Bw. Eric Shigongo
Mgombea Urais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania kupitia CCM, Rais Jakaya Mrisho Kikwete akiwahutubia wananchi
katika kata ya Nyehunge jimbo la Buchosa,wilaya ya Sengerema mkoani Mwanza Juzi.
Mgombea urais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania kwa tiketi ya CCM, Jakaya Mrisho Kikwete, amemtambulisha Mwalimu wa Kimataifa wa Ujasiriamali, Eric James Shigongo kwamba ndiye mpigadebe mkuu wa chama hicho jimboni hapa.
Kikwete, alimtambulisha Shigongo jana kwenye mkutano wa hadhara wa kampeni jimboni hapa na kueleza kwamba ndiye atakayesimamia na kuongoza mpango mzima wa kumnadi Mgombea Ubunge wa Buchosa,Dk. Charles Tizeba.
Shigongo, alikuwa mmoja wa wana CCM, walioomba kuteuliwa kugombea ubunge Buchosa katika kura za maoni, lakini Halmashauri Kuu ya chama hicho (NEC), ilipitisha jina la Tizeba.
Katika hotuba yake jana, JK alimuelezea Shigongo kama kada mwaminifu wa CCM na kueleza kwamba alimuomba avunje kambi na kumuunga mkono Tizeba.
Huna haja ya kununa, mimi mwaka 1995 nilishindwa na mzee Mkapa (Rais Mstaafu), nikakubali matokeo baada ya miaka 10 nikashinda na kuwa Rais, alisema JK na kuongeza:
Namfahamu Shigongo kwa sababu kwanza ni mtani wangu, halafu pale Dar es Salaam ana kampuni yake ya magazeti, nadhani mnayajua.
JK aliendelea kusema:
Zaidi ya hayo yote Shigongo ni jirani yangu, ana shamba la mananasi kule Bagamoyo linapakana na la kwangu.
Aidha, JK alitania na kuifanya hadhira iangue kicheko:
Kipindi fulani alitaka kusogeza mpaka wa shamba lake na kuingia kwangu, nikamwambia huku usifike.
Baada ya kusema maneno hayo, JK alisema Shigongo ni safi na Tizeba ni safi na kusababisha umati uliohudhuria mkutano huo umshangilie kwa nguvu.
Duh nilishtuka sana kuona Jk eti anamtambulisha huyu jamaa maana najua alishidwa kumbe anamtambulisha kama mpiga kabobo aka debe wa Dr.Tizeba... Teh Teh, ila si bure huenda ameaahidiwa kitu huko mbeleni tusubiri tuone...
Nukuu in RED and bolded inashangaza kweli Rais waweza ongea maneneo haya???