JK afagilia Jitolee Tanzania | JamiiForums | The Home of Great Thinkers

Dismiss Notice
You are browsing this site as a guest. It takes 2 minutes to CREATE AN ACCOUNT and less than 1 minute to LOGIN

JK afagilia Jitolee Tanzania

Discussion in 'Habari na Hoja mchanganyiko' started by BabuK, Nov 29, 2011.

 1. BabuK

  BabuK JF-Expert Member

  #1
  Nov 29, 2011
  Joined: Jul 30, 2008
  Messages: 1,847
  Likes Received: 69
  Trophy Points: 145
  RAIS Jakaya Kikwete amesema mpango wa Jitolee Tanzania unaowatuza Watanzania walioonesha moyo wa kujitolea katika jamii zao, ni ishara tosha kuwa Watanzania wanatambua
  maana ya kuishi kama Watanzania na dhana ya kushirikiana katika kujenga taifa la watu wanaoheshimiana na kusaidiana.

  Amesema nchi haiwezi kuwa na watu wasiotambua shida na kero za wengine, akisema “nchi haiwezi kuwa na jamii zisizokubali kuwa maisha ya watu hutegemeana na hatuwezi kuishi
  kama visiwa ama milima iliyosimama eneo hilo hilo kila siku.”

  Rais Kikwete aliyasema hayo juzi usiku jijini Dar es Salaam wakati alipokuwa mgeni rasmi katika sherehe za kuwapongeza wananchi walioonesha moyo wa kujitolea katika jamii zao.

  Katika hotuba yake iliyosomwa na Naibu Waziri wa Habari, Vijana, Utamaduni na Michezo, Dk. Fenella Mukangara, Rais Kikwete aliwaambia waasisi wa tuzo hiyo kwamba wameanzisha jambo jema linalolenga kuwakumbusha Watanzania wenzao umuhimu wa kukumbukana katika
  shida na raha.

  “Mnachokifanya hapa mnaweza kudhani ni kidogo, lakini kwangu na Watanzania wenzenu tunakithamini sana. Mnatukumbusha tulikotoka, mnatuonesha kwa vitendo tulikopitia na pia mnatufafanulia njia nzuri ambayo tunatakiwa kwenda katika miaka ijayo ya kutathmini uhuru wa Taifa letu,” alisema Rais Kikwete.

  Katika tuzo hizo, waliotuzwa ni pamoja na Fatma Gwao, anayeendesha shule ya yatima na mabibi eneo la Mbagala Dar es Salaam; Evance Tegete ambaye anaendesha shule ya watoto
  walioko katika mazingira hatarishi Dar es Salaam; Juliana Jerry wa Singida aliyesaidia kufanya jamii ya Wahadzabe kuacha kula mizizi na kwenda shule na Anna Lukona wa Morogoro
  ambaye kwa miaka 10 sasa, anaendesha shule ya viziwi.

  Aidha, katika sherehe hizo, mbunge wa zamani na mwalimu mkongwe, Maria Kamm alipewa Tuzo ya Elimu kwa kutambua mchango wake katika maendeleo ya elimu nchini.

  Source: HabariLeo
   
Loading...