Jitihada zetu katika kutafuta Maarifa

Shayu

Platinum Member
May 24, 2011
608
1,653
Maendeleo ya binadamu yanategemea sana watu. Watu ndio resource kubwa sana ambayo taifa lolote linalo, Kwa kiongozi mwenye akili atajua jinsi ya kutumia watu vizuri ili kujiletea maendeleo.

Kwahiyo focus kwa kiongozi yeyote yule mwenye akili huwa ni kwa watu. Mapinduzi yeyote yale makubwa katika taifa huletwa na watu.

Kwahiyo ni muhimu kujua tuna watu wa namna gani katika kizazi hiki tulichonacho na tungependa kutengeneza watu wa namna gani , hapo baadae.

Watu ndio nguvu kazi ya jamii yeyote. Sasa inategemea sana . Jinsi gani watu wetu tumewatengeneza kujiletea maendeleo yetu wenyewe.

Hapa ni fikra za watu wetu zikoje kwa taifa lao. Na jinsi gani tutabadilisha mtazamo wao na jinsi wanavyolichukulia taifa lao. Mwelekeo wa akili za watu wetu kwa taifa lao ni muhimu sana. Ni lazima kuwepo na dira kwenye mawazo ya watu wetu kwa taifa lao. Na vitu gani wanataka Ku achieve kama taifa. Maendeleo yetu yanategemea aina ya watu tulionao na mitazamo yao.

Inategemea sana akili na maarifa pamoja na skills za watu wetu na mwelekeo wa watu wetu kwa taifa lao. Pasipo maarifa na skills , Taifa letu haliwezi kuendelea.

Inategemea pia jinsi gani tumejiorganize kuleta maendeleo ya watu wetu.

Bila ushiriki wa dhati wa wananchi wenyewe katika ujenzi wa taifa lao ni vigumu kwa taifa lolote kuendelea. Ni lazima kuwepo na lengo na watu wawe tayari kujitolea maisha yao kulifikia.

Taifa lolote hujengwa katika mioyo na akili za watu. Huo ndio msingi wa kwanza. Kama utaifa hauko kwenye mioyo ya watu basi watu hao sio wamoja.

Taifa huundwa katika umoja katika malengo, na kujitolea kwa dhati kuona taifa likifanikiwa. Kama watu wote watashiriki kwenye ujenzi wa taifa lao watajivunia walicho kijenga.

Kufanikiwa kwa taifa kutakuwa kufanikiwa kwa watu wote sio chama fulani au kikundi fulani cha watu.

Ni muhimu na ni lazima kwanza kulitumikia taifa hili , pili kujenga pride yetu ambayo itakuwa na misingi na values za kufanikiwa kwetu na misingi ya maadili yetu. Ni muhimu na ni lazima tujenge taifa lenye dira na watu wenye malengo kwa taifa lao.

Msingi wa maendeleo ya kizazi kijacho ni lazima ujengwe sasa. Na msingi huu
ni muhimu ujengwe kwenye maarifa na umoja wa watu wetu. Kwa kila mtu kujua wajibu wake kwa taifa lake.

Pasipo maarifa hakuna taifa litakalopiga hatua ya kimaendeleo. Ujinga ni adui wa maendeleo. Jamii yeyote inayotaka maendeleo lazima ikumbatie maarifa kwa nguvu zote na iwafundishe watu wake kati ya sahihi na potofu.

Na watoto na vijana wajue yaliyo sahihi na kuyafuata ni hapo tu kutakuwa na matumaini kwa kizazi kijacho. Jitihada zetu na kufuata yaliyo sahihi zitatufanya tuendelee kama taifa.

Jitihada zetu katika kutafuta maarifa na kuondoa ujinga ni chachu ya maendeleo yetu. Ujinga ni kufanya matendo yeyote ambayo si sahihi yenye madhara kwa binadamu na maendeleo yake. Lakini pia tupate maarifa ya kutengeneza na kugundua vitu kwa maendeleo yetu.

Naendelea kuamini ni maarifa pekee ambayo ni tumaini letu kwa kizazi hiki pamoja na kizazi kijacho. Tutakapoyakataa maarifa na kufuata ujinga taifa letu litaangamia.

Hakuna maendeleo ya binadamu pasipo maarifa na maarifa ni lazima yasaidie jamii kuendelea na sio kuwa na maarifa na kuyaficha.
 

Similar Discussions

Back
Top Bottom