Jiunge na mfuko wa afya ya jamii!

Mfumo huu ni mzuri sana, shida ni jinsi unavyotekelezwa. Umewekewa madaraja ambayo mimi naona ni dhambl na ubaguzi. Vitambulisho vya wengine vinaruhusu kutibiwa hospitali zote kwa walioajiriwa na kwa wengine wenye vyeti vyenye rangi fulani hapana.
Kwani ugonjwa wa watu una madaraja ? Bima isibague. Kwa maana wako watu wanachangia na hawaugui hata miaka mitano.
Hii bima wote tuwe na vitambulisho vinavyofanana (kwa watumishi wa serikali ) Na hata hao wa CHF uwepo utaratibu wa usawa.
 
Mfuko huu ni muhimu sana hasa kwa watu wenye matatizo ya ya kudumu / magonjwa sugu ambayo tiba zake ni aghali mno kwa mwezi unakuta m2 anatakiwa dose ya 50000 na zaidi ukiwa na bima hata kama hspt hazipo dawa unapewa form ya kuchukulia dawa hizo katika maduka binafsi, ni kweli hujazipatia hospitali lakini bado hukatoa cash kuzipata.
 
 
Hizi huduma za afya jaman,sio tu kana kwamba wananchi hawazipendi bali wananch wengi hawana uelewa hata kidogo juu ya haya maswala ya bina,ningependa watu humu mfafanue vizuri,manufaa yake,maana NHIF wana nyodo kweli.eti wanataka mwanacha private atoe laki9 hyo kujiunga.na kuchangaia ni 70elfu kila mwezi,je wangapi wangependa ila wanakwama kwasabab ya aina hii ya vikwazo
 
Utaratibu wenu siyo mzuri hasa kwa wategemezi wangu kuniwekea limit kuwa ni mke wangu,watoto wangu,baba na mama wakati mm mpaka sasa sina mke wala watoto na mama kashafariki yupo baba tu.kwa nini msinipe furusa ya kuunganisha ndg zangu wasio na uwezo ili nitumie nao bima yangu ambayo nakatwa kila mwisho wa mwezi????
Bora mngerudisha ule utaratibu wa zamani ili Sisi tusio na wategemezi wa damu pia tuweze kunufaika na NHIF

Kero nyingine ukienda hospitali na hicho kikadi unatazamwa kama mavi na hata dawa ukipata basi ni panadol na kuambiwa zingine ukanunue madukani kwani hapo dawa hakuna.je kwa bali hiyo kuna haja ya kuwa na bima????@acheni kutunyanyasa watumishi kumbukeni kuwa hata Sisi tunakatwa hela siyo makARATASI.
 
Hii inaonyesha hasa ni ubinafsi na kama unajiunga na bima baxi ni vema na ndugu zetu wasio jiweza nao wa ngaliwe na si mpka mfanyazi toka serikalini mjitahidi kuboresha
 
Hiyo kidogo itasaidia na pia somo linatakiwa kwa maana kuna watu wagumu wa kuelewa
 
Hawa jamaa ni wadhaifu kifikra najuuta kuwa mwanachama wao. Wanajua vizur mazingira ya watanzania kuwa wateja wao wengi wako vjjn alafu usajili unafanyka wilayan. Unalipia nauli kuwafuata na bado unatozwa elfu 20000 kwa kumsajili hata mke wako ilhali wanakata fedha zetu kila mwez. Hapa kuna ufisad mkubwa kuliko Escrow
 

Inawezekana wewe nimmoja wafanilia zile ambazo ukitamkaka jina la ukoo unajilikana lakini akina sisi ambao hata nafasi yakitongoji haijawahi shikwa na member waukoo ukifika kupata matibabu dawa unaambia zimeisha kanunue duka la madawa kunahaja gani kuchangia?
 
Last edited by a moderator:
Nipo Mwanza kata ya nyakato. Wilaya ilemela. Naomba kujuzwa ni wapi naweza pata huduma ya kujiunga na CHF. . nishakwenda buzuluga hata wao hawaijui. Pale nyerere road karibu na star times wao wanaijua nhif tu. Wananiambia nilipe laki Tisa+. Mliopo Mwanza nisaidien wapi naweza pata huduma hii. Au contact zao
 
Mkuu hii huduma hapa Dar es Salaam ipo na inapatikana wapi kwa mfano wilaya ya Ilala?
Kwa hapa Dar pia imegawanyika kwa wilaya zote tatu? Naomba unisaidie majibu yake.

Kwa maeneo ya miji inajulikana kama TIKA.
Nenda kwa mganga mkuu wa manispaa utapata ufafanuzi zaidi.
 
Bima hii ikiboreshwa tunaweza kufika mbali katika afya
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…