Jk akiomba atutawale kipindi kingine cha 3

Hercule Poirot

JF-Expert Member
Mar 14, 2011
1,717
1,472
Wakuu hivi mmewahi kufikiria au imewahi kukupitia ktk mawazo yako ikiwa Rais wetu Mheshimiwa sana Dk. Jakaya M. Kikwete akaomba kugombea tena Urais 2015 kwa mwanya/kisingizio cha kuwapo KATIBA MPYA (Kama ikiwa ishapita kabla ya 2015 - ujanja huo anaufanya sasa Abdoulaye Wade wa Senegal)....
Wewe kama mwana JF na Mtz ikiwa itatokea hivyo (UWEZEKANO HUO UPO, SIJAWAHI KUMSIKIA MKULU KUZUNGUMZIA KUNGATUKA KIKATIBA 2015) una m,aoni gani? Na utachukua hatua gani ? Ni mawazo tu wajameni..
 
Mleta uzi anajua kabisa hiki ni kitu ambacho hakiwezekani ila kaona alete umbea tu!
 
Usi jaribu kuwapa wananchi waliokuwa hoi dhana mbaya kama hizo.

Kiama kinweza kikaja haraka zaidi. Sababu hafai, hafai, hafai na hafai kabisa.

Mkuu doctore sio dhana mbaya mkuu haya mambo mbona ya kawaida kwa waafrika..angalia kinachotokea Swenegal.....UWEZEKANO HUO UPO HATA HAPA TZ...WAPAMBE WAKE JK WANAWEZA LIUNDIA HOJA HILI KWA KISINGIZIO CHA KATIBA MPYA MFUMO MPYA //hivyo yeye kutokufungwa na katiba ya zamani inayomzuia kugombea baada ya vipindi v2 vya urais
 
huyuhuyu mbayuwayu au mwingine? Huyu hapana,waosemwa wapole wabongo watakua kama paka vichaa!!
 
Mleta uzi anajua kabisa hiki ni kitu ambacho hakiwezekani ila kaona alete umbea tu!
MMBEYA SHANGAZI YAKO KABLA SIJASAHAU..........hivi uko dunia yangapi kengemaji wewe..huoni au hujasikia vituko vya RAIS WADE wa Senegal anayegombea kwa mara ya 3 kwa kisingizio cha katiba mpya......tupe maoni yako kuwa utafanyeje ikitokea hali kama hiyo...

Mimi najaribu kuwazindua tu kuhusu uwezekano wa kitu kama hicho kutokea hapa TZ
 
katiba hairuhusu...period.

Unaleta dhihaka za ushindani wa chadema na CCM huna hoja hapa.

aseme anang'atuka wakati katiba iko wazi? katiba imeweka kikomo kwa nini aseme anang'atuka?

Nani kasema katiba mpya itakuwa na vipindi vitatu? JK kasema katiba mpya itakuwa tayari April 26, 2014 siku ya kuadhimisha miaka 50 ya Muungano wa Tanzania. hapo ni mwaka mmoja kabla ya uchaguzi muda wa kuongeza kutawala utatoka wapi
 
huyuhuyu mbayuwayu au mwingine? Huyu hapana,waosemwa wapole wabongo watakua kama paka vichaa!!

kumbuka mkuu zaidi ya nusu ya wa tz hawakupiga kura mwaka 2010....mtu waweza sema watu hao hawana mwamko wa siasa na uchaguzi hapa bongo nini kitakachomzuia Mkulu kutuburuza kwa kipindi kingine? au wataka sema sasa watu wameaamka na hawampendi vasco wetu
 
Nampenda sana kikwete, hata akiwa Rais mara 10 yaani awe tu, niko radhi kabisa. usiniulize kafanya jambo gani jema ktk nchi hii sitakuambia hata moja, ingawa simaanishi kuwa hakufanya mazuri ktk utawala wake, wala simchukii kwa7bu ya mabaya yake, hapa pia simaanishi kwamba hana mabaya ktk uongozi wake! pengine 7bu za kumchukia zipo lakini me simchukii bali nampenda jamani huyu mtu pasi na 7bu, yaani nampenda tu....!!
 
MMBEYA SHANGAZI YAKO KABLA SIJASAHAU..........hivi uko dunia yangapi kengemaji wewe..huoni au hujasikia vituko vya RAIS WADE wa Senegal anayegombea kwa mara ya 3 kwa kisingizio cha katiba mpya......tupe maoni yako kuwa utafanyeje ikitokea hali kama hiyo...

Mimi najaribu kuwazindua tu kuhusu uwezekano wa kitu kama hicho kutokea hapa TZ

Rais WADE ndiye JK acha ushabiki wewe.
 
Tutamuacha aombe lakini tutamuadhibu this time kwa kura!!akiambulia kura zinazofaa kuhesabika,zitakuwa za wazee wa Dar es salaam!!!!
 
Nampenda sana kikwete, hata akiwa Rais mara 10 yaani awe tu, niko radhi kabisa. usiniulize kafanya jambo gani jema ktk nchi hii sitakuambia hata moja, ingawa simaanishi kuwa hakufanya mazuri ktk utawala wake, wala simchukii kwa7bu ya mabaya yake, hapa pia simaanishi kwamba hana mabaya ktk uongozi wake! pengine 7bu za kumchukia zipo lakini me simchukii bali nampenda jamani huyu mtu pasi na 7bu, yaani nampenda tu....!!

Hata mimi nampenda wasiompenda wajinyonge babu weeeeeeeeeeee Jk katunyanyua wanawake hakuna Rais kama yeye japo mfumo dume bado umetuzingira.
 
Hell NO, hata kumtoa kwa mtutu tutamtoa, utumbo aliotufanyia unatosha. Bora nchi isiwe na Rais kuliko kuwa na Kikwete.
 
katiba hairuhusu...period.

Unaleta dhihaka za ushindani wa chadema na CCM huna hoja hapa.

aseme anang'atuka wakati katiba iko wazi? katiba imeweka kikomo kwa nini aseme anang'atuka?

Nani kasema katiba mpya itakuwa na vipindi vitatu? JK kasema katiba mpya itakuwa tayari April 26, 2014 siku ya kuadhimisha miaka 50 ya Muungano wa Tanzania. hapo ni mwaka mmoja kabla ya uchaguzi muda wa kuongeza kutawala utatoka wapi

Sio dhihaka mkuu....inapoundwa katiba mpya ile ya zamani (inayomfunga kugombea vipindzaidi ya 2) inaacha kutumika, hivyo kwa mwanya huo- anautumia Rais Wade, na kuwepo kwa katiba mpya anaweza gombea kama candidate mpya kabisa.....labda ktk vifungu vya katiba hio mpya iweke bayana kuwa rais analiyemaliza utawala wake- yaani JK..hatoruhusiwa kugombea ktk uchaguzi wa mwaka 2015.......think again mkuu weka chuki yako pembeni mkuu na angalia hoja pamoja na uwezekano wa kutokea jambo hili hapa bongo......mifano hai tunayo kama inavyotokea hivi sasa Senegal..na ilivyokua Uganda jkwa M7 na Zimbabwe kwa mbabe Mugabe kama siokosei
 
Back
Top Bottom