JK alitoa nafasi adhimu sana ya kupata Katiba mpya lakini tukaipoteza, itatuchukua miaka mingine zaidi ya 50 kuipata Katiba mpya!

Watanzania acheni unafiki, hivi unakumbuka hotuba ya kikwete bungeni kwenye ufunguzi wa Bunge la Katiba???

Pale Mzee ndio alimaliza kila kitu. Raisi yule ndio alivuruga mchakato wa katiba. Ingia hata Youtube uone ile hotuba yake ndio utaelewa kwanini sisi watanzania ni wanafiki wa kuogopa duniani.
Wewe mwenyewe unajua kuwa wahafidhina ndiyo Waloharibu mchakato wa Katiba.....

Ila yeye mwenyewe kama JK alikuwa na moyo safi ya upatikanaji wa Katiba hiyo

Siyo kama Huyu Jiwe anatamka wazi kuwa Karibu mpya siyo kipaumbele chake!

Yeye kama yeye Jiwe,hataki upatikanaji wa Katiba mpya, lakini ni matakwa ya watanzania zaidi ya milioni 50 wanaotaka Katiba mpya

Kwa hiyo hawezi kilupingana na matakwa ya wananchi waliomweka madarakani
 
Last edited:
Tena ni nafasi adhimu sana tena Sanaa.....

Ambayo watanzania tutaijutia sana kuipoteza
Kikwete ndiyo chanzo hasa cha kushindwa kupatikana kwa katiba mpya! Hakuwa na utashi wa kuleta katiba mpya bali alikuwa na nia ya kuongezea viraka kwenye katiba ya sasa. Ni vizuri sana ilishindikana kwani ingetuweka mahali pabaya zaidi. Haya ya kuanzisha ''kiwanda'' huko Kisarawe ni kilele cha uzembe lakini mimi nadhani ni tanuru zuri la kupika watanzania na kuwaamsha kwenye usingizi wa pono waliolala. Kila kiti kina mwisho na kiwanda kilichoanzishwa huko Kisarawe kitawafungua hata wale ma-CCM waliokuwa wamelala na kuwafanya wagundue kumbe wasipokuwa makini wakaja na katiba mpya na nzuri tunaelekea kubaya!
 
Kikwete hakuwa na nia ya kuleta Katiba mpya, ilikua ni kiini macho. Aliuanzisha yeye, akauvuruga yeye. Mchakato ulianzishwa kinafiki.
Alikuwa nayo nia, isipokuwa aliharibiwa na wahafidhina ndani ya Chama chake cha CCM ambao wanaamini kuwa Tanzania ni mali yao binafsi.......
 
Kikwete ndiyo chanzo hasa cha kushindwa kupatikana kwa katiba mpya! Hakuwa na utashi wa kuleta katiba mpya bali alikuwa na nia ya kuongezea viraka kwenye katiba ya sasa. Ni vizuri sana ilishindikana kwani ingetuweka mahali pabaya zaidi. Haya ya kuanzisha ''kiwanda'' huko Kisarawe ni kilele cha uzembe lakini mimi nadhani ni tanuru zuri la kupika watanzania na kuwaamsha kwenye usingizi wa pono waliolala. Kila kiti kina mwisho na kiwanda kilichoanzishwa huko Kisarawe kitawafungua hata wale ma-CCM waliokuwa wamelala na kuwafanya wagundue kumbe wasipokuwa makini wakaja na katiba mpya na nzuri tunaelekea kubaya!
Kama angekuwa hana nia asingeanzisha mchakato ule ambao ulikula mabilioni ya pesa za walipa kodi..........

Mimi naendelea kusisitiza kuwa wahafidhina ndani ya CCM ndiyo waliomuharibia JK na kutopatikana kwa Katiba mpya
 
Watanzania sisi ni wanafiki sana. Sisi ni manyumbu na itatuchukua muda kujielewa.

Sometimes huwa nashukuru ujio wa Magufuli ili Kutuyeyusha na akili ziturudie na tuwe imara.

Kwa mtu aliekuwa akifuatilia mchakato mzima wa katiba mpya. Kuharibka kwa mchakato kulianza baada ya hotuba ya Kikwete Bungeni. Kwa mdomo wake nakumbuka alisema hapendi serikali tatu ambazo kwa mujibu wa maoni yale ilikuwa ni mapendekezo ya Wananchi.

Ftom there tukashuhudia vioja bungeni.

Leo anajitokeza mtu anajifanya hatukuwepo kwenye mchakato.

Poor TanZanians
Mkuu, hata angekuja nani bado Watanzania ni Vichwa Maji. Inaweza ikawa laana ya Uweusi huu nao! Sikupenda Kuzaliwa Mweusi, Sikutaka niwe sehemu ya laana hii!
 
Kikwete ndiyo chanzo hasa cha kushindwa kupatikana kwa katiba mpya! Hakuwa na utashi wa kuleta katiba mpya bali alikuwa na nia ya kuongezea viraka kwenye katiba ya sasa. Ni vizuri sana ilishindikana kwani ingetuweka mahali pabaya zaidi. Haya ya kuanzisha ''kiwanda'' huko Kisarawe ni kilele cha uzembe lakini mimi nadhani ni tanuru zuri la kupika watanzania na kuwaamsha kwenye usingizi wa pono waliolala. Kila kiti kina mwisho na kiwanda kilichoanzishwa huko Kisarawe kitawafungua hata wale ma-CCM waliokuwa wamelala na kuwafanya wagundue kumbe wasipokuwa makini wakaja na katiba mpya na nzuri tunaelekea kubaya!
Umewahi ona wapi a proved Maiti ikaamkaa?
 
Hivi kwa mfano alipoteua kile "kiwanda chake" kule Kisarawe, na hakuna mtu mwenye ubavu wa kuhoji uteuzi huo!
 
Mtu wa pwani alitutia hasara huwezi anzisha jambo kubwa kama hilo usilimalize. Wakulaumiwa ni jk si magufuli. Mkwele alinikela watu walilipana posho kubwa sana kwa jambo lisilo fanikiwa
 
Watanzania acheni unafiki, hivi unakumbuka hotuba ya kikwete bungeni kwenye ufunguzi wa Bunge la Katiba???

Pale Mzee ndio alimaliza kila kitu. Raisi yule ndio alivuruga mchakato wa katiba. Ingia hata Youtube uone ile hotuba yake ndio utaelewa kwanini sisi watanzania ni wanafiki wa kuogopa duniani.
Naikumbuka. Nilikuwa naisikiliza nikiwa nasafiri, Niliboeka sana kwa kweli
 
Katiba mpya ilikuwa danganya toto muulizeni Polepole leo na mzee Warioba kama bado wana hamu na katiba mpya
 
Mtu wa pwani alitutia hasara huwezi anzisha jambo kubwa kama hilo usilimalize. Wakulaumiwa ni jk si magufuli. Mkwele alinikela watu walilipana posho kubwa sana kwa jambo lisilo fanikiwa
Kwa taarifa yako ni kuwa ule mchakato wa Katiba mpya uligharimu pesa ya walipa kodi zaidi ya shilingi bilioni 40!

Maana yake ni kuwa pesa yote hiyo ni kama tumeitosa kwenye shimo la choo!
 
Sio katiba tu kuja kupata tolerant and sympathetic leader kama JK, itachukua ka mda kidogo such leaders appears once after 50yrs.....ntakupa mfano huyu Jk alikua nauwezo wakumwambia Mh Mbatia ahame chama ili ampe ubunge wa kuteuliwa, ila cha hajabu alimpa akiwa bado kwenye chama chake chakipinzani.

Huu ndiyo unafiki unaosemwa…..si ni Kikwete huyu huyu ambao watu walisema ni dhaifu na hatufai? Kikwete hakutaka chochote juu ya ile katiba ilikuwa ni usanii tu.
 
mnyonge mnyongeni ila haki yake apewe jk kwangu alikuwa nyerere wa pili sijui kama tutakuja kupata baba wa namna ile
Jk alikua nyerere kwa kwangu,..... kwasababu utawala wa wayerere sikuushuhudia, hakuwa na wapizani, elites kipindi chake walikua 0.9%. Nchi ulikua na umoja kwasabab ya vugu vugu za uhuru, alitawala miaka 25 mda wakutosha kujiimalisha, watu walikua masikini sana, kajipanga ....kwa JK hayo yote yalikua kinyume chake, lakini watu walizidi kumpenda watu walipata neema za uchumi Diplomasia liliongezeka Tz ikapendwa na kuheshimika na nchi zingine.
 
Kikwete alikuwa na nia njema, aliacha Demokrasia na Sheria iliyianzisha mchakato vichukue mkondo wake katika suala hilo, hakutaka kulazimisha mambo. Wahafidhina wa CCM wakauteka mchakato and the rest is history.

Hata Hivyo Rasimu ya Warioba haikuwa Alfa na Omega, Sheria iliyoanzisha mchakato ilitaka bunge la katiba liiboreshe Rasimu. Na Mchakato kimsingi upo Inahitajika Kura za maoni tu Twende na Rasimu ya Chenge
 
Mnamsema JK lakini hamuwaoni Wajumbe wa Rasimu yenyewe akina Kabudi na Polepole ambao leo wanasema katiba mpya si kipaumbele, wakati ni wao waliokuwa mbele kuifanya hiyo kazi!.

Pili kama Watanzania walikuwa wanaipenda sana Rasimu yao ya Warioba kwa nini Waliipigia Kura CCM iliyovuruga mchakato na kuirudisha madarakani mwaka 2015?

JK as JK si tatizo ni waTZ
 
Back
Top Bottom