JK amteua Mwambene Mkurugenzi wa MAELEZO

JK amteua Mwambene Mkurugenzi wa MAELEZO

Ungekuwa msomaji wa magazeti haya ya Kiingereza ungelijua hili jina. Huyu Assah amewahi kuwa mwandishi wa Daily News kwa miaka kadhaa kabla ya kwenda wizara ya mambo ya nje

ninawasiwasi na umri wangu na wake! ninauhakika wakati anaandika ili gaazeti! sikuwa na mazingira haswaa ya kuweza kuwa mmoja wa anayesoma makala zake! labda nilikuwa bado kwenye level ya elimu ambayo yenyewe na daily newz haviendan, au uwezo wakununua ilo gaazeti haukuwepo, ndo foolish age nk, lakini kumjua namjua mana nina brother pale foreing na huwa naendaenda sana kuvuta zakuwekea budle za jf! sema sikujua kuwa ni alikua mwandishi wa gazeti ili ndo unanijuza afu kwanza twawaona kwa sura tu kwenye magari yao na koridoni au mapokezi!
 
I met with this guy once he is cheap minded and sikuweza kuelewa amekuwaje afisa habari pale mambo ya nje...leo mkurugenzi....daahh nchi hii bana...
Kigogo Naweza kukubaliana nawe somehow, lakini binadamu hubadilika
 
Last edited by a moderator:
Asah Andrew Mwambene ameteuliwa kuwa Mkurugenzi wa Idara ya Habari (MAELEZO) katika Wizara ya Habari, Vijana, Utamaduni na Michezo kuanzia tarehe 01 Julai, 2012. Bw. Mwambene anachukua nafasi iliyoachwa wazi na Bw. Clement Mshana ambaye mwaka jana aliteuliwa kuwa Mkurugenzi Mkuu wa Shirika la Utangazaji Tanzania (TBC).

Bw. Mwambene (41) kabla ya uteuzi huu alikuwa Kaimu Mkuu wa Kitengo cha Mawasiliano Serikalini katika Wizara ya Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Kimataifa. Aidha, Bw. Mwambene amewahi kufanya kazi katika Kampuni ya Magazeti ya Serikali (TSN) akiwa mwakilishi wa Kampuni hiyo huko Zanzibar.

Idara ya Habari (MAELEZO) ndiyo Msemaji Mkuu wa Serikali hapa nchini.

IMETOLEWA NA WIZARA YA HABARI, VIJANA, UTAMADUNI NA MICHEZO

AGOSTI 1, 2012

Source: Assah Mwambene ateuliwa kuwa Mkurugenzi Mkuu Mpya wa Idara ya Habari, Maelezo - wavuti
 
wanaudhi sana hawa watu mkuuIssue ndogo tuu wanaingiza maswala ya dini humoKwani dini yake ndio itasaidia utendaji wake wa kaziKuna watu hawana dini yoyote ila ni watendaji wazuri na kuna watu wenye dini ila hawafai kabisa kutokana na matendo yao
achana na hao wadini kaka, mods watu kama huyo jamaa inabidi wawe banned, wanadhan jf ni facebook
 
Back
Top Bottom