JITAMBUE NA UJIKUMBUKE: Unaweza lolote lile na wewe ndiye mmliki wa dunia. usipojijua hapa hutajijua tena

Kiukweli Mkuu Rakims ndio aliefanya nikajiunga rasmi JF miaka kadhaa iliyopita(ID ile nimeacha nayo). Nilikuwa msomaji tu ila uzi wa "Meditation" ndio ulipoanza nikajiunga rasmi. Hongera mkuu umenisaidia vingi sana mpaka sasa kwenye matumizi sahihi ya ubongo na kiroho.
Mwenyezi Mungu akupe kila lililo na Kheri kwako Brother.
 
Asante sana mkuu
Tupo pamoja

Rakims

Sent from my TECNO KB8 using JamiiForums mobile app
 
Mtiririko wa mawazo yako ni mazuri kwa fikra nyumbulifu nikupongeze kwa hilo ila sikubaliani na fikra za mwanadamu kujikweza juu ya viumbe wenzake kuwa ni mungu wao(mtawala) eti kisa kwa akili zako wajiisi umeumbwa special kuliko wao,

Umeelezea kuusiana na maumbile ya mwanadamu ukioanisha na nyakati,maumbile ya ulimwengu na vilivyomo,upande mzuri na mbaya n.k ambavyo vyote vimepangwa/kugunduliwa au ku-originate kutokana na fikra za mwanadamu hili vitumike na mwanadamu kuweza kuyamudu mazingira yake(hili aweze kuishi yampasa kusaka maarifa)

Pointi yangu ni kuwa kama walivyo viumbe wengine(wasivyojua uwepo wao duniani na purpose) hata mwanadamu ni mjinga kwenye hilo pia
Kama wewe utamzidi bundi au paka kwa maarifa yakibinahadamu kwa kufanya/kuunda vitu kwaajili ya matumizi yako na ukahisi kuwa paka au kuku ataelewa/ku-appreciate ulichofanya ni ujinga

kwa maana kila kiumbe anaishi katika mipaka ya ufahamu wake mwenyewe na kile afanyacho nikulingana na mazingira ya uwepo wake katika ulimwengu huu hivyo wewe na mwewe mnaishi dunia mbili tofauti ndani ya dunia moja kila mmoja wenu akimjaji mwenzake juu ya uelewa wake.
Mwanadamu ni bora kwa lipi ikiwa anakufa kama viumbe wengine?
Ni kiumbe gani mwenye mwili mkubwa(umbo) aliyeumbwa dhaifu kuhimili hostility ya mazingira yake tu ikawa mtihani kama siyo binadamu?

-Kwa maana hiyo akawa na/akatumia uwezo wa kufikiri zaidi hili kuweza kusurvive kama wenzake na siyo kuwa ni bora kuliko wengine wanaoweza kuhisi zaidi,kunusa zaidi,kuona usiku, kukimbia zaidi,kulala kwenye mvua na barafu,kujitafutia au kujitengenezea chakula chao wenyewe kama miti n.k

Ni binadamu tu ndo mwenye hizo 4 Elements na viumbe wengine hawana hizo sifa,Je ni kitu gani mwanadamu anacho cha ziada kuliko hao wanyama?

Itoshe kusema tu kwamba mimi naamini kuwa kila kiumbe yupo tofauti kimaumbile na kiakili katika hali ya msawazo(balanced) inayomfanya aendane na mazingira ambayo ndo chanzo chake na uwepo wake na hiyo akili uliyonayo/au anayokuwa nayo mnyama inawatosheleza wote

na hakuna aliyezaidi ya mwingine mkivaa uhusika wa kila mmoja wenu mtajishangaa kuwa hakuna penye kasoro bali ni kipimo cha kusurvive na kila kiumbe anatafakari usiku na mchana atasurvive vipi na kile kinachotekea kama matokeo ya struggle hii ndo kinachomtofautisha binadamu na miti,wadudu au wanyama kimtizamo,

Wakati ukweli hapo ni kuwa licha ya akili tofauti(mitizamo) kulingana na uwezo waliopewa kimazingira viumbe wote hapo hakuna anayeweza kung'amua fumbo lakuishi pasipo mwenzake/dunia au kuacha kuangaikia kusurvive nakuchange/kushepu ulimwengu kuwa wanachotaka na wasife n.k hivyo wote bado wanaukomo wa maarifa na hawajapiga hatua kubwa katika ufahamu.
 
Yeah hili thread iko ina nyama za kutosha,hongera
 
Habari mkuu, Asante kwa sifa uliyonipa vile vile asante kwa kujaribu kunikosoa maana napenda zaidi wanaonikosoa kwa maana wananipa nafasi either kama sio kuwaelimisha zaidi basi ni kuingia nao mjadala katika kuexpand mind yangu na wao pia,
Nikueleweshe jambo moja baada ya jingine kulingana na hoja zako.

  • Unaposema akili ya mwanadamu ina ukomo kwanza hapo unakuwa umekosea kwa maana ukomo wa akili ya mwanadamu ni pale anaposema kwamba "hili naishia hapa sitaki zaidi", au "wacha mengine niachie wenye kutaka kuendelea nayo" maana yake ni kwamba mwanadamu hana mpaka maalumu wa fikra yake ama akili yake ni hadi pale ambapo alipokadiriwa na muumba wake in case una amini uwepo wa Mungu maana tangu tu umesema tuko balanced unaonekana kurefer kwenye balance of nature(life cicle & dealth) ambayo ni ya watu ambao wapo brain washed kwamba(zaliwa=soma=ajira=oa=zaa=lea=wekeza=kula pension=kufa) hadithi imeisha. tuna sababu ya kuumbwa kwa maumbile haya na tuna purpose ya kuwa hapa duniani.

  • Pili elewa ya kwamba kikubwa alichokadiriwa mwanadamu bora kuliko viumbe wengine ni uwezo wa akili yake(UBONGO) usije kuaminishwa kuna kiumbe duniani ana uwezo wa kukuzidi akili ikiwa unaamini hivyo basi kwenye cicle yenyewe ya neno IMANI haupo.

  • Kuhusu fumbo unalozungumzia elewa ya kuwa binadamu teyari alishafumbuliwa yote yanayohusu dunia mwanzo na mwisho wake na anaakili hiyo ambayo inaweza kumuonyesha mwanzo wake ni upi na mwisho wake ni upi ikiwa wewe bado unatafuta kujua njia yako basi usiifunge akili yako mkuu kuishia hapo uliposema kuwa nanukuu "Mimi naamini (kuamini ni asili ya kiumbe binaadamu akiwa na maana ya kukubali kitu au jambo lipo au ni kweli hasa yale ambayo hana uthibitisho nayo hadi pale yanapotokea. hivyo kwa kusema kila mtu afuate imani ya kila mtu tutajikuta leo tunasali uchi msikitini na kesho kanisani na siku inayofuata tutajikuta tunaabudu chakula kwa maana kinatupa uhai na vilevile tutaamini hata bange ni Mungu. Hivyo usiamini kitu chochote bila uthibitisho kila kitu kinachoaminika basi kimethibitika uwepo wake.
Rakims
 
Mkuu Rakim nakukubali..kuna power tunazaliwa nazo lakini tunazidumaza..Mimi kupitia wewe na kusoma soma nimeanza kuziamsha inner power zangu kupitia meditation na astral projection..
Naanza kujiona tofauti positively..na kwa sasa kila saa 3:30 usiku lazima niamke(wewe unajua maana ya hii)
 
Kuna jambo la kiroho akili yako inakuamsha kufanya muda huo mara nyingi huwatokea watu wenye kufanya ibada usiku

Rakims
 
Reactions: BRN
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…