo wapo mtaani wanatembea na ma V8 kwa mbwembwe zote.
MUNGU IBARIKI TANZANIA.
Hapo kwenye red ni 94bil. plus gharama za kesi natakataka nyingine
ambapo ki uhalisia ni 111bil.tsh.
kinachoniuma ni mahakama iliweka masharti ya kuwa DOWANS
hawaruhusiwi kufanya chochote bila ruhusa ya mahakama ila
cha kushangaza wakajiuza kwa SYMBION bila ya ridhaa ya mahakama.
leo hii mahakama hiyo nayo inatoa hukumu dowans ilipwe mimi sielewi
na sipendi kutoamini kama hakuna rushwa au mkono wa mkulu!!
Mwagito pole, nafikiri hujui maana ya Siasa ndo maana ukadhani kupuuza kwake maoni ya wanaotaka tija ya uongozi wake basi ndo ukomavu. Siasa sio ulaghai au blahblah, siasa ni sayanzi na inaendeshwa kwa utafiti na uhakika wa ukisemacho. Tafsiri ya siasa ni sayansi ya uongo ndiyo iliyomfikisha hapo huyu jamaa, alidhani akishasema jukwaani baasi yamekwisha, kumbe ndo kalianzisha, alidhani unaweza kuwadanganya watu wote kwa muda wote, kumbe sivyo, aghlabu mambo yake yanawafanya watu wengi wajisikie wanyonge na ukiwa katika kipindi chake cha uongozi. Ni kweli jamaa ni muungwana, anakiri kuwa mambo yamemshinda ndo maana badala ya kukemea, analalamika. Sasa sijui anataka nani afanyie kazi keroNimejifunza jambo kwa JK. na nampongeza sana kwa ukomavu wa siasa, kwani pamoja na matusi, kashfa, maombi yote mabaya, na kutomtakia mema, ameendelea kuwa mvumilivu kisiasa sifa ambayo viongozi wengi duniani wameshindwa. chukua mfano tu wa vyama vingi ikiwemo vile tu ambavyo hata bado havijapewa dhamana kwa kiasi fulani inapofikia tu kiongozi kukosolewa anavyogeuka mbogo. angalia ya Mrema na mzee Tau, (TLP). Maamuzi zidi ya madiwani Arusha, na kwingineko ni baadhi tu ya ukosefu wa uvumilivu wa kisiasa.