JK amteua Kairuki kumrithi Makamba
Tuesday, 30 November 2010 19:09 newsroom
Na Mwandishi Wetu
RAIS Jakaya Kikwete, amemteua Mbelwa Brighton Kairuki kuwa Msaidizi wa Rais katika masuala ya hotuba. Kwa mujibu wa taarifa ya Katibu Mkuu Kiongozi, Phillemon Luhanjo, iliyotolewa kwa vyombo vya habari mjini Dar es Salaam, jana, imesema kuwa uteuzi huo ulianza juzi.
Mbelwa Kairuki anachukua nafasi iliyoachwa wazi na Januari Makamba, ambaye amechaguliwa kuwa Mbunge wa Jimbo la Bumbuli mkoani Tanga. Kabla ya uteuzi huo, Kairuki alikuwa Ofisa Mambo ya Nje na alikuwa Msaidizi wa Waziri wa Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Kimataifa, Bernard Membe.
source:JK amteua Kairuki kumrithi Makamba