JK alitoa nafasi adhimu sana ya kupata Katiba mpya lakini tukaipoteza, itatuchukua miaka mingine zaidi ya 50 kuipata Katiba mpya!

Mkuu, hata angekuja nani bado Watanzania ni Vichwa Maji. Inaweza ikawa laana ya Uweusi huu nao! Sikupenda Kuzaliwa Mweusi, Sikutaka niwe sehemu ya laana hii!
Mkuu kwa hiyo na wewe ni kichwa maji? Mimi simo! Ila kuna vichwa maji hasa wapiga kura na viongozi wanaowachagua kutuwakilisha!
 
Bora tungeondoka na ile pamoja na mapungufu yake halafu tukajipanga thereafter mana ilikua na mambo mazuri sana.
Kwasasa ni ngumu sana
 
Aliyeianzisha katiba ndo aliyeiharibu japo aliita watu kumshauri hakutekeleza makubaliano. Tusimlaumu mtu ila yeye hakuwa na nia ya dhati ktk hili. Aliogopa alipoambiwa chama kitashindwa vibaya.

Mkuu ww umesema ukweli. Huyo JK alikubali katiba mpya baada ya kuzidiwa hoja na Dr. Slaa kwani ujengaji hoja wa Dr ulizaa hamasa. JK akawa hana jinsi ikabidi aikubali hoja ile shingo upande ili kushusha shinikizo la hamasa ile. Lakini kiukweli hakutaka katiba mpya na kwa bahati mbaya hakuwa na ushawishi wala uwezo wa kuwalazimisha wanaccm wenzake waikubali katiba ile. Matokeo yake ndio rasimu ya Warioba kukutana na mizengwe na JK akajiunga na wanaccm wenzake kuhujumu maoni halisi ya wananchi.

Sasa hivi kuna namna fulani ya kumpaka JK mafuta kwa mgongo wa chupa hapa nchini eti kuonyesha alikuwa mzuri. Ni hivi tuwe wakweli tu, JK hakuwa mzuri wa hivyo bali kwakuwa kipimo chake ni Magufuli basi anaonekana mzuri. Kama kipimo cha ubora wa JK katika demokrasia ni Magufuli basi JK ni bora, lakini kama kipimo chao ni demokrasia basi wote wawili wana maksi za chini. Sana sana kilichomfanya JK atekeleze demokrasia kwa kiwango fulani ni kwakuwa alipenda kusafiri hivyo alikutana na shinikizo la jumuiya ya kimataifa kuhusu demokrasia na wangalau alikuwa na soni. Magufuli yeye anahujumu demokrasia waziwazi kwani hawezi ushindani, hana hoja zenye mvuto, hasafiri kwenda nje hivyo shinikizo kuhusu tabia yake kwenye demokrasia inakuwa ndogo.
 
Miongoni ya maono mazuri sana aliyokuwa nayo Rais wa awamu ya 4, Jakaya Kikwete, ni kuanzisha mchakato wa Katiba mpya, ambapo aliunda Tume ya Warioba, ambayo ilikusanya maoni ya watanzania na baadaye kuyafikisha maoni hayo kwenye Bunge la Katiba, ambalo wabunge wake wengi ni wa CCM

Matokeo ya Bunge lile, kila mtu anayakumbuka ni kwa wale wabunge wa CCM kuamua kuitupa kwenye "dustbin" ile Rasimu nzuri ya Katiba ya Tume ya Warioba na badala yake kutaka kutuletea Katiba pendekezwa ya "Lumumba" ambayo matokeo yake ni kuwa Katiba hiyo pendekezwa nayo "ilibuma"

Matokeo ya "blunder" ile kubwa ndiyo haya tunayoyaona, kwa kila kukicha tunatangaziwa toka Jumba kubwa ya kuteua na kutumbua.......

Tukumbuke pia miongoni ya mambo mazuri sana yaliyokuwemo kwenye ile Rasimu ya Tume ya Warioba ni kumpunguzia madaraka makubwa mno ambayo Rais amepewa kwenye hii Katiba ya sasa

Likiwemo hilo la kuteua na kutengua kuwa ni kazi ya mtu mmoja tu ambaye ni Rais

Matokeo yake ni uteuzi wa "vituko" wa DC wa Kisarawe na DC wa Arumeru!

Kwa hiyo kwa sasa tunaisoma namba sote wale wa upinzani na wale wa CCM!

Ee Mungu tunakuomba ulimulike Taifa hili ulilolijaalia sana amani ambayo sasa ni kama iko ukingoni kabisa kutoweka
JK kama angekuwa ni mwanasiasa mzuri angeruhusu demokrasia ya ukweli katika kupata mgombea urais kupitia chama cha CCM 2015 badala ya kuja na majina ya mfukoni.
 
Hebu jaribu kuimagine hivi kama JK angekuwa hana nia safi na Katiba mpya angewateua wale wajumbe kwenye Tume ya Warioba??

Tena Tume iliyotumia zaidi ya shilingi bilioni 40 za walipa kodi wa nchi hii??

Bado ninaamini kuwa yule Mzee wetu alikuwa na nia safi, isipokuwa wahafidhina ndani ya Chama chake ndiyo "waliomtisha" hadi akawa mdogo kama "pilitoni"
Mtu mwenye determination na kujua umhimu wa hicho unakifanya huwezi kutishwa na watu wenye njaa...hata wakati wa kuanzishwa kwa vyama vingi wengi walitaka kibaki kimoja, lakini viongozi mahiri waliona mbali wakasema hapana lazima, dunia inabadilika tuwasikilize hawa wachache ili kipanua wigo wa demokrasia
 
Back
Top Bottom