JK amtaka CAG asilegee | JamiiForums | The Home of Great Thinkers

Dismiss Notice
You are browsing this site as a guest. It takes 2 minutes to CREATE AN ACCOUNT and less than 1 minute to LOGIN

JK amtaka CAG asilegee

Discussion in 'Habari na Hoja mchanganyiko' started by Babuu Rogger, Jan 18, 2012.

 1. B

  Babuu Rogger JF-Expert Member

  #1
  Jan 18, 2012
  Joined: Nov 16, 2011
  Messages: 970
  Likes Received: 302
  Trophy Points: 80

  OFISI ya Mdhibiti na Mkaguzi Mkuu wa Hesabu za Serikali imetakiwa kutokubali kuingiliwa na viongozi wa kisiasa ama wa kiserikali katika utendaji wao wa kazi, wakati wa kushughulikia watendaji wanaofanya ubadhirifu wa fedha na rasilimali za umma.
  Agizo hilo lilitolewa na Rais Jakaya Kikwete wakati wa hafla ya uzinduzi wa jengo la ofisi ya mdhibiti na Mkaguzi Mkuu wa Hesabu za Serikali Tawi la Mkoa wa Morogoro.
  Kikwete alisema kitendo cha kukubali kurubuniwa kwa namna yoyote na wanaofanya matumizi mabaya ya fedha za umma, kutarudisha nyuma jitihada za serikali katika kuboresha maisha ya Watanzania. SOURCE TANZANIA DAIMA.

  Sasa ndugu zangu toeni maoni yenu, hapa legelege ni CAG au MKUU WA KAYA? sababu mambo ya kifisadi ameshindwa kuyafanyia kazi mpaka leo hii, makarabrasha yanaozea kabatini na yupo anakunywa nao KAHAWA. nawasilisha.
   
 2. l

  luckman JF-Expert Member

  #2
  Jan 18, 2012
  Joined: Oct 11, 2010
  Messages: 1,202
  Likes Received: 174
  Trophy Points: 160
  alisema yeye hataingilia utendaji wa ofisi ya mkaguzi (si mdhibiti) ni mkaguzi, hataingilia, mambo yende ovyo yasiende ovyo yeye hataingilia kwani ofisi ipo kwa mujib wa katiba na akiingilia atakuwa anavunja katiba ya nchi, labda akisikia kelekele za wananchi ndo anaweza kufanya hivo ila hayuko tayari,

  my take, sina uhakika kama tanzania ya sasa watu wanaoteuliwa kugombea urais wanajua roles haswa za rais, na vilevile sijui hata yeye kama anajua ni maneno gani ya kutamka kwenye public na maneno yapi si ya kutamka, then siamini kama anaelewa maana ya kusimamia sheria aliyoapa kuilinda na ka kumwagiza mtu afanye yale anayotakiwa au kumhoji au kumuwajibisha unakuwa unavunja katiba, ifike mahala sisi watanzania tuwe na vigezo vya kitaifa vitakavyotumika kutuletea rais anayeserve purpose ya urais na si rais jina.
   
Loading...