JK Akwepa kuzindua Ukarabati CRDB Shinyanga | JamiiForums | The Home of Great Thinkers

Dismiss Notice
You are browsing this site as a guest. It takes 2 minutes to CREATE AN ACCOUNT and less than 1 minute to LOGIN

JK Akwepa kuzindua Ukarabati CRDB Shinyanga

Discussion in 'Habari na Hoja mchanganyiko' started by Mgoyangi, Jan 20, 2010.

 1. Mgoyangi

  Mgoyangi Senior Member

  #1
  Jan 20, 2010
  Joined: Feb 6, 2008
  Messages: 184
  Likes Received: 3
  Trophy Points: 35
  Kuna habari hivi sasa kuwa JK amegoma kufungua jengo la CRDB shinyanga lililokarabatiwa na nyeti zinasema kuwa kuna ubadhirifu wa hisa za wananchama -- ambazo zimechotwa kinamna na -- kutokana na skandali hiyo kiasi kama zaidi ya milioni 200 zimeishia mikononi mwa wajanja wachacha na tayari afisa Ushirika mmoja yupo mbaroni.

  JK yupo katika ziara mkoani Shinyanga ambapo leo anazindua shule ya msingi ya Masengwa wilaya ya Shinyanga ambayo ilianza kujengwa na wapinzani -- lakini baadaye ikatekwa na Buzwagi na makada wengine kuhakikisha kuwa inakamilika.

  Kesho anazindua Savannah Plains Int Schoo ya mjumbe wa NEC Hamad Hilal ambayo nimeona walimu wazungu tupu na mtanzania mmoja tu
   
 2. Msanii

  Msanii JF-Expert Member

  #2
  Jan 20, 2010
  Joined: Jul 4, 2007
  Messages: 6,427
  Likes Received: 370
  Trophy Points: 180
  hehehehehe
  only in tanzania.

  Hiyo ya kufungua shule ambayo walimu wake ni wazungu watupu huku mmoja akiwa ni Mtz anatupa mtazamo gani?? asije akasema kwamba walimu wa bongo hawaajiriki na wawekezaji huria kwa kuwa ni wezi!!! lol

  Lakini kwa nini rais hakai ikulu na kutulia?? je hawaamini wasaidizi wake? au anakasimu madaraka kwa watu ambao anadhani wanamsaidia?? maana kila baada ya kitambo kidogo utasikia rais yupo mkoa au nchi fulani. au anataka kuvunja rekodi ya safari???
   
 3. Mchaga

  Mchaga JF-Expert Member

  #3
  Jan 20, 2010
  Joined: Apr 11, 2008
  Messages: 1,371
  Likes Received: 10
  Trophy Points: 135
  safi sana JK ila hiyo ya walimu wazungu na mtanzania mmoja tu nadhani si tatizo maana ndio mambo ya soko huru hayo.
   
 4. Masaki

  Masaki JF-Expert Member

  #4
  Jan 20, 2010
  Joined: Mar 7, 2006
  Messages: 3,465
  Likes Received: 163
  Trophy Points: 160
  Hiyo Savannah Plains International School iko njiani ukiwa unatoka Shinyanga kwenda Mwanza. Ni shule kubwa na ya kisasa sana! Mwekezaji wake anawatarget wazungu wanaokuja kufanya kazi katika migodi iliyoko kanda ya Ziwa. Ila kwa uzoefu wangu, wengi wao huwa hawaji na watoto wao. Anyway, its an investment.
   
 5. Mgoyangi

  Mgoyangi Senior Member

  #5
  Jan 20, 2010
  Joined: Feb 6, 2008
  Messages: 184
  Likes Received: 3
  Trophy Points: 35
  Hivi hali ya shule kama savannah Int school hapa tanzania ikoje? zipo ngapi na umiliki wake ukoje na zinafuata syllabus gani?

  Maana kuna fikra mbadala kwam,ba nyingi ni za wazungu ambao wanawatumia wabongo kama vibaraka?

  Mwenye nondo atushushie tafadhali?
   
 6. PakaJimmy

  PakaJimmy JF-Expert Member

  #6
  Jan 20, 2010
  Joined: Apr 29, 2009
  Messages: 16,236
  Likes Received: 309
  Trophy Points: 180
  Aangalie hizi zinduzi-zinduzi zake.!

  Wajanja wasije wakamshikisha mapembe kama ilivyofanyika Arusha kwenye hoteli ya snow-crest, ambako alizindua hoteli na jioni yake ikabomolewa na manispaa!

  Maana washauri wa huyu bwana ni bogus wooote!
   
 7. StaffordKibona

  StaffordKibona JF-Expert Member

  #7
  Jan 20, 2010
  Joined: Apr 21, 2008
  Messages: 671
  Likes Received: 5
  Trophy Points: 0
  Kwani ada yake ni Shs ngapi au dollar ngapi nijaribu kumpeleka mmoja wa vitegemezi vyangu?
   
Loading...