Jitambue kama un a laana ama hapana.

Bujibuji Simba Nyamaume

Platinum Member
Joined
Feb 4, 2009
Posts
79,036
Reaction score
168,673
Neno la leo linatoka katika kitabu Kitakatifu kilichoandikwa na nabii Yeremia 17: 5-8, nalo lasema hivi:-

5. Bwana asema hivi, Amelaaniwa mtu yule amtegemeaye mwanadamu, Amfanyaye mwanadamu kuwa kinga yake Na moyoni mwake amemwacha Bwana.
6. Maana atakuwa kama fukara nyikani, Hataona yatakapotokea mema; Bali atakaa jangwani palipo ukame, Katika nchi ya chumvi isiyokaliwa na watu.
7. Amebarikiwa mtu yule anayemtegemea Bwana, Ambaye Bwana ni tumaini lake.
8. Maana atakuwa kama mti uliopandwa kando ya maji, Uenezao mizizi yake karibu na mto; Hautaona hofu wakati wa hari ujapo, Bali jani lake litakuwa bichi; Wala hautahangaika mwaka wa uchache wa mvua, Wala hautaacha kuzaa matunda



Mungu atubariki sana, tumtegemee yeye pekee. Tuwasahau waganga na waganguzi, wachawi, hirizi na vile vyote mwanadamu anavyovitegemea kwa nguvu zake mwenyewe.​

 
Bujibuji naona kuna watu una hasira nao.
mi kwa leo siwataji, watakuja hapa kutetea chale na hirizi zao
 
Psalms 1:1-3

blessed is the man that walketh not in the counsel of the ungodly nor standeth in the way of sinners nor sitteth in the seat of the scornfull
2.but his delight is in the law of the LORD;and in his law he meditates day and night
3.and he shall be like a tree planted by the rivers of water that bringeth forth his fruit in his season;his leaf also shall not wither;and whatsoever he doeth shall prosper
 
haleluyaaa haleluyaaa......nyie mnaotumia vigagula.....mtakomajeeeee.......
 
Chimbuvu hapa nimeweka tafsiri ya Kiswahili
[h=1]Zaburi 1[/h]1 Heri mtu yule asiyekwenda Katika shauri la wasio haki; Wala hakusimama katika njia ya wakosaji; Wala hakuketi barazani pa wenye mizaha.
2 Bali sheria ya Bwana ndiyo impendezayo, Na sheria yake huitafakari mchana na usiku.
3 Naye atakuwa kama mti uliopandwa Kandokando ya vijito vya maji, Uzaao matunda yake kwa majira yake, Wala jani lake halinyauki; Na kila alitendalo litafanikiwa.
 
Last edited by a moderator:
Thanx Bujibuji kwa hiyo tukiona sehemu wanaleta mzaha kuhusu watumishi wa MUNGU na MUNGU hatutakiwi kukaa karibu na hayo mazungumzo yao
 
Last edited by a moderator:
Amen and Amen....wewe Asprin acha kutegemea vigagula
Asprin si ni babu? Mi nilidhania ni babu wa umri kumbe ni AMBILIKILE MWASAPILE!!! Asante sana Zion Daughter kwa kunifungua macho. Ndio maana siku ile kwenye mkesha wa maombi cacico alianguka halafu akaanza kutaja Asprin, Asprin, sasa kwa akili yangu ndogo kiroho nikadhani anataka apewe dawa aina ya Asprin ili kumrejesha katika hali ya kawaida, kumbe vilikuwa ni vibuyu vya urithi.
 
hamna kitu Bujibuji umeenda lini kanisani wakati wewe kutwa simba kapakatwa pub pale makumbusho
 
Last edited by a moderator:
Thanx Bujibuji kwa hiyo tukiona sehemu wanaleta mzaha kuhusu watumishi wa MUNGU na MUNGU hatutakiwi kukaa karibu na hayo mazungumzo yao
Dawa ni kukaa nao mbali kabisa. Mungu wetu anaishi, wala hamna haja ya kung'ang'aniza watu waamini kuwa anaishi. Kwa matendo yake makuu watauona utukufu wake, na hakika watakiri huku wakipiga magoti
Warumi 14:10 10 Kwa kuwa imeandikwa, Kama niishivyo, anena Bwana, kila goti litapigwa mbele zangu; Na kila ulimi utamkiri Mungu.
 
Am trying to think loud here....sijui niseme sijui nisiseme! enewei ngoja niulize tu.
Mchungaji Bujibuji, hivi wale raia walioenda kule Loliondo kumtegemea babu, na wale viongozi wa chama na serikali, ndio kusema wamelaaniwa pia?
 
Last edited by a moderator:
Kama hawatatubu kwa MUNGU muumba atawalaani.


Am trying to think loud here....sijui niseme sijui nisiseme! enewei ngoja niulize tu.
Mchungaji Bujibuji, hivi wale raia walioenda kule Loliondo kumtegemea babu, na wale viongozi wa chama na serikali, ndio kusema wamelaaniwa pia?
 
Last edited by a moderator:
wamelaaniwa wale waliokuwa wakikipigia debe kikombe cha babu wa Loliondo.
Amelaaniwa yule aliyepewa ulinzi usio onekana na shehe Yahaya
 

Similar Discussions

Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…