JK amegewa mbinu za maendeleo Malaysia!!! | JamiiForums | The Home of Great Thinkers

Dismiss Notice
You are browsing this site as a guest. It takes 2 minutes to CREATE AN ACCOUNT and less than 1 minute to LOGIN

JK amegewa mbinu za maendeleo Malaysia!!!

Discussion in 'Jukwaa la Siasa' started by Mr. Zero, Jun 21, 2011.

 1. Mr. Zero

  Mr. Zero JF-Expert Member

  #1
  Jun 21, 2011
  Joined: Jun 5, 2007
  Messages: 9,499
  Likes Received: 2,743
  Trophy Points: 280
  [TABLE="class: contentpaneopen"]
  [TR]
  [TD="class: contentheading, width: 100%"]JK amegewa mbinu za maendeleo Malaysia [/TD]
  [TD="class: buttonheading, width: 100%, align: right"] Send to a friend [/TD]
  [/TR]
  [/TABLE]
  [TABLE="class: contentpaneopen"]
  [TR]
  [TD="class: createdate"]Monday, 20 June 2011 20:48 [/TD]
  [/TR]
  [TR]
  [TD]0diggsdigg

  Mwandishi Wetu
  RAIS Jakaya Kikwete jana alikuwa miongoni mwa Wakuu wa Serikali za Nchi za Afrika waliopewa mada maalumu kuhusu Muundo Mpya wa Maendeleo wa Malaysia (New Economic Model for Malaysia) programu zake za utekelezaji.

  Taarifa iliyotolewa na Kurugenzi wa Mawasiliano ya Rais jana ilieleza kuwa mpango huo unalenga kuivusha nchi hiyo ya Kusini Mashariki mwa Asia kutoka kwenye hadhi yake ya sasa ya kuwa nchi yenye uchumi wa kati na kuwa nchi tajiri ambayo watu wake wana pato ya dola 15,000 na zaidi kwa mwaka.

  Mada hiyo maalumu kwa viongozi hao wa Afrika ilitolewa na Dk Dato’ Sri Idris Jala, Waziri katika Ofisi ya Waziri Mkuu wa Malaysia, katika shughuli maalumu kwa viongozi hao iliyofanyika ofisini kwa Waziri Mkuu huyo katika mji mpya wa Serikali ya Malaysia wa Patrajala, nje ya mji mkuu wa nchi hiyo wa Kuala Lumpur.

  Dk Jala aliwaeleza viongozi hao wa Afrika ambao walikuwa ni pamoja na Rais wa Zimbabwe, Robert Mugabe na Waziri Mkuu wa Lesotho, Pakalitha Mosisili katika hatua zote muhimu ambazo nchi hiyo imepitia kuweza kufikia kwenye muundo huo.

  Dk Jala pia alimwambia viongozi hao kuhusu jinsi wananchi wa Malaysia walivyoshirikishwa katika maandalizi ya muundo huo ambao unalenga kuifanya Malaysia nchi ya dunia ya kwanza katika miaka 10 ijayo, yaani 2020.

  Alisema kuwa baada ya muundo na programu zake kuwa vimebuniwa, wadau mbalimbali kiasi cha watu 500 walikusanywa na kuwekwa katika chumba kimoja ili kujadili programu za utekelezaji wa mpango huo na baada ya hapo uliwasilishwa kwa wananchi katika mikutano ya hadhara ili kuwajulisha wananchi kuhusu muundo huo na kutaka maoni yao. Baada ya hapo, muundo huo na programu zake vilichapishwa katika machapisho.

  Dk Jala aliwapitisha viongozi hao katika vipengele muhimu vya muundo huo na progamu zake za utekelezaji ambazo ni pamoja na Programu ya Mageuzi ya Uchumi (ETP) na Programu ya Mageuzi ya Serikali (GTP).

  Kaulimbiu kuu ya muundo huo mpya wa maendeleo katika Malaysia ni Big Results Fast, yaani Mipango Mikubwa ya Kuleta Matokeo Haraka.

  Muundo huo na programu zake vitawagharimu wananchi wa Malaysia kwa maana ya Serikali, sekta ya umma na sekta binafsi kiasi cha RM 444 bilioni (fedha za Malaysia) na mipango 131 itakatekelezwa kwa lengo la kubadilisha wananchi wa Malaysia na kuwafanya matajiri.

  Dk alisema wananchi katika mikutano yao na viongozi walioandaa muundo huo, wananchi walisema kuwa walikuwa na wasiwasi kuhusu kuongeza kwa hali ya uhalifu, hali isiyoridhisha ya usafiri wa umma, hali ya elimu, miundombinu ya msingi ya maeneo ya vijijini na hali ya rushwa.

  Wakati wa mada hiyo, Rais Kikwete alitaka kujua ni hatua zipi hasa Malaysia ilichukua ili kuondokana na umaskini mkubwa uliokuwa unawakabili wananchi wa nchi hiyo iliyopata uhuru mwaka 1957, sawa na Ghana, kutoka kwa Waingereza.

  Dk Jala alisema kuwa pamoja na kwamba Malaysia imepiga hatua bado inayo matabaka matatu yaani ya kundi la watu walioendelea, kundi la watu wa kati na kundi la maskini, hasa katika maeneo ya vijijini.

  Hata hivyo, alishauri kuwa muhimu ni kwa Tanzania kuamua maeneo gani muhimu ya uchumi yanayoweza kubadilisha haraka maisha ya Watanzania na kuelekeza nguvu kwenye maeneo hayo.

  Kwa ushauri, alitaka maeneo la msingi kwa maendeleo ya haraka kuwa ni miundombinu na hasa barabara, elimu na hatua nyingine zinazoweza kuboresha kwa haraka maisha ya watu wa kipato cha chini.

  Viongozi hao wa Afrika wako mjini Kuala Lumpur kuhudhuria mkutano wa mwaka huu wa Ushirikiano wa Kimkakati baina ya nchi zinazoendelea wa Langkawi International Dialogue 2011 unaofanyika kwenye Kituo cha Mikutano ya Kimataifa cha Putrajaya (PICC).

  Add this page to your favorite Social Bookmarking websites
  [​IMG] [​IMG] [​IMG] [​IMG] [​IMG] [​IMG] [​IMG] [​IMG] [​IMG] [​IMG]
  [/TD]
  [/TR]
  [/TABLE]
  [h=4]Comments [/h]


  0 #12 jumbe 2011-06-21 14:00 MNAOTOA MAONI WENGI WENU MNA CHUKI NA RAIS WETU VILE NI KIPENDO CHA WANANCHI SIJAONA SIKU MOJA MKIMSIFIA- NGOJENI MWAKA 2015 AJE RAIS MKRISTO NAFIKIRI HAKUNA ATAKAYETHUBUTU KUMSEMA - SI MNAKUMBUKA MKAPA ALIPOMNYANG'ANYA PASSPORT MPENDWA WETU ALI HASSAN MWINYI ??
  Quote


  0 #11 Michael Zunzu 2011-06-21 11:28 Wandishi wa habari wakati mwingini huwa mnakosea vichwa vya habari, ni mbinu zipi asizozifahamu Kikwete namna ya kuleta maendeleo ya nchi ambazo hazifahamu? N mbinu zipi hajazisikia, je Kwete hajawahi kwenda Malaysia na kukutana na viongozi wa nchi hiyo na kujionea walicho fanya?
  Serikali inawataalamu wa kila aina na waliofuzu, ni viongozi kukosa dhamira na kuridhika na hali iliyopo kwa vile wao wako pema hapo walipo, asiyekuwa nacho kwao sicho kinachowakera mioyoni mwao.
  Quote


  0 #10 Gabriel 2011-06-21 10:23 Kikwete na Pinda kwa kauli zao wenyewe hawajui kwa nini Tanzania ni maskini. Karibu kila mtanzania wa umri wa kufikiri anajua kinachotuasibu lakini hawa wawili la hasha. Kwa kuuliza swali hilo kikwete alitegemea apewe magic wand itakayomwezesha kusema akrakadabra na voila umaskini wetu unayeyuka. Wataalamu tunao, ardhi tunayo, siasa mbovu na uongozi mbovu vinatuponza.
  Quote


  0 #9 Pj 2011-06-21 10:17 Asome ripot.......!!!!!!halafu safari amuachie nani???????wewe bwana weweeeee....alishasema tutakufa njaaaa akikaaa hapa.....UMESAHAU????
  Quoting mandope1:
  Kwa maoni yangu ni kwamba rais hakuhitajika kuuliza swali hilo. Raisi aliyetangulia Mr. Mkapa alimwajiri kwa mkataba Prof. mmoja toka malaysia na akainisha mambo mengi ya kufanya ili kuondokana na umasikini hapa kwetu. Ni juu yake kusoma ripoti ile na ripoti nyingi ambazo zimeandaliwa na watanzania. Azifanyie kazi.​
  Quoting nelson:
  KWA RAISI WETU NINAVYOMJUA ALIVYO NA MAMBO MENGI ANAWEZA KUSAHAU,NINGEPE NDEKEZA YEYE ASINGEENDA BADALA YAKE ANAGEWAAGIZA MAKATIBU WAKUU NA WAKURUGENZI .HILI SOMO LIMEFUNDISHWA NA LINAACHWA KWENYE NDEGE SIKU YA KURUDI​
  halafu posho amuachie nan????
  Quote


  0 #8 Pj 2011-06-21 10:09 Another POSHO DEAL,we acha tuuu
  Quoting Anonymous:
  Amualike Huyo Waziri Mkuu kutembelea Tanzania ili aje atoe darasa kwa viongozi wetu (Mawaziri, Makatibu wakuu, wakurugenzi .n.k)​
  Quote


  +1 #7 mandope1 2011-06-21 10:08 Kwa maoni yangu ni kwamba rais hakuhitajika kuuliza swali hilo. Raisi aliyetangulia Mr. Mkapa alimwajiri kwa mkataba Prof. mmoja toka malaysia na akainisha mambo mengi ya kufanya ili kuondokana na umasikini hapa kwetu. Ni juu yake kusoma ripoti ile na ripoti nyingi ambazo zimeandaliwa na watanzania. Azifanyie kazi.
  Quote


  +1 #6 Pj 2011-06-21 10:06 Ajabu ni kwamba FYDP.....imezinduliwa pale dodoma then mkuu wa kaya akawashukuru wabunge kabla bunge halijapitisha,, ,,,,,,,hata afundishweje hawez kutuvusha.....
  Quote


  0 #5 Anonymous 2011-06-21 08:28 Amualike Huyo Waziri Mkuu kutembelea Tanzania ili aje atoe darasa kwa viongozi wetu (Mawaziri, Makatibu wakuu, wakurugenzi .n.k)
  Quote


  +2 #4 ahmed00 2011-06-21 08:14 Aambiliki huyo JK, tunao wataalam wengi na wazuri sana wazawa lakini JK na serikali yake hawapendi kukosolewa.
  Mfano mdogo: Suala la Posho
  Quote


  +4 #3 Bakari 2011-06-21 07:31 Mkutano ulifaa kuhudhuliwa na maofisa wa TUME YA MIPANGO... lakini Rais hataki kuhachia per-diem!

  Ukweli ni kwamba hata kama tungeudhulia mikutano mingapi, kama uongozi wa juu hauna NIA ya dhati ya kuondosha umasikini, itakuwa kazi bure. Bajeti ya juzi ina VIPAUMBELE kibao, lini tutajifunza toka kwa wenzetu? Au JK akirudi atamwambia Mkullo apunguze vipaumbele?
  Quote


  +4 #2 nelson 2011-06-21 06:08 KWA RAISI WETU NINAVYOMJUA ALIVYO NA MAMBO MENGI ANAWEZA KUSAHAU,NINGEPE NDEKEZA YEYE ASINGEENDA BADALA YAKE ANAGEWAAGIZA MAKATIBU WAKUU NA WAKURUGENZI .HILI SOMO LIMEFUNDISHWA NA LINAACHWA KWENYE NDEGE SIKU YA KURUDI
  Quote


  0 #1 Mchangiaji 2011-06-21 04:00 Haya mheshimiwa Rais nadhani umejionea mwenyewe nchi amabayo ilikuwa na shida ya chakula miaka ya nyuma na Tanzania tukawasaidia. Sisi bado tunasuwa suwa na hali ngumu ya maisha, nadhani ni wakati muafaka kukubali kushirikiana na nchi kama Malaysia ambayo ilikuwa kama sisi mwanzo na wamebadilika sasa.
   
 2. Kinyungu

  Kinyungu JF-Expert Member

  #2
  Jun 21, 2011
  Joined: Apr 6, 2008
  Messages: 4,380
  Likes Received: 3,339
  Trophy Points: 280
  Hata kama angekuja Malaika Mkuu Gabriel JK hafundishiki na wala hana maono ya kuikwamua hii nchi kiuchumi.
   
 3. Trustme

  Trustme JF-Expert Member

  #3
  Jun 21, 2011
  Joined: Jan 7, 2011
  Messages: 1,172
  Likes Received: 9
  Trophy Points: 0
  Kwani kuna mtu asiyejua kwamba hakuna kiongozi yeyote aliyoko madarakani kwa sasa anampango wa kuindeleza Tz! Tumejionea wenyewe ccm inachokiita mpango wa maendeleo wa Taifa! Eti kwa mwaka mpango ili utekelezwe unahitaji Tshs 8 trilioni, halafu unautengea tshs 2.6 trilioni, huo ndo utekelezaji au wanataka kutuibia pesa zetu? Yan ni wazi kwamba huo mpango hautekelezeki, na hiyo 2.6 trilioni itaishia hewani. SASA MIMI NILITAKA KUJUA HUO MPANGO MPYA WA MAENDELEO WA MALAYSIA AMBAO UTAGHARIMU RM 444 BILIONI KWA MIAKA 10, YAN KWA MWAKA WATATENGA 44.4 BILIONI, SASA WAMETENGA SHILING NGAPI KWA MWAKA? NI ASILIMIA 35% KAMA JK ALIVYOFANYA? SASA HICHO NDO ANATAKIWA KUJIFUNZA NA ASIMAMIE UTEKELEZAJI WAKE
   
 4. Ronal Reagan

  Ronal Reagan JF-Expert Member

  #4
  Jun 21, 2011
  Joined: Nov 4, 2010
  Messages: 4,739
  Likes Received: 1,453
  Trophy Points: 280
  Zero return. Hamna kitu hapo!
   
Loading...